Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Mbele ya Baraza Tena

  Wakati Luther alipofikishwa kwa wakuu tena alikuwa mtulivu bila kuwa na wasiwasi, akiwa na hali ya ujasiri kama mjumbe wa Mungu kati ya wakuu wa nchi. Sasa mkuu wa serikali alitaka atoe uamuzi wake. Je, aliazimia kukana imani yake? Luther alijibu kwa utulivu bila kutumia maneno ya karaha. Hakujitukuza, lakini hali yake ilikuwa imara sana hata iliwashangaza watu wote waliokuwepo.TU 71.3

  Mfalme mtukufu na wakuu mashuhuri Luther alisema “Nasimama mbele yenu leo kama nilivyoagizwa jana. Kama nikikosea kwa ujinga naomba samahani, maana sikukulia katika jamii ya kifalme, ila nilikuwa katika mazingira ya kishambashamba”TU 71.4

  Kisha akaeleza katika baadhi ya maandishi yake yaliyopigwa chapa, ambayo hata adui zake wanayasifu kwamba yafaa, basi kuyakanusa hayo ni kuikanusha kweli ambayo inaaminiwa na watu wote. Sehemu ya pili ya maandishi yake yalikuwa juu ya uovu na udhalimu juu ya Roma ikiongozwa na mapapa. Kuyatangua maandishi haya kutaimarisha na kustawisha udhalimu na uonevu wa Roma na kufungua mlango wa ukaidi wa kutojali mambo matakatifu ya Mungu. Sehemu ya tatu ya maandishi yalikuwa shambulio juu ya watu mmoja mmoja waliokuwa wakiutetea uovu. Kuhusu sehemu hii alikubali kuwa alikosea kushambulia watu kupita kiasi. Lakini hata kuhusu sehemu hii hakubali kuifuta. Maana akiifuta maadui wa ukweli watapata nafasi ya kuwadhulumu watu wa Mungu kwa ukatili mkuu.TU 71.5

  Aliendelea kusema “Nitajitetea kama Kristo alivyofanya. Kama nimesema maovu, hayo yatanishuhudia ….. Kwa rehema za Mungu nakusihi mtukufu mfalme, na ninyi waheshimiwa wote, pamoja na watu wote mnithibitishie kutoka katika maandiko ya manabii, na maandiko ya mitume kwamba nimepotoka. Nikithibitishiwa hivyo kutoka katika Maandiko Matakatifu, nitakuwa tayari kukana na kuungama kila kosa nililolifanya. Nami nitakuwa mtu wa kwanza kuchukua vitabu vyangu na kuvitupa motoni.TU 72.1

  Zaidi ya kuaibishwa, nafurahi kuona kuwa Injili sasa inaleta vita na mafarakano kama ilivyokuwa zamani. Hii ndiyo tabia ya hali ya Neno la Mungu. Yesu Kristo alisema, Sikuja kuleta amani duniani bali upanga….” Jihadharini msije mkasababisha mafarakano kwa kiburi. Mnaweza kulidhihaki neno Takatifu la Mungu, na kutumia nguvu za kutisha kulazimisha mambo kwa uwezo mkuu na kuleta uangamivu wa milele.TU 72.2

  Luther, alikuwa amezungumza katika lugha ya Kijerumani, na sasa alitakiwa aseme maneno yale yale kwa lugha ya Kilatini. Basi aliyarudia maneno yale kwa Kilatini katika ufasaha kamili. Mungu alimwongoza usemi wake. Mara ya kwanza baadhi ya wakuu walipofushwa wasielewe ujumbe wa Luther, lakini aliporudia kusema kwa Kilatini waliona maana yake.TU 72.3

  Wale waliofumba macho yao kwa ukaidi walikasirishwa na maneno ya Luther. Msemaji mmoja alinena kwa hasira. “Hakujibu swali aliloulizwa….. unatakiwa utoe jawabu wazi na dhahiri. Je, utakanusha mafundisho yako au hutayakanusha?”TU 72.4

  Luther alijibu, “Kwa kuwa mfalme mtukufu na waheshimiwa wote mnataka nijibu wazi na dhahiri, nitawajibu hivi: Mimi sitakana imani yangu mbele ya papa wala mbele ya baraza, kwa sababu ni ya hakika kama siku, hata wapinzani wangu wanatofautiana katika maoni. Mimi nisipothibitishiwa kosa la Maandiko Matakatifu,….. sitaikana imani yangu kamwe, maana siyo salama kwa mkristo kusema kinyume cha dhamiri yake. Huo ndio msimamo wangu, siwezi kufanya vinginevyo, Mungu anisaidie. Amen”TU 72.5

  Hivyo ndivyo alivyosimama mtu huyu mwenye haki. Ukuu wake, na ubora wa tabia yake, utulivu wake na furaha ya moyo wake vilidhihirika kwa wote walioshuhudia ukuu wa imani hiyo ishindayo ulimwengu.TU 72.6

  Katika jawabu lake la kwanza Luther alizungumza katika hali ya heshima sana. Waroma walidhania kwamba kukawia kawia kwake kulikuwa kunatayarisha ili akane imani. Charles mwenyewe aliyemwona Luther katika hali hafifu, mdhaifu, mwenye mavazi ya kawaida tu, mwenye usemi wa taratibu sana, “Mtu huyu hatanidhihaki” Lakini ujasiri wake, uwezo wa maneno yake, uliwashangaza wote. Mfalme katika mshangao wake alisema “Mtawa huyu ananena kishujaa bila kutishika na lolote”.TU 72.7

  Wafuasi wa Roma wameshindwa kabisa na sasa wanataka kutumia vitisho ili kurudisha heshima yao iliyopotea. Wameshindwa kimaandiko. Msemaji mmoja alisema. “Kama hutaikana imani yako, mfalme na dola yake watatafuta njia nyingine ya kumfanyia mtu huyu asiyewezekana”. Luther alisema kwa utulivu, “Mungu awe msaada wangu, maana hakuna kitu cha kukana katika imani yangu”.TU 73.1

  Aliambiwa aondoke wakati wakuu walipokuwa wakishauriana. Kuendelea kwa Luther kukataa kukiri kwamba alikosa huenda kukaleta badiliko fulani katika taratibu za kanisa. Basi iliamuliwa kwamba angepewa nafasi moja zaidi ya kukana mafundisho yake. Lakini swali liliulizwa tena kwamba, “Je, angekubali kukana imani yake na mafundisho yake?” Luther akasema, “Mimi sina jawabu lingine kuliko hilo nililojibu”.TU 73.2

  Viongozi wa papa walijawa na chuki na uchungu, kwamba madaraka yao na mamlaka yao yanadharauliwa na mtu tu wa kawaida kama Luther. Luther amezungumza mbele yao kwa ujasiri na utulivu wa Kristo, akasema bila kutapatapa wala kubahatisha. Alijisahau, akasema akiwa mbele ya Mkuu anayewazidi wote hata mapapa, wafalme na watawala Roho wa Mungu amekuwa karibu naye na kuwatia uvuli wakuu wote waliokuwa barazani.TU 73.3

  Baadhi ya wakuu walikubali kuwa maandishi ya Luther ni ya kweli kabisa. Watu wengine hawakusema neno wakati huo, lakini baadaye walimwunga Luther mkono. Mheshimiwa Frederick alisikiliza kwa makini sana usemi wa Luther akikiri kuwa huo ni usemi murua kabisa na akaazimu kumlinda na kumtetea kwa kila njia. Aliona kuwa hekima ya papa na ya wakuu na wafuasi wote wa Roma imeonekana bure kabisa mbele ya ukweli wa Luther.TU 73.4

  Mjumbe wa papa alivyoona matokeo ya usemi wa Luther alikusudia kutumia kila njia ili amwangushe. Alimshawishi kwa njia zote mfalme kijana ili asimwache Luther kuendelea. Siku ya pili yake baada ya jawabu la Luther, Charles alitangaza mbele ya wakuu kuwa anaazimu kuilinda dini ya Katoliki, Akasema kuwa njia zozote zitatumiwa kumpinga Luther na wafuasi wake. Akasema, “Nitaacha utawala wangu, mali yangu, rafiki zangu, mwili wangu damu yangu, roho yangu na uhai wangu ….. Nitaendelea kupingana naye pamoja na Wafuasi wake kama wazushi. Nitatumia kila njia ili kuwaangamiza”. Walakini mfalme alitaka kuwa Luther lazima alindwe kabisa, na lazima arudi kwao kwa usalama.TU 73.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents