Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mabishano Pamoja na Roma

  Wafuasi wa Roma walipoona kuwa mateso hayakufaulu kuvunja mafundisho ya Luther katika Ujerumani, waliazimia kushindana na Zwingli. Walihakikisha ushindi wao kwa njia ya mabishano ya wazi na kwa kuchagua waamuzi ambao wangeamua ukweli ulivyo. Kama wangemshinda Zwingli wangehakikisha kuwa asingeponyoka toka mikononi mwao. Kusudi hili walilificha kabisa.TU 83.2

  Mahojiano yalipangwa yafanywa huko Baden. Lakini baraza la Zurich likishuku juu ya makusudio ya mapapa na kwa kuhadharishwa na wingi wa marundo ya kuni ya kuchomea wanaofuata imani ya watengenezaji wa kanisa, walimzuia mchungaji wao asijihudhurishwe kwenye mahojiano hayo ya hatari. Kwenda Baden, ambako damu za wafia dini wengi zimemwagwa, hakika ilikua kwenda mautini. Oecolampadius na Haller walichaguliwa wakamwakilishe Zwingli katika mabishano hayo na Dr. Eck alikuwa akiitetea Roma huku akiungwa mkono na wataalamu na makasisi wengi.TU 83.3

  Waandishi wa mambo hayo wote walichaguliwa na Roma na wengineo wote walikatazwa kuandika lolote au sivyo, wangepata adhabu ya kifo. Walakini wanafunzi waliohudhuria waliandika mambo hayo kila siku jioni baada ya maojiano. Maneno hayo yaliyoandikwa na yalitumwa kwa Zwingili kila siku na wanafunzi wawili, pamoja na barua za Oecolampadius. Kila siku Zwingli alijibu na kutoa ushauri. Ili kuepa udhia wa walinda mlango, watu hao walikuwa wakibeba makapu ya kuku, kwa hiyo walikuwa wakiruhusiwa kupita bila taabu.TU 83.4

  Myconius alisema “Zwingli amefanya mengi zaidi kwa njia ya maombi, na kukesha, pamoja na kushauri kuliko vile ambavyo angehojiana na adui zake uso kwa uso”TU 84.1

  Warumi walihudhuria huko Baden katika mavazi yao rasmi na taji zenye kung'aa vichwani mwao. Vyakula vyao vilikuwa vya kianasa kabisa. Kinyume cha hayo walionekana watengenezaji wa kanisa wakiwa katika hali ya kawaida, na chakula chao cha kiasi tu. Mwenye nyumba waliyokuwa wakikaa alikuwa akimtembelea Oecolampadius mara fulani fulani, na kila mara alimkuta akisoma, au akiomba. Taarifa aliyotoa alisema, “Mtu huyu mzushi ni mcha Mungu sana”TU 84.2

  Kwenye mkutano, Eck alipanda madhabahuni kwa kiburi, huku akiwa amevalia rasmi kabisa, mavazi yenye kumetameta na wakati ule ule mnyenyekevu Oecolampadius akiwa na nguo zake za kawaida tu, alilazimika kuketi juu ya kiti kidogo mbele ya mpizani wake. Eck mwenye sauti ya ngurumo alikuwa na hakika ya kufaulu. Mtetea imani angekuwa atunukiwe hadhi ya utaalamu. Kama majadiliano ya kawaida yangeshindikana, aliazimu kutumia matusi hata kuapiza.TU 84.3

  Oecolampadius mpole, mwenye kujitumaini aliyakimbia mashindano. Ingawa ni mpole, jasiri mwenye nia thabiti alijithubutisha kuwa mtu imara asiyenyumbayumba. Mtengenezaji wa kanisa aliambatana na Maandiko matakatifu. Alisema “kawaida tu, hazina nguvu katika Uswissi, isipokuwa zinaambatana na katiba. Lakini kuhusu mambo ya imani, Biblia ndiyo katiba yetu”TU 84.4

  Hoja za kweli za mtengenezaji wa kanisa, zilitolewa kwa utulivu, ziliwaingia watu waliokusanyika, wakayadharau maneno ya Eck ya majivuno matupu.TU 84.5

  Majadiliano yaliendelea siku kumi na nane. Wafuasi wa papa wakadai kuwa wameshinda. Wakuu wengi waliunga Roma mkono. Wakatangaza kuwa wafuaasi wote watengenezaji wa kanisa pamoja na Zwingli wameharamishwa na kufutwa kanisani. Lakini mashindano yalikuwa matokeo ya mvuto wa kuendelea katika njia ya upinzani. Muda haukupita, miji mashuhuri ya Bern na Basel ikajitangazia kuunga mkono matengenezo ya kanisa.TU 84.6

  Marejeo: TU 84.7

  Wylie, bk. 8. ch. 5 TU 84.8

  ibid bk. 8, ch. 6 TU 84.9

  D'Aubigne bk. 8 ch. 9 TU 84.10

  Ibid. bk. 8 ch. 9 TU 84.11

  Ibid TU 84.12

  Ibid bk. 8, ch. 6 TU 84.13

  Ibid. TU 84.14

  Ibid. bk. 8 ch. 9 TU 84.15

  Wylie bk. 8 ch. 11 TU 84.16

  D'Aubigne bk. 11 ch. 13 TU 84.17

  Ibid.TU 84.18

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents