Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Zwingli Aitwa Kwenda Zurich

  Baada ya kupita miaka mitatu, Zwingli aliitwa ili akahubiri katika kanisa kuu la Zurich, ambao ni mji maarufu sana katika Uswiss. Mvuto ambao ungeonyeshwa hapo ungeenea sana. Makasisi hawakukawia kumwongoza kuhusu kazi zinazompasa. Wakamwambia: “Utafanya bidii sana kukusanya mapato ya wakuu wa kanisa, bila kuachia hata kidogo kidogo…… uangalie sana kuongeza mapato katoka kwa wagonjwa, na kwa waabudu na kutoka katika huduma ya makasisi” “Kuhusu usimamizi wa huduma ya pasaka, na mahubiri, na utunzaji wa kundi …. Unaweza kubadili mambo hasa mafundisho unayohubiri”.TU 81.1

  Zwingli alisikiliza maagizo hayo kwa utulivu, kisha alijibu “Maisha ya Kristo yamefichika kwa watu siku nyingi sana. Mimi nitahubiri Injili ya Mathayo yote kama ilivyo ….. Huduma yangu itakuwa lengo la kumtukuza Mungu, na kumtukuza Mwana wake Yesu Kristo, na kudhihirisha njia wazi ya wokovu, na imani ya kweli inayotakiwa”.TU 81.2

  Watu walimiminika ili kusikia mahubiri yake. Alianza huduma yake kwa kufundisha mambo ya Injili zote, na kueleza habari za maisha na kazi ya kifo cha Kristo. Akasema. “Mimi nia yangu ni kuwaogozeni kwa Kristo ambaye ndiye asili ya wokovu.” Watu wataalamu wakuu, wenye elimu, na wakulima walimsikiliza Zwingli kwa makini. Aliyalaani maovu yanayotendwa na kanisa la Roma wazi wazi bila hofu. Wengi walikuwa na furarha na kumtukuza Mungu kwa mahubiri hayo. Walisema “Mtu huyu ni mhubiri wa ukweli. Atakuwa mkombozi wetu kama Musa, atakayetuongoza kutoka katika giza la Misri” Baada ya muda upinzani ulitokea. Watawala walimshambulia kwa maneno ya dharau wakimcheka na kumdhihaki. Wengine walikuwa wakimwendea na kumfanyia ufedhuli na kumtisha. Lakini Zwingli aliyavumilia yote hayo.TU 81.3

  Mungu anapoandaa kuvunja pingu za ujinga na ushirikina, shetani naye hujitahidi sana kuwafunga watu wakae gizani. Roma ilijitahidi mno kueneza masoko yake ya kuuzia vyeti vya msamaha wa dhambi. Waliweka viwango mbalimbali vya dhambi na bei yake. Kama hazina ya kanisa ilikuwa imejaa vyeti vya msamaha wa dhambi vilitolewa bure. Kwa hiyo misimamo miwili ilikuwa inaendelea kusambaa: Roma inauza vyeti vya kusamehewa dhambi na kujaza hazina yake na Watengenezaji wa Kanisa wakilaani dhambi na kuwaelekeza wenye dhambi kwa Kristo ambaye ndiye mwokozi waoTU 81.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents