Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Berquin Shujaa

  Juhudi ya Bequin ilizidi kuwa kubwa. Alikusudia kutenda makuu kijasiri. Yeye hakuitetea kweli peke yake, bali alishambulia makosa bila kujali. Wapinzani wake walikuwa watawa wasomi hasa waliosomea Biblia katika chuo kikuu cha Paris, ambacho ni chuo maarufu nchini. Katika maandiko ya watu hawa Berquin alipata makosa kumi na mawili ambayo alidai kuwa ni kinyume cha Biblia. Watu hawa walikuwa wataalamu. Alimwomba mfalme aamue katika mashindano hayo.TU 99.4

  Akifurahia nafasi hii ya kushusha kiburi cha watawa hawa, mfalme aliwaagiza Warumi wajitetee na kutetea msimamo wao kwa kutumia Biblia. Silaha hii itawasaidia kidogo tu. Mateso na kuchoma moto, ndizo silaha zao wazijuazo bora zaidi. Sasa wakaona kuwa wamo mtegoni kunaswa katika shimo walilotaka kumtupa Berquin na sasa wakatazamana na kutafuta njia ya kukwepa.TU 99.5

  Wakati huo huo sanamu ya bikira Maria iliyokuwa imesimamishwa kwenye kona ya barabara, ilikuwa imevunjwa. Watu wengi walijazana mahali hapo penye sanamu wakiomboleza na wenye uchungu. Hata mfalme alisikitika. Watawa walipaza sauti zao wakisema “Haya ni matokeo ya mafundisho ya Bequin Vitu vyote vitaondolewa sasa, yaani dini, sheria na serikali yenyewe na hawa Waluther waasi”.TU 100.1

  Mfalme akaondoka toka Paris, na watawa wakaachwa peke yao ili wafanye wapendavyo. Basi Berquin akashitakiwa na kuhukumiwa kufa. Na isiwe mfalme Francis kuingilia kati na kumwokoa, hukumu ingetekelezwa siku ile ile. Wakati wa adhuhuri watu wengi walikusanyika ili kushuhudia tukio hili. Wakashangaa kuona kuwa mtu aliyehukumiwa ni mtu mashuhuri katika nchi ya ufaransa. Mshangao na uchungu na wasiwsi vilijaa nyusoni mwa makutano. Lakini uso wa mtu mmoja tu ulikuwa na utulivu. Huyu aliyehukumiwa kufa, yaani Berquin, ndiye alijua kuwa Bwana wake yuko karibu hapo.TU 100.2

  Uso wa Berquin uling'aa kwa nuru ya mbinguni. Alivaa vazi la mahameli, la hariri na soksi za dhahabu, Alikuwa karibu kumshuhudia mfalme wa wafalme. Hakuwa na alama ya huzuni katika uso wake. Alijaa furaha.TU 100.3

  Wakati mkutano ulipoanza safari barabarani kwa taratibu, watu wakashangaa kumwona akiwa mwenye furaha. Watu wakasema, “Alifanana na mtu anayekaa hekaluni akitafakari mambo matakatifu”.TU 100.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents