Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Agano Jipya La Kifaransa

  Lakini matumaini ya Watengenezaji hayakutimia. Mateso na majaribu yaliwangojea wanafunzi wa Kristo. Walakini ni wakati wa amani ulipita kati; ili wajiandae kukutana na tufani kali. Wakati huo watengenezaji waliendelea sana. Lefevre alijishuhgulisha na kazi ya kutafsiri Agano Jipya kwa lugha ya Kifaransa. Wakati ule Biblia ya Kijerumani iliyotafsiriwa na Luther ilipotoka mitamboni huko Wittenberg. Agano Jipya ya kifaransa pia ilichapishwa huko Mequx. Basi wakulima wa Mequx wakapata kisomo Neno la Mungu. Basi wafanyakazi, mafundi, wakulima waliburudika sana na kuchangamka wakati walipokuwa wakingojea na kutafakari mafungu ya Biblia. Wao hao, ingawa hawakuwa wenye elimu ya juu, wakiwa wakulima tu, nguvu ya neema ya Mungu ilionekana katika maisha yao.TU 98.4

  Nuru iliyowashwa huko Meaux ilipeleka mwanga wake mbali. Hesabu ya waumini ilizidi kila siku. Kwa muda ghadhabu ya serikali ya kanisa la Rumi ilizuiliwa isiwaingilie watengenezaji, lakini baadaye viongozi wa papa walifaulu. Uchomaji moto wa wale wanaopinga Rumi ulianza. Wengi walichomwa moto hadharani kwa ajili ya imani yao.TU 99.1

  Katika majumba ya mabwana, na majumba ya wafalme, kulikuwamo watu waongofu ambao walithamini ukweli wa Biblia zaidi ya vyeo, mali, hata maisha yao. Lois de Bequin alikuwa mtu wa uzao wa kikubwa, yaani wazazi wake walikuwa maarufu. Yeye alijishuhgulisha na kujifunza Biblia akaongoka, ingawa kwanza alikuwa amewachukia Waluther, Baadaye aliposoma Biblia akaona kuwa mafundisho yaliyomo siyo ya Rumi, bali ya Luther. Basi akawa mfuasi. Warumi wa Ufaransa walimtupa kifungoni kama mtu mzushi, lakini alifunguliwa na mfalme. Kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa Francis alisitasita kati ya Rumi na matengenezo.TU 99.2

  Berquin naye alifungwa na wafuasi wa papa mara tatu, lakini alifunguliwa na mfalme aliyekataa kumtia hatiani kama mzushi. Bequin alionywa mara kwa mara kuhusu hatari iliyomkabili katika ufaransa, na akashauriwa atoke nchini akae mahali pengine penye usalama.TU 99.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents