Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utawala wa Hofu Kuu

  Mfuasi mmoja wa imani ya matengenezo aliyezoea kuita waumini, wakutane mahali pa siri ili waabudu na kujifunza neno la Mungu, alikamatwa. Mtu huyu alikabiliwa na kifo cha kuchomwa moto, na matisho yake, aliamuriwa aingie kila nyumba ya mfuasi wa Kiprotestant katika mji huo ajitambulishe kama mfuasi wa papa. Hofu ya kuchomwa moto ilimtisha, naye akakubali kuwasaliti wenzake, yaani akafanya jinsi alivyoamuriwa kufanya. Morin, mpelelezi wa serikali pamoja na msaliti huyu alipita pole pole barabarani mjini. Walipofikia nyumba ya mfuasi wa Luther, yaani mluther, yule msaliti alionyesha dalili bila kutamka neno. Basi msafara ukasimama, ukaivamia nyumba hiyo ya mkristo mluther, watu waliokuwaamo wakakamatwa na kufungwa, halafu wakaendelea kutafuta wakristo wengine. “Morin aliutetemesha mji, ulikuwa utawala wa hofu kuu”TU 103.4

  Wale waliokamatwa waliuawa kikatili mno. Walipochomwa moto, iliamriwa kwamba moto upunguzwe makali yake ili wazidi kuungua kwa muda mrefu bila kuteketea. Lakini hata hivyo walikufa kishujaa bila kuonyesha hali ya kubabaika wakiwa washindi wa kweli. Watesi wao waliaibika, wakafedheheka. Watu wote wa Paris wakatambua aina ya wakristo wanaofuata imani ya matengenezo. Hapakuwako na madhabahu ya kuhubiri Injili sawa na iliyong'aza nyuso za watu hao waliopitia katika matatizo makuu mpaka kufa ilitangaza uwezo wa Injili.TU 104.1

  Waprotestanti walishitakiwa kuwa wanafanya njama ya kuwaangamiza Wakatoliki, na kuipindua serikali na kumwua mfalme. Lakini hakuna ushahidi hata kidogo uliopatikana kuhusu mambo hayo. Hata hivyo walitendewa yasiyosemeka. Lakini baada ya kupita karne moja, mambo hayo waliyowasingizia Waprotestant yaliwapata, yaani mauaji ya kupindua serikali na mfalme wao. Hayo yaliletwa na Uprotestant ndiyo ilileta maafa haya ya kutisha katika nchi ya ufaransa. Tuhuma, mashaka, hofu na wasiwasi vilikumba watu wote, wala hapakuwako na utulivu. Watu maelfu walikimbia kutoka Paris, wakawa wakimbizi katika nchi nyingine. Hali hii ikawafanya watu wapende imani ya matengenezo zaidi. Wafuasi wa papa walishangaa kuona watu hawa wazushi hawaonewi mashaka, ila watu wanaridhika kuwa nao.TU 104.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents