Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mashahidi Katika Kuchomwa Moto

  Kwa bahati, siku moja Calvin alibahatika kushuhudia tendo la kuchoma mtu aliyedhaniwa kuwa ni mzushi hadharani. Katika tukio hilo la mateso ya kikatili akibisha kwa ajili ya hukumu iliotolewa na kanisa, kijana huyu aliona mfia dini akionyesha imani na ujasiri kabisa, na alipojipambanisha na yeye mwenyewe alijiona kuwa hafai. Akashangaa kuona kuwa mafundisho ya Biblia ndiyo “uzushi” na imani ya mzushi imejengwa katika Biblia. Kwa hiyo yeye aliazimu kujifunza Biblia na kuichunguza kwa makini.TU 101.5

  Katika Biblia alimgundua Kristo. Akapaza sauti na kusema “O Baba, dhabihu yake imetuliza ghadhabu yako, damu yake imeniosha uchafu wangu, msalaba wake umenitetea; kifo chake kimenipatanisha na Mungu. Umenigusa moyo wangu ili niyachukie mambo yote, isipokuwa yale ya Yesu tu”TU 102.1

  Sasa akakusudia kujitolea kwa Injili katika maisha yake yote. Lakini aliogopa na akajishughulisha kujifunza. Ila kwa ajili ya maoni na mashauri ya rafiki zake, mwisho akakubali kuwa mwalimu. Maneno yake yalifanana kana kwamba ni umande unavyoanguka majanini, na kuiburudisha nchi. Sasa alikuwa katika mji mkuu wa mkoa, akiwa chini ya ulinzi wa Margaret, binti wa mfalme, ambaye kwa kupenda injili, aliwalinda wapenda injili wenzake. Kazi ya Calvini ilianza katika nyumba za watu. Waliosikia Ijili, nao walipitisha kwa wenzao, na vivi hivi. Aliendelea kuweka msingi wa kanisa ulio imara, ambalo litatoa ushuhuda bila woga.TU 102.2

  Ilipasa Paris ipate nafasi nyingine ya kuhubiriwa Injili. Mahubiri ya Lefevre yalikataliwa, walakini ilipasa Injili ihubiriwe kwa watu wote wakaao humo. Mfalme alikuwa hajawaunga mkono Warumi na kuwapinga watengenezaji. Margret alikubali kuwa imani iliyosahihishwa lazima ihubiriwe katika mji wa Paris. Akaamuru kuwa mchungaji wa Kiprotestant lazima ahubiri makanisani. Jambo hili lilipigwa marufuku na waongozi wa Papa. Margret akaruhusu Injili ihubiriwe hata katika jumba la ufalme. Iliamriwa kuwa kila siku mahubiri yatolewe mara moja. Watu maelfu walikuwa wakihudhuria kwenye mahubiri hayo. Mfalme akaamuru kuwa makanisa mawili ya Paris yafunguliwe. Mji wa Paris ulikuwa haujahubiriwa Neno la Mungu kama wakati huu. Hali ya kiasi, usafi na utulivu pamoja na shughuli vilichukua mahali pa ulevi, ufisadi, ugomvi na uvivu. Watu wengine walipoiamini Injili, wengine walikataa. Baadae watu wa papa walifaulu kupata madaraka kwa hiyo wakaamuru makanisa yafungwe, na kuanza tena kuchoma watu moto waliowapinga.TU 102.3

  Wakati huo Calvin alikuwa angali Paris. Mwishowe wenye madaraka wakakusudia kumwingiza katika ndimi za moto. Calvin hakuwa na wazo lolote kuhusu hatari, wakati rafiki zake walipomwendea chumbani mwake, na kumwambia kuwa wakuu wako njiani wanakuja kumkamata. Basi muda si muda pakasikika hodi kwenye mlango wa nje. Basi rafiki zake hawakupoteza wakati. Walikwenda kuwachelewesha wakuu pale mlangoni wakati wengine walimshusha Calvini dirishani, akakimbilia katika nyumba ya mtu mmoja aliyekuwa rafiki yake. Huko akajigeuza na kuvaa mavazi mengine, akatia jembe begani akaaza safari. Alisafiri kwenda kusini ya ufaransa, mwisho alijikuta amefika katika utawala wa Margret, Huko akapata hifadhi.TU 102.4

  Calvin hakuzidi kujikalia bila kazi. Mara ile hatari iliyomkabili ilipotulia alitafuta mahali pengine pa kufanyia kazi huko Poitiers, ambapo paliyakaribisha mawazo mapya. Hapo watu walisikiliza Injili kwa moyo. Wafuasi walipoongezeka ilionekana kuwa ni bora watoke mjini wawe nje ya mji. Pango moja zuri lilichaguliwa liwe mahali pa mkutano. Mahali hapo pa siri neno la Mungu lilisomwa na kutafakariwa. Mahali ambapo hapo waliadhimisha siku kuu ya meza ya Bwana kwa waprotestant wa Ufaransa. Kutoka katika kanisa dogo hili watu kadhaa wa kadhaa waaminifu walitumwa huko na huko kuitangaza Injili.TU 103.1

  Mara nyingine tena Calvin alirudi Paris, lakini alikuwa karibu kila aina ya kazi ya matengenezo imefungwa. Mwisho akakata shauri kwenda kuishi Ujerumani. Wakati tufani ya mateso ilipolipuka ufaransa, Calvin alitoka huko kwa shida sana. Waprotestant wa ufaransa, yaani watengenezaji walikusudia kuanzisha shambulio maalumu juu ya Rumi ambalo lingetaharikisha nchi nzima. Matangazo ya kushambulia ubatili wa misa yaliwekwa usiku moja mahali pote nchini. Bidii hii ambayo ilikuwa dhaifu iliwapa Warumi sababu ya kutaka wazushi hawa waangamizwe, kwamba wanahatarisha serikali, na kuvuruga amani nchini.TU 103.2

  Mojawapo ya tangazo hili lilibandikwa kwenye mlango wa mfalme ujasiri huu wa ovyo uliothubutu hata kufika katika nyumba ya mfalme ulichochea ghadhabu. Ghadhabu yake ilikuwa katika usemi huu: “Washikwe wote bila kujali wanaoshukiwa. Bora wawe Waluther. Nitawango'a wote” Mfalme aliunga mkono Warumi.TU 103.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents