Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maumivu Ya Roho Yaliwekwa Juu ya Luther

  Wafuasi wa papa walitangaza kuwa maasi yote yaliyotokea yametokana na mafundisho ya Luther. Malaumu hayo hayakumhuzunisha Luther sawa na kule kuhesabu ukweli aliohubiri kuwa sawa na upotovu wa hawa washupavu wa dini. Waongozi wa kundi hili walimchukia Luther. Luther hakuyakanusha mafundisho yao tu, bali pia aliwalaumu kwa ajili ya maasi yao juu ya wenye mamlaka. Wao nao walimwita kuwa mtu mwovu ajifanyaye mfuasi.TU 88.3

  Wafuasi wa Roma walikuwa wakitazamia maanguko ya utengenezaji wote wa kanisa. Wakalaumu Luther kwa makosa ambayo anasahihisha kwa juhudi. Wale wapotoshaji walidai kuwa wanatendewa ukatili, na kujihesbu katika kundi la wafia dini, nao waliungwa mkono na Waroma. Wapinzani hao walisifiwa na kuungwa mkono. Hali ilikuwa kazi ya roho ile ile iliyojitokeza mbinguni ambayo ni roho ya uasi.TU 88.4

  Shetani daima anatafuta kuwadanganya watu na kuwaongoza katika upotevu wa kuita dhambi kuwa haki, na haki kuwa dhambi. Maigizo kuwa kweli, kujipendekeza kuwa utakaso. Roho ya namna hiyo ingali inafanya kazi kama siku za Luther, ikiwaongoza watu waende mbali na Maandiko matakatifu, ili wafuate maoni yao na maongozi ya watu, badala ya maongozi ya sheria ya Mungu.TU 88.5

  Luther alitetea Injili bila hofu katika upinzani. Alipigana na udhalimu wa Roma, akitumia Neno la Mungu. Alisimama imara kama mwamba akipingana na upotovu uliotaka kuunganika na kazi ya matengenezo ya kanisa.TU 88.6

  Vikundi hivi vya upotovu, kila kimoja kiliweka Biblia kando, kikatukuza hekima ya binadamu, na kujifanya kuwa kanuni ya dini ya kweli. Waroma wakijidai kuwa walipata utaratibu wao moja kwa moja tokea mitume, madai hayo yalitoa nafasi kubwa kwa ajili ya upotovu na udhalimu ulioingia kanisani kwa kifuniko hicho. Madai ya Munzer ya kwamba amefunuliwa na Mungu ambayo ni ya kipumbavu yaliongeza udhalimu. Ukristo wa kweli huongozwa na Neno la Mungu ambalo ndilo kipimo cha kupima madai ya kila namna.TU 88.7

  Luther aliporudi kutoka Wartburg, alikamilisha kazi yake ya kutafsiri Agano Jipya, na injili katika lugha ya Kijerumani, na mara baadaye watu wa Ujerumani wakapata Neno la Mungu katika lugha yao. Tafsiri hii ilipokelewa kwa shangwe kuu na watu wote walioipenda kweli.TU 89.1

  Sasa makasisi walishindwa kwa kuwa watu wa kawaida wangeweza kuusoma ukweli na kuujadili pamoja nao tena kwamba wangefahamu mambo na kuung'amua ujanja wao wa kijinga na udanganyifu wao. Roma ikawakutanisha wakuu wake wote ili wachukue hatua ya kuzuia Agano Jipya lililotafsiriwa lisitolewe kwa watu. Lakini kadiri walivyozuia Maandiko Matakatifu yasisomwe, ndivyo hamu ya watu ilivyoamshwa ili wachunguze na kuona ukweli ulivyo. Watu wote waliojua kusoma walinunua na kusoma na kukariri mafungu moyoni kwa wingi. Mara moja Luther alianza kutafsiri Agano la Kale.TU 89.2

  Maandiko ya Luther yalipokewa mijini na mashambani katika nyumba za watu. Luther na rafiki zake walipomaliza sehemu fulani, wengine walichukua na kueneza kwa watu. Watu walikubali upigaji marufuku wa vitabu hivi katika nyumba za watawa, lakini waliviuza vitabu vya Luther na rafiki zake, ingawa wenyewe hawakuweza kueleza Maandiko Matakatifu kwa usahihi. Mwisho Ujerumani ilifunikwa na jeshi hili la wauza vitabu.TU 89.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents