Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Msimamo Bora wa Wakuu

  Mfalme Fredinand mwakilishi wa mfalme mkuu alijaribu kutumia mvuto wa ushawishi. Aliwaomba wakuu waikubali amri iliyotolewa akiwahakikishia kuwa hata mfalme mkuu atapendezwa. Lakini watu hawa waaminifu walijibu kwa uthibiti wakisema “Tutamtii mfalme kwa kila jambo lenye kuleta amani na lenye kumtukuza Mungu”TU 93.1

  Mwishowe mfalme alitangaza kwamba jambo lililobakia ni kufuata wingi wa watu. Baada ya kusema hivyo aliondoka bila kuwapa watengenezaji nafasi ya kujibu. Walituma ujumbe kwake, wakimwomba arudi. Yeye alijibu, “Imeamuriwa kufuata kama ilivyoamuriwa ndilo jambo lililobaki”TU 93.2

  Wajumbe wa serikali walijivuna wenyewe kwamba shauri lao na la papa limefaulu na kuwa mambo ya watengenzaji yameshindwa. Kama watengenezaji wangelitegemea msaada wa kibinadamu peke yake, mambo yao yangalikuwa kazi bure, kama wafuasi wa papa walivyodhani. Lakini wao waliomba kutoka katika taarifa ya baraza kuhusu neno la Mungu na kuhusu mfalme Charles kwa Yesu Kristo, mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.TU 93.3

  Kwa vile Ferdinand alikataa kutambua haki ya imani ya dhamiri zao, watawala waliamua kuendelea na mipango yao bila kujali kutokuwako kwake. Hasa kuleta maazimio ya mbele ya baraza la taifa bila kuchelewa. Basi tamko rasmi lilitayarishwa na kuletwa mbele ya baraza. Tamko lilisema, “Sisi tunapinga azimio au amri iliyotolewa pamoja na jambo lolote ambalo ni kinyume cha Neno la Mungu, kwamba hatutakubaliana nayo kwa ajili yetu wenyewe, na watu wetu kwa ajili ya wokovu wa roho. Tunapinga hayo kwa ajili ya uhuru na haki ya dhamiri zetu. Kwa hiyo tunakataa kutiwa chini ya kongwa. Na wakati ule ule matazamio yetu ni kwamba mtukufu mfalme atatufikiria kwa wema kama mkristo na mjumbe wa Mungu anayempenda kuliko kitu kinginecho; na sisi tunatamka rasmi kuwa tuko tayari kujitoa kwake kamili na kwako, tukiitii na kutumika na kutoa upendo wetu kwa kila kazi njema. Hivyo ndivyo haki na wajibu wetu”TU 93.4

  Wengi walishangaa kwa ujasiri wa hawa wapingaji. Ikaonekana kuwa, mafarakano na ugomvi na kumwagika kwa damu vitatokea. Lakini watengenezaji huku wakimtegemea Mungu walikuwa watulivu na wenye moyo mkuu.TU 93.5

  Kanuni zilizokuwamo katika maazimio haya ya upingaji wa dhamiri kuliko mahakama, na uwezo wa Neno la Mungu kuliko maagizo ya kanisa. Manabii na mitume wanasema, taji ya mfalme Charles V waliinua taji ya Kristo. Wale wapingaji wa Spires walikuwa mashahidi halisi na watetea dini kweli, waliotafuta uhuru wa dini ili kila mtu amwabudu Mungu kufuatana na dhamira yake.TU 94.1

  Hali ya watengenezaji hawa na kanuni zao hutoa fundisho kwa wote kwa vizazi vijavyo. Shetani angali anapinga Neno la Mungu ambalo ndilo kiongozi halisi maishani. Katika siku zetu hizi kuna haja ya kurudi na kusimama katika kanuni za watengenezaji hao, yaani, Biblia na Biblia peke yake, ndiyo mwongozo katika mambo yote. Shetani angali anajitahidi kuharibu uhuru wa dini. Uwezo wa wapinga Kristo kama ule wa Spires unatafuta njia ya kujiimarisha sasa, kuuimarisha uwezo ule ulioangushwa na watu wa Spires.TU 94.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents