Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujasiri wa Mfia Dini

  Kwa kadiri mtengenezaji wa mambo ya kanisa, yaani Luther alivyoendelea na mafundiso yake walimkusanyikia huku wakiwa na hamu kuu ya kusikia ujumbe wa mbinguni, wakati huo sauti za amani zilimzungumzia kwamba adui zake Waroma wanamkabili. Walisema, “Watakuchoma, na kukuteketeza kabisa uwe majivu, kama walivyomfanya John Huss” Luther akajibu akasema: “Hata kama wakiwasha moto toka Worms mpaka Wittenberg ….. nitapita kati yake kwa jina la Yesu Bwana, nitaonekana mbele yao…. nikimkiri Yesu Kristo”.TU 68.5

  Kufika kwake huko Worms kulileta wasiwasi mkubwa. Marafiki zake walihofia usalama wake, na maadui zake walikuwa na wasiwasi juu ya kusudi lao. Kwa ajili ya chuki na mchocheo wa Kiroma, ilisisitizwa kuwa Luther aende katika makao ya Wakuu ambao ni wa amani, ambavyo kulitangazwa kwamba tofauti zote zimesawazishwa na kuachwa. Lakini marafiki wa Luther walisema kuwa hatari ni kubwa, na hilo ni kubwa. Lakini Luther akitulia bila kutetemeka, alisema “Ingawa waovu wataongezeka katika Worms kama vigae juu ya paa la nyumba, hata hivyo nitaingia humo”.TU 68.6

  Alipoingia Worms watu walijazana ili kumkaribisha. Taharuki ilikuwa kubwa. Luther alisema, Mungu ndiye atakuwa mlinzi wangu.TU 68.7

  Kufika kwake kuliwatia wafuasi wa papa wasiwasi. Mfalme aliwaita washauri wake akawauliza: “Ni hatua gani itakayochukuliwa. Wakadai wafuasi wa papa walisema ‘Tumeshughulikia jambo hili kwa muda mrefu sasa. Hebu, mfalme mtukufu amalize jambo hili kwa kumwondoa mtu huyu asiishi. Je, Sigismund hakutoa amri John Huss akachomwa moto? Hatupaswi kuendelea kumtunza mzushi huyu’ Mfalme akasema” “La, lazima tutunze ahadi yetu”. Ikaamuliwa kuwa mtengenezaji wa kanisa budi asikilizwe.TU 69.1

  Mji mzima ulitamani sana kumwona mtu huyu mashuhuri. Luther alikuwa amechoka na safari ndefu, alihitaji pumziko. Lakini alikuwa amepumzika kwa muda wa saa chache tu, wakati wakuu, mapadri, watu mashuhuri na raia wa mjini walipomkusanyikia. Kati ya watu hao waliokuwamo watu waliomtaka mfalme amlaani na kumtukana Luther. Walio wengi, maadui na marafiki pia walikuja kumwona mtawa huyu jasiri. Alionekana kuwa mtu jasiri. Uso wake ulionekana mtulivu uliojaa furaha. Maneno yake yalikuwa ya kishujaa hasa, hata adui zake walitekewa. Baadhi ya watu walikiri kuwa alikuwa na uwezo wa kimbingu, wengine walitamka kuwa alikuwa na pepo sawa kama walivyotamka kwa Kristo. Yohana 10:20.TU 69.2

  Siku ya pili, mkuu wa serikali alimleta Luther katika jumba la baraza, katika mkutano. Kila mahali palijaa watu waliotaka kumwona mtu aliyethubutu kumpinga papa. Jemadari mzee ambaye alipigana vita vingi na kushinda alimwambia taratibu: “Wewe maskini, sasa uanenda kuamua uamuzi wa ajabu ambao, mimi au jemadari mwingine yeyote hakuufanya katika vita vyetu vya kumwanga damu. Lakini iwepo njia yako ni ya haki …. Endelea mbele katika jina la Mungu, usihofu kitu. Mungu hatakuacha”TU 69.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents