Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Alindwa Hatarini

  Mara nyingine tena wajumbe wa papa walidai kwamba Luther asipewe ulinzi. Wakasema “Mto wa Rhine budi upokee majivu yake kama ulivyopokea majivu ya Joh Huss”. Lakini wakuu wa Ujerumani, ingawa walikuwa adui wa Luther, hawakukubali dhana hiyo. Walikumbusha kuhusu fujo na maafa yaliyotokana na kifo cha Huss. Hawakutaka Ujerumani irudie kupata maafa ya namna hiyo mara ya pili.TU 74.1

  Charles katika jawabu lake kuhusu madai ya wajumbe wa papa, alisema “Ingawa wenye imani tofauti wanapaswa kuondolewa mbali ulimwenguni, lakini pia wanapaswa kulindwa na wakuu” Baadaye wajumbe wa papa walimhimiza Charles kama vile Sigsmund alivyomtendea Huss. Lakini Charles alikumbuka mabaya yaliyompata Huss kwa ajili ya imani yake, na msukosuko uliotokana na mambo hayo akasema, “Mimi sitaki kuingia katika hali ya aibu kubwa namna hii kama Sigsimund” Walakini Charles hakuamini ukweli ulipofundishwa na Luther. Hakupenda kuacha njia za mazoea yake na kufuata njia mpya. Kwa kuwa wazee wake waliishi humo, hivyo hata yeye hakutaka kuacha ukatoliki.TU 74.2

  Siku hizi watu wengi huishi katika njia za baba zao. Hatutakubaliwa na Mungu eti kwa kuwa tunaishi kwa mapokeo toka kwa wazee wetu badala ya kuchunguza Maandiko Matakatifu sisi wenyewe. Nuru mpya inayotumulikia lazima tuifuate, ingawa baba zetu hawakuwa nayo.TU 74.3

  Uwezo wa mbinguni ulipita kwa Luther ukawafikia wafalme na wakuu wa Ujerumani. Roho wa Mungu aliwasihi watu katika baraza hilo. Charles V akawa kama Pilato wa amani, akajitoa kufuata anasa za ulimwengu, na kwa kiburi akaukataa ukweli aliopewa.TU 74.4

  Njama za kumwangamiza Luther zilienea mahali pengi, na zikasababisha msukosuko mji mzima. Marafiki wengi wa Luther hali wakitambua ukatili wa kikatoliki waliazimia kwamba Luther asitolewe mikononi mwa Wakatoliki. Watu maelfu walijitolea kumlinda. Milangoni mwa nyumba na katika mahali pa hadhara matangazo yalipigiliwa pote, mengine yakimlaani na mengine yakimuunga Luther mkono. Tangazo moja liliandikwa maneno haya: “Ole wako nchi, akiwa mfalme wako ni kijana” Mhubiri 10:16. Watu wajulikanao kwa ajili ya vyeo au utajiri walimthbitishia mfalme na wakuu kwamba, ikiwa Luther atapatwa na baa lolote, amani ya ufalme itatahayarika, na hata ufalme wenyewe utakuwa hatarini.TU 75.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents