Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matunda ya Mafunzo Yadhihirika

  Watu waliongozwa kinyume kabisa. Walifundishwa kutojali Biblia isemavyo, au kushika Biblia kidogo tu. Wanafunzi wakitupilia mbali vizuizi vyote, walitoka katika vyuo vilivyokuwa vikiwapa mafunzo, wakaendeleza mbele kazi ya matengenezo, ndiyo walioiharibu na kuangamiza. Sasa Waroma walijipa moyo, na kusema kwa majivuno “Shambulio moja tu la nguvu, na wote watakuwa mateka wetu”.TU 86.2

  Luther akiwa huko Wartburg aliposikia mambo yaliyotokea alisema kwa kusisitiza “Mimi kila mara nilitazamia kuwa shetani atatuletea tauni hii.” Alifahamu tabia ya kweli ya hao waliojifanya kuwa manabii ilivyokuwa. Upinzani wa hao waliojifanya kuwa manabii ilivyokuwa. Upinzani wa papa na wa falme haukutetea wasiwasi kama ilivyo hivi sasa. Kutokana na watu waliojifanya kuwa marafiki wa watengenezaji wamezuka maadui wakali zaidi walioleta machafuko na matatizo katika kazi hii.TU 86.3

  Luther alikuwa amesukumwa na Roho wa Mungu kuendesha kazi hii, naye alifanya. Walakini alitetemeka kwa matokeo ya kazi yake. Alisema, “Kama ningalijua kuwa kazi yangu ingemwumiza hata mtu mmoja tu ingawa awe mdogo ambavyo sivyo, maana ni Injili yenyewe, ingekuwa bora mara kumi mimi nife, kuliko kupotosha, na kupotoka”.TU 86.4

  Mji wa Wittenberg wenyewe umeangukia katika udhalimu na machafuko. Maadui wa Luther walikuwa wakimlaumu Luther aliuliza kwa uchungu, “Je, hayo yaweza kuwa ndiyo mwisho wa kazi hii kubwa ya matengenezo ya kanisa?” Lakini alipokuwa akimlilia Mungu kwa njia ya sala, amani ilijaza moyo wake. Alisema “Kazi hii siyo yangu, bali ni kazi yako” Lakini aliazimu kurudi huko Wittenberg.TU 86.5

  Alikuwa amezuiliwa na utawala. Adui zake walikusudia kumwulia mbali, nao walikuwa huru kufanya hivyo. Rafiki zake walikatazwa kumlinda au kumsaidia. Lakini yeye aliona kuwa kazi ya Injili inahatarishwa. Kwa hiyo akatoka kwa jina la Bwana bila hofu akaitetea Injili. Katika barua aliyomwandikia mtawala, Luther alisema “Ninakwenda Wittenberg chini ya ulinzi mkuu kuliko ule wa wakuu na watawala. Sifikiri kukuomba msaada wa ulinzi, lakini badala yake mimi natamani kukulinda. Hakuna silaha itakayoendesha kazi hii. Mungu pekee yake ndiye awezaye kuifanya.” Kutoka barua ya pili Luther, alisema, “Mimi niko tayari kushutumiwa na wewe, ee mfalme, na kukasirikiwa na ulimwengu wote, je, watu wa Wittenberg sio kondoo zangu? Nami hainipasi kufa kwa ajili yao ikilazimu?”TU 86.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents