Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  12/Kwapambazuka Ufaransa

  Upinzani wa Spires na ungamo la Augsburg vilifuatiwa na miaka ya mapambano makuu na machafuko kabisa. Uprotestant ukiwa umedhoofishwa na mafarakano, ulionekana ukielekea kufa.TU 97.1

  Mfalme akitazamia kuwa atafaulu, ndipo kushindwa kwake kulimtokea ghafla. Mwishowe alilazimika kukubali kupitisha ushindi wa mafundisho aliyokusudia kuyaharibu tangu zamani. Aliona majeshi yake yakiangamizwa katika vita, hazina zake zikikaushwa na sehemu kubwa ya nchi yake ikikabiliwa na uasi, ambavyo imani ile aliyochukia na kuipinga ikizidi kustawi na kufanikiwa. Charles V amekuwa akijaribu kupigana na mwenyenzi na uwezo wake. Mungu alikuwa amesema “Na iwe nuru”, lakini mfalme alikuwa amedumisha giza. Akiwa amedhoofishwa na mapambano ya muda mrefu, mwisho alijiuzulu kiti chake cha enzi, akajikalia kama mtawa.TU 97.2

  Katika Uswisi, wakati wengi walipoipokea imani ya Watengenezaji, wengine waling'anga'ania imani ya Rumi. Mateso yaliyokuwepo yalisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Zwingli na wengine wengi ambao walijiunga na watengenezaji waliangukia katika vita na kumwaga damu vilivyokuwa vikipiganwa huko Cappel. Rumi ilikuwa ikishinda, na mahali pengi ilionekana kwamba inarudisha mali yake iliyotekwa. Lakini Mungu hakuwa ameachilia mbali kazi yake na watu wake. Katika nchi nyingine Mungu aliamua watendakazi wengine ili waendeleze kazi ya matengenezo.TU 97.3

  Katika ufaransa aliyepata nuru mara ya kwanza alikuwa Lefevre, aliyekuwa mwalimu mtaalamu katika chuo kikuu cha Paris. Katika uchaguzi wake wenye maandiko ya zamani, aligundua Biblia, na akaanza kuwafundisha wanafunzi. Alijishughulisha na historia ya watakatifu na wafia dini kama ilivyonakiliwa na kanisa. Naye alikuwa ameendelea sana, katika uchunguzi huo, ndipo wazo lilipomjia la kutafuta msaada wa Biblia juu ya habari hiyo. Basi akaanza kuisoma na kuichunguza. Kwa kweli alikuta watakatifu wanatajwa katika Biblia, lakini hawatajwi kwa namna wanavyotajwa katika taratibu za kanisa la Roma Catholic. Basi akachukia na kuachilia mbali uchunguzi huo, akijishughulisha na mafunzo ya Biblia, yaani Neno la Mungu.TU 97.4

  Katika mwaka wa 1512, kabla Luther au Zwingli hawajaanza kazi ya matengenezo, Lefevre aliandika na kusema “Mungu ndiye alitupatia haki kwa njia ya imani, ambayo inatupeleka katika uzima wa milele, kwa neema tu”. Wakati alipokuwa akifundisha kwamba utukufu wa wokovu ni wa Mungu peke yake, akasema kuwa wajibu wa utii ni wa binadamu.TU 97.5

  Baadhi ya wanafunzi wa lefevre walimsikiliza kwa makini sana, hata wakatamani kuwa watangazaji wa maneno hayo ya Mungu, wakati mwalimu wao atakapofariki. Mmojawapo wa watu hao alikuwa William Farel. Wazazi wake walikuwa waumini mashuhuri katika kanisa la Roman. Naye alichukizwa sana na watu waliokuwa wakipinga mafundisho ya kanisa la Rumi. Alikuwa na nia ya kuwaangamiza watu kama hao alisema, “Ninaposikia mtu akisema maneno kinyume cha papa, ninamsagia maneno kama mbwa mwitu mwenye ghadhabu”. Lakini taratibu za ibada, kutukuza watakatifu kuabudu madhabahuni na kutoa matokeo ya kila namna haviwezi kuleta amani moyoni. Kutubu na kutoa kitubio cha dhambi na kadhalika haviwezi lolote. Maneno ya Lefevre yalikuwa, “Wokovu ni wa neema Msalaba wa Kristo pekee yake ndio hufungua mlango wa mbingu, na kufunga mlango wa kuzimu”.TU 98.1

  Farel akiwa ameongoka kama Paulo aligeuka kabisa kutoka katika kifungo cha mapokeo na kuingia katika uhuru wa wana wa Mungu. Alisema, “Badala ya kuwa na roho ya ghadhabu kama ya mbwa wa mwitu, aligeuka akawa mpole kama mwana kondoo, akiwa ameachana kabisa na papa na kumgeukia Kristo”TU 98.2

  Wakati lefevre alipokuwa akiitawanya nuru ya Injili kwa wanafunzi, Farel aliitawanya kwa watu wote hadharani. Mkuu wa kanisa, askofu wa Meaux alijiunga pamoja nao. Walimu wengine pia wakajiunga nao katika kutangaza Injili, na kuongoa watu wa aina mbalimbali, tangu mafundi, wakulima hata watu wa Ikulu, katika jumba la mfalme. Dada wa mfalme Francis I aliipokea imani ya watengenezaji. Watengenezaji walitazamia kwa matumaini makubwa wakati ambapo ufaransa ingeongolewa kwa Injili.TU 98.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents