Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito wa Calvin

  Katika mojawapo ya shule za Paris, kulikuwamo kijana mmoja, mwangavu, mtu asiye na lawama yoyote, mwenye akili, mcha Mungu. Hali yake bora alifanya chuo chake kijivune kwa ajili yake. Na ilitumainiwa kwamba kijana huyu ambaye anaitwa John Calvin atakuwa mtetea ukweli kanisani.TU 101.2

  Lakini nuru ya Mungu ilipenya kuta za chuo ikamfikia Calvin na kuupenya ushirika uliomzunguka. Olivetan binamu wa Calvin alikuwa amejiunga na watengenezaji. Wawili hao waliongelea mambo yaliyokuwa yakitatiza ukristo. Oliven alisema, “Kuna dini mbili duniani Protestant: Moja ambayo imebuniwa na watu, ambayo ni hujiokoa mwenyewe kwa njia ya maadhimisho yake na matendo yake mema. Dini nyingine ni ile inyofunuliwa katika Biblia, ambayo humwelekeza mtu apate wokovu kwa njia ya neema ya Mungu itolewayo bure”TU 101.3

  Calvin akasema “Sitataka mafundisho yako mapya unadhani kuwa nimeishi makosani kwa miaka hii yote?” Lakini Calvin alipokuwa peke yake katika chumba chake aliyatafakari maneno ya binamu yake. Alijikuta hana mtetezi mbele ya hakimu wa haki; yaani Mungu mkuu. Matendo mema, maadhimisho ya kanisa, yote yalikuwa bure kuweza kusamehe dhambi. Maungamo ya kitubio haviwezi kumpatanisha mtu na Mungu.TU 101.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents