Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mafunzo ya Biblia Po Pote.

  Wakati wa usiku walimu wa skuli waliwasomea vikundi vya watu vilivyokusanyika vikiwa kando ya moto wa jioni. Kwa njia mbali mbali watu waliongolewa. “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga” Zaburi 119:130.TU 89.4

  Wafuasi wa Roma, mapadri, makasisi wote waliitwa ili kila mtu awe tayari kukanusha mafundisho haya mapya. Lakini wakiwa gizani kabisa kukanusha mafundisho haya mapya, bila ujuzi wo wote wa Biblia walishindwa kukanusha ukweli huu. Mkatoliki mmoja aliandika, akiwa na masikitiko “Luther amewashawishi wafuasi wake wasiamini kitu kingine ila Maandiko Matakatifu peke yake” Watu waliweza kukusanyika ili kumsaikiliza mtu wa kawaida tu asiye na elimu ya juu, akiwahubiri. Aibu kubwa iliwapata watu maarufu, walipohojiana na watu wadogo walio na ukweli wa Neno la Mungu na kushinda vibaya, Vibarua askari, wanawake hata na watoto walifahamu Biblia kuliko makasisi na wataalamu.TU 89.5

  Vijana wenye mawazo mazuri walijitoa kujifunza Biblia, wakichunguza maandiko na sehemu mbalimbali za Biblia ili wazoee na mafungu mbalimbali. Vijana hawa walikuwa waelekevu sana, na mioyo yao ilizingatia maneno mengi ya Maandiko, hata haikuwezekana kuwashinda. Watu waligundua katika mafundisho mapya haya mambo yale ambayo mafunzo ya Roma hayakuweza kuwatosheleza. Nao waliyatupilia mbali mambo yale ya Roma ambayo yalikuwa ya bure, yaliyojengwa kwa hadithi za biandamu.TU 90.1

  Wakati mateso yalipotokea juu ya walimu hawa wa kweli hawakuyajali, ila walilishikilia neno la Mungu. “Watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine” Mathayo 10:23. Basi wakimbizi hawa wakapata mahali fulani wenye huruma wakawapatia msaada, na hao wakaendelea kumhubiri Kristo. Mahubiri yao pengine yalifanywa nyumbani au kanisani au uwanjani, ukweli ukaenea kwa nguvu ya ajabu.TU 90.2

  Wakuu na watawala walijitia kuwatesa, kuwafunga, kuwachoma moto, lakini yote ilikuwa kazi bure. Watu maelfu walifunga maisha yao kwa damu zao wenyewe. Walakini mateso yalizidi kueneza injili tu. Wale watu wapotevu ambao shetani aliwaingiza ndani walidhirisha tu na kupambanua ukweli wa Mungu na uongo wa shetani.TU 90.3

  Marejeo: TU 90.4

  D'Aubigne, bk. 9, ch. 1 TU 90.5

  Ibid. bk. 9, ch. 7 TU 90.6

  Ibid. TU 90.7

  Ibid. TU 90.8

  Ibid, bk. 9 ch. 8 TU 90.9

  Ibid. TU 90.10

  Ibid. bk. 10 ch. 10 TU 90.11

  Ibid. bk. 9 ch. 8 TU 90.12

  Ibid. bk. 10 ch. 10 TU 90.13

  Ibid. bk. 9, ch 11 TU 90.14

  Ibid.TU 90.15

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents