Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  9/Nuru YawashwaUswisi

  Majuma machache baada ya kuzaliwa Luther katika kibanda kidogo cha wachimba madini katika Saxony, Zuric Zwingli naye akazaliwa katika nyumba ya mfuga mifugo katika milima ya Alps. Kwa kuwa alikulia katika mazingira safi ya kawaida, mawazo yake yalianza kutafakari mambo ya Mungu na ukuu wake. Akiwa chini ya bibi yake, alisimuliwa hadithi nyingi za Biblia alizojifunza katika kanisa.TU 79.1

  Alipopata umri wa miaka kumi na mitatu alikwenda katika mji wa Bern, ambako kulikuwa na shule maarufu katika Switzerland. Walakini hapo Bern hatari ilitokea. Watawa waliazimia kabisa kumshawisi ili aingie katika kundi la watawa. Kwa bahati nzuri baba yake alipata habari ya maazimio ya watawa hao. Akaona kuwa maisha ya mwanawe ya usoni hayatafaa lolote, tena yumo mashakani. Kwa hiyo alimwita arudi nyumbani.TU 79.2

  Kijana alirudi lakini hakuridhika na maisha ya kwao kwenye mabonde ya milima. Baada ya muda akaenda Basel na kuanza tena masomo yake. Hapa ndipo Zwingli aliposikia Injili ya neema ya Mungu mara ya kwanza. Wittembach alipokuwa akijifunza Kigiriki na Kiebrania, aliongozwa na Roho kuchunguza Maandiko Matakatifu. Kwa njia hii nuru ya Mungu ikapenya mawazoni mwake. Akatangaza kwamba kifo cha Kristo ndicho fidia pekee ya mwenye dhambi. Maneno hayo yalipenya mawazoni mwa Zwingli, yakawa ndiyo mwanzo wa pambazuko la asubuhi.TU 79.3

  Baadaye Zwingli aliitwa kutoka Basel kufanya kazi ya maisha. Mahali pake pa kazi poliko katika majimbi ya milima ya Alps. Alipowekewa mikono kuwa padri alishughulika na mambo ya kiroho, na kuchunguza maandiko ya kweli ya Mungu.TU 79.4

  Kwa kadiri alivyozidi kuchunguza Maandiko Matakatifu ndivyo alivyozidi kupambanua wazi baina ya ukweli na uzushi wa Roma. Alijitolea kuamini Biblia kama Neno la kweli la Mungu, ambalo linatosha kuongoza watu. Aliona kuwa halina haja ya maelezo zaidi, maana lenyewe linajieleza. Alitafuta kila njia ya kumsaidia ili aelewe bila kupotoshwa. Aliomba Roho Mtakatifu amsaidie. Aliandika akasema “Nilianza kumwomba Mungu anipe nuru yake, halafu Biblia iliniwia rahisi kuelewa”.TU 79.5

  Mafundisho ya Biblia Zwingli aliyofundisha hakuyapata kwa Luther. Aliyapata kwa Kristo. Mswisi huyu aliandika na kusema “Kama Luther anamhubiri Kristo, anafanya kama vile nifanyavyo….TU 79.6

  Kamwe hakuna neno lolote nililoandika kwa Luther, wala Luther kwangu ambalo linahusu wokovu. Kwa nini? Kwa kuwa mahubiri ya Luther na ya kwangu yote huongozwa na Roho Mtakatifu na wala hayatofautiani kwakuwa yanatokea mahali pamoja”TU 80.1

  Katika mwaka wa 1516 Zwingli alialikwa ahubiri katika nyumba ya watawa huko Einsiedeln. Mahali hapa aliacha mvuto bora kabisa kama mtengenezaji wa kanisa halisi. Mvuto huo ulienea katika nchi yote ya kwao, milimani Alps.TU 80.2

  Baina ya mambo makuu ya Einsiedeln ilikuwa sanamu ya bikira, ambayo ilisemekana kuwa ilikuwa na uwezo wa kufanya miujiza. Juu ya lango la nyumba ya watawa palikuwa na andiko lisemalo, “Hapa msamaha kamili wa dhambi hupatikana” Hapo palipohesabiwa kuwa mahali patakatifu watu makundi makundi walitoka pote katika nchi ya Switzerland, ufaransa hata Ujerumani pia, ili kupata msamaha wa dhambi. Zwingli alitumia nafasi hiyo ya kuwatangazia uhuru upatikanao katika Injili ya neema ili kuwatoa katika kifungo cha ushirikina.TU 80.3

  Zwingli aliwaambia “Msidhani kuwa Mungu yumo katika hekalu hili kuliko mahali pengine, je, mambo hafifu haya mtendayo, kama vile safari ndefu kwa ajili ya dini, kutoa sadaka, kuheshimu sanamu za watakatifu, na kadhalika yatawapatia msamaha wa neema ya Mungu? Kuna manufaa gani ya kuvaa kofia yenye kung'aa, majoho maridadi, na mapambao ya aina aina? Kristo aliyetolewa kafara juu ya msalaba ndiye fidia ya dhambi kwa wote wamwaminio milele”.TU 80.4

  Kwa wengi, walitiwa uchungu kuambiwa kuwa matendo yao kama safari ndefu wasafirizo ni za bure. Hawakuweza kuelewa maana ya msamaha wa dhambi kwa njia ya imani katika Kristo. Walitosheka tu na njia zile za Roma ilizowapangia. Kwao waliwatumaini mapadri na papa ili wawapatie ukombozi wala hawakujishughulisha na usafi wa moyo.TU 80.5

  Lakini watu wengine walipokea habari ya wokovu kwa njia ya kumwamini Kristo kwa furaha kuu. Kwa imani wakapokea damu ya Kristo kuwa ndiyo njia ya kuwapatia wokovu. Watu hawa walirudi makwao wakawatangazia wenzao habari njema hii aliyoipokea. Kwa njia hii ukweli ulienea toka mji mpaka mji mwingine. Hesabu ya wasafiri waliokuwa wanamwendea bikira ikapungua. Hivyo matoleo yalipungua, hata mshahara wa Zwingli pia ukakatwa, maana ulitokana na matoleo hayo. Lakini jambo hili lilimfurahisha kwa kuona uwezo wa ushirikina unavunjika. Ukweli ulizidi kushikwa na watu wengi.TU 80.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents