Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  10/Maendeleo Katika Ujerumani

  Kutoweka kwa Luther kwa siri kuliwataharukisha na kuwatia hofu watu wote wa Ujerumani. Uvumi mwingi ulitokea, na wa watu wengi waliamini kuwa ameuawa. Maombolezo mengi yalitokea na watu wengi walifunga kwa kiapo kwamba watalipiza kwa kifo chake. Ijapokuwa adui zake walifurahi hapo mwanzo kwa kudhania kuwa Luther amekufa, lakini baadaye walifadhaika kujua ya kuwa amefungwa tu, wala hakufa. Mmoja wao alisema, “Kitakachotuokoa ni kumtafuta kwa bidii mahali popote duniani, tumlete katika nchi maana taifa zima linamhitaji”. Habari za kwamba Luther yu hai, tu analindwa mahali fulani, ziliwatuliza watu. Na maandiko yake yaliyopokelewa watu waliyasoma kwa hamu kuliko hapo mwanzo. Watu wengi walizidi kujiunga na shujaa huyu aliyelitetea neno la Mungu.TU 85.1

  Mbegu zilizopandwa na Luther ziliota kila mahali. Kutokuonekana kwake kulitimiza mengi ambayo yasingalitimizwa na kuwako kwake. Na sasa kwa kuwa kiongozi wao mkuu ameondolewa, budi wengine waendeleze kazi hiyo iliyoanzishwa isije ikazuilika.TU 85.2

  Sasa Shetani alijaribu kuingiza kazi hiyo, kwa kuharibu misingi ya kweli na kutia mambo bandia. Kama vile kulivyozuka manabii wa uongo katika karne ya kwanza vivyo hivyo hata katika karne ya kumi na sita walizuka.TU 85.3

  Watu wachache walijidai kuwa wamepata ufunuo kutoka mbinguni ili waendeleze kazi ya matengenezo ya kanisa, ambayo walidai kuwa ilianzwa kwa unyonge na Luther. Kwa hakika hawakufanya kazi iliyofanywa na Luther na kukamilisha. Wao walikataa kanuni za utengenezaji, kwamba neno la Mungu ndilo mwongozo wa imani na maisha budi kufuatana nalo. Walipoacha neno la kweli la Mungu wakajiwekea kanuni zao zisizo za hakika kwa kufuata maoni yao.TU 85.4

  Wengine ambao kwa asili ni watangatangaji walijiunga nao. Watu hawa waliendelea vikubwa sana, na kuleta msisimko mkubwa. Luther alikuwa amewaamsha watu na kuwaweka katika matengenezo kamili, lakini sasa watu hawa wamepotosha watu wa kweli wa Mungu. Wao ni manabii wa uongo.TU 85.5

  Viongozi wa kundi hili walitupa madai yao juu ya Malancthon, wakisema, “Tumetumwa na Mungu kufundisha watu, tumekuwa na maongezi na Bwana tunafahamu matokeo yake, Sisi ni mitume na manabii. Walimtaja Luther awe mmoja wao.”TU 85.6

  Watengenezaji wa kweli walitatanishwa. Melanchthon alisema, “Katika watu hawa, kwa kweli kuna roho nyingine ndani yao. Lakini ni roho ya aina gani hiyo? Kwa vyovyote tujitahadhari tusije tukakufuru Roho wa Mungu, pia tujihadhari tusije tukapotoshwa na roho wa Shetani”TU 86.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents