Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  1 Utabiri wa Ajali ya Ulimwengu

  Kutoka juu ya kilele cha mlima wa mizeituni, Yesu aliutazama mji wa Yerusalemu. Hekalu lile maarufu lilionekana wazi. Jua la jioni lilitupa miale yake myeupe ya kuta za mawe na marumaru ing'aayo tangu mnara wake wa dhahabu mpaka chini. Mwisraeli ye yote angewezaje kulitazama bila kusifu kwa jinsi iliyvokuwa maarufu! Lakini Yesu alikuwa na mawazo mengine “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia” Luka 19:41.TU 1.1

  Machozi ya Yesu hayakuwa kujililia mweneywe, ingawa mbele yake palikuwa na Getsemane, mahali pa mateso makali yaliomkabili, na Kalwari, mahali pa kusulubishwa pake. Walakini siyoTU 1.2

  mambo hayo yaliyomtia huzuni kiasi cha kulia. Aliwalilia maelfu ambao watafikwa na ajali waliomo Yerusalemu.TU 1.3

  Historia ya miaka elfu ya watu wa Mungu walio wateule, na jinsi Mungu alivyokuwa akiwaangalia kwa huruma nyingi, ilipita katika macho yake Yerusalemu, mji uliotukuzwa na Mungu kuliko yote duniani mwote. “Bwana ameichagua Sayuni …… akae ndani yake”. Zab. 132:13. Kwa muda wa vizazi vingi manabii watakatifu walikuwa wakitoa ujumbe wa maonyo. Damu za kondoo zilikuwa zikitolewa kila siku kafara zikielekeza kwa Mwanakondoo wa Mungu.TU 1.4

  Kama Israeli angedumisha ushirika wake na mbingu, Yerusalemu ungedumu milele, maana ni mteule wa Mungu. Lakini historia nzima ya watu hawa walipendwa na Mungu imekuwa ya uasi tu. Mungu alikuwa amewahurumia watu wake zaidi ya upendo wa Baba kwa mtoto wake. “Kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake” 2Mambo ya Nyakati 36:15. Maonyo na kusihi kote viliposhindwa, aliwatumia kipaji maarufu kabisa cha mbinguni, mwana wa Mungu mwenyewe, ili kushughulikia mji muasi. Kwa muda wa miaka mitatu Bwana na Nuru na utukufu, amekuwa akienda huku na huko kati ya watu wake, “Akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi”. “Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka uliokubaliwa”. “Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema” Matendo 10:38; Luka 4:18; Mathayo 11:5.TU 1.5

  Aliishi kati yao bila kuwa na makao maalumu ili apate kuwasaidia katika hali zao za kuhurumiwa, akiwasihi ili wapate kukikubali kipawa cha mbinguni, ambacho ni cha uzima. Huruma zake nyingi zilikataliwa na waasi hawa kwa masikitiko makubwa. Lakini Israeli alimkataa rafiki yake mkuu na msaidizi wake wa pekee. Kusihi kwake kwa upendo mwingi kumedharauliwa na kukataliwa.TU 2.1

  Muda wa rehema na msamaha ulikuwa unatoweka. Mkusanyo wa ghadabu kwa ajili ya uasi wao, ambao ni wa muda mrefu, ulikuwa umejaa karibu kupasuka juu yao. Yule ambaye ndiye angeweza kuwaokoa na ajali dhahiri iliyokuwa ikiwakabili, amedharauliwa, amekataliwa na karibu atasulubishwa.TU 2.2

  Kristo alipoutazama Yerusalemu na ajali yake ikiukabili, pamoja na taifa zima, aliona maangamizo yake yote kwa ukamilifu. Alimwona Malaika mwenye upanga tayari kuharibu na kuangamiza mji ambao umekuwa makao ya Mungu kwa muda mrefu. Kutokea mahali pale pale alipokuwa akisimama mpaka sehemu yote ya mji ambao baadaye Titus jemadari alisimama pamoja na jeshi lake, alitazama ng'ambo pale hekalu takatifu liliposimama. Machozi yakilengalenga machoni mwake, akiona jinsi kuta za mji zitakavyozungukwa na majeshi ya wageni. Alisikia vishindo vya majeshi vikijipanga kwa vita. Alisikia sauti za akina mama na watoto wao wakililia chakula, wakati mji umezingirwa na majeshi ya adui. Aliona nyumba takatifu ya Mungu ikiteketea katika ndimi za moto, na maangamizo makuu.TU 2.3

  Akitazama mbele katika vizazi vingi aliona watu wa agano na Mungu wakitawanyika katika nchi zote, kama “mavunjiko jangwani”. Huruma za Mungu, upendo usio kifani, unaonekana katika maneno ya maombolezo ya Yesu juu yao. “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uuaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wake, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa yake, lakini hamkutaka” Mathayo 23:37.TU 2.4

  Kristo aliona katika Yerusalemu mfano wa ulimwengu ambao ni mgumu kwa kutokuamini na uasi, nao una haraka kuingia katika hukumu za Mungu. Roho yake ilijaa huzuni kwa ajili ya maangamizo ya nchi. Alitamani kuwaokoa wote. Alikuwa tayari kujitoa kabisa mpaka kifo ili kuwaletea watu wote wokovu.TU 2.5

  Mtukufu wa mbinguni analia! Jambo hilo laonesha jinsi ilivyo kazi ngumu mno ya kumwokoa mkosaji na matokeo ya kuvunja sheria ya Mungu. Yesu aliuona ulimwengu umehusika katika uasi sawa na Yerusalemu ulivyoangamizwa kwa uasi ule ule.TU 2.6

  Dhambi kuu ya Wayahudi ilikuwa ile ya kumkataa Kristo. Dhambi kuu ya ulimwengu ni ile ya kukataa sheria ya Mungu, ambayo ndio msingi wa utawala wake, mbinguni na duniani. Watu mamilioni waliomo dhambini ambao wataangamia, katika mauti ya pili watakataa kusikia ukweli katika wakati wao wa wokovu.TU 2.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents