Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uchapaji Watangazwa Kuondolewa

  Francis I alikuwa anapendelea kujikusanyia watu wa kila hali, kutoka nchi zote. Kwa kuwa alikuwa na hamu ya kuwafutilia mbali wazushi wote, basi kundi hili la wataalamu likatoa sheria ya kupiga marufuku uchapaji wote katika nchi ya Ufaransa. Francis alitoa mfamo mmoja kati ya mingi iliyochapwa na kuhifadhiwa, akasema, kuwa utamaduni wa kisomi haufai kupingia dini na kuafikiana na mateso. Mapadri walidai kwamba matusi yaliyotolea kutukana mbingu kwa njia ya kudharau misa, lazima yalipwe kwa damu. Januari 21, 1535 ndiyo siku iliyochaguliwa kwa ajili ya adhimisho rasmi. Kila nyumba penye mlango paliwashwa kimuli kwa ajili ya kuheshimu ushirika mtakatifu (sacrament ya Kikatoliki). Kabla ya kupambazuka msafara ulianzishwa kwenye jumba la mfalme.TU 104.3

  “Msafara uliongozwa na askoru wa Paris katika fahari kubwa, huku akiungwa mkono wa wana wanne wa kifalme hakuvaa taji, wala mavazi ya kifalme” katika kuenenda, alijiinamisha kwa kila madhabahu, si kwa ajili ya makosa yaliyomtia unajisi, wala si kwa ya damu isiyo na hatia aliyomwaga, ila kwa ajili ya dhambi ya kifo ya watu wake ambao wamethubutu kuidharau huduma ya misa.TU 105.1

  Katika ukumbi wa jumba la askofu, mfalme alionekana katika maneno ya masikitiko, akiombolezea maovu yaliyoliangukia taifa. Aliitangaza siku hiyo kuwa ni siku ya kazi ya kuwang'olea mbali “wazushi” hawa wenye madhara, ambao wanatishia nchi yetu ya ufaransa. Alipokuwa akisema hayo machozi yalikuwa yakimtoka, na mkutano wote ukalia huku wakisema, “Tutaishi na kufa tukishikila dini ya Kikatoliki” Neema iletayo wokovu imeonekana na kuimulikia Ufaransa, lakini imesukumiwa mbali, wakichagua giza zaidi ya nuru. Wameyaita maovu kuwa ndiyo mema, na mema wakayaita kuwa maovu, mpaka wakazama kabisa katika udanganyifu mkuu. Nuru ambayo ingewaongoza kutoka katika udanganyifu na kifungo cha giza. Wameitupilia mbali.TU 105.2

  Mara nyingine tena msafara wa maandamano ulianzishwa. Mbali kidogo majukwaa ya kuchomewa wakristo wa Kiprotestanti yalijengwa, na ikapangwa kuwa kuni za kuchochea watu hao ziwashwe wakati mfalme atakapoonekana, na ya kwamba maandamano yatasimama kushuhudia mambo hayo. Mambo yalipotokea, wale waliochomwa hawakuonyesha alama yoyote ya kusitasita wala kufadhaika. Walipoambiwa wakane imani yao mmoja alisema, “Mimi ninaamini kile manabii na mitume walichoamini na kuhubiri na wakristo wote wanachoamini. Imani yangu imejengwa kwa Mungu atakayeshinda nguvu za kuzimu”TU 105.3

  Waliporudi na kufika jumba la mfalme, watu walitawanyika na mfalme na maaskofu wakaenda zao huku wakijitia moyo kwamba, wataendelea na kazi hiyo ya kuwaangamiza “wazushi”TU 105.4

  Amani ya Injili ambayo ufaransa imeikataa itaendelea kwa hakika, lakini matokeo ya Ufaransa yatakuwa ya hatari. Katika Januari 21, 1793 maandamano mengine yalipita katika barabara za Paris. Safari hii tena mfalme ndiye alikuwa mwanzilishi wa maandamano. Tena kulikuwa na makelele na ghasia wakitafuta wazushi wapya. Tena siku hiyo ilishia kwa kuchoma watu wengine. Mfalme Louis XVI alipokamatwa alijaribu kushindana sana na walimkamata, mwisho akakatwa kichwa na kuchomwa. Mahali hapo pa kuchomea watu, karibu watu 2,800 walipoteza maisha yao.TU 106.1

  Matengenezo yameifunua Biblia katika ulimwengu. Upendo mkuu wa Mungu ulizidhihirisha wazi kanuni za mbinguni. Ufaransa ilipokataa kipawa cha mbinguni, ikajiwekea akiba ya uharibifu. Mwenendo wa njia yao na makusudi yao ilitokeza uasi na mapinduzi yaliyoleta utawala wa hofu kuu.TU 106.2

  Shujaa Farel alifukuzwa nchini kwao akaenda Uswisi. Hata hivyo mvuto wake haukuzimwa ufaransa. Akisaidiana na wengine waliofukuzwa kama yeye, walitafsiri maandiko ya Kijerumani katika lugha ya Kifaransa; walitafsiri pia Biblia katika Kifaransa, na vyote vikachapishwa. Kwa kuwa vilichapishwa kwa wingi, Wainjilisti wa vitabu walikuwa wakiviuza huko ufaransa.TU 106.3

  Farel aliifanya kazi yake huko Uswisi akiwa kama mwalimu, huku akieneza mafundisho ya Biblia kwa hadhari kubwa. Watu wengine waliamini, lakini mapadri waliinuka na kukomesha kazi hiyo, na washirikina waliipinga kazi Mapadri walisema “Kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu maana kuhubiri kwake hakuleti amani ila vita”.TU 106.4

  Farel alisafiri kijiji kwa kijiji, huku akivumili njaa baridi, uchovu na hatari ya maisha yake. Alihubiri sokoni makanisani, na mara nyingine katika mahekalu ya Wakatoliki. Mara moja alikamatwa na kupigwa karibu kufa, lakini aliendela mbele. Alikwenda mji hata mji, mahali ambapo ni ngome ya Ukatoliki, akigongagonga milango yao kwa Injili.TU 106.5

  Farel alitamani kuimarisha Uprotestant huko Geneva. Kama akifaulu kupanda Uprotestanti katika mji huu, ndipo patakuwa kituo kikubwa cha kuendeshea kazi katika Ufaransa, Uswisi na Italia. Miji mingi na vijiji vilivyozunguka vilipokea Injili.TU 106.6

  Aliingia Geneva akiwa na mwenzake mmoja tu. Huko aliruhusiwa kuhubiri mahubiri mawili peke yake. Mapadri walimwita katika baraza, ambako walikuja na silaha wameficha nguoni, ili wapate kumwulia mbali. Watu wengi walikusanyika kuhakikisha kuwa hawezi kutoroka. Hata hivyo mahakimu na askari walimwokoa. Kesho yake asubuhi mapema alisindikizwa akavuke ziwa kwenda mahali pa usalama. Huo ndio ulikuwa mwisho wa mahubiri yake ya kwanza huko Geneva.TU 107.1

  Jaribio la pili walichagua kijana mnyonge aliyetendewa vema na watengenezaji. Lakini yeye atafanya nini mahali ambapo Farel alikataliwa? “Mungu amechagua mambo mapumbavu ya dunia, awaaibishe wenye hekima” Kor. 1:27TU 107.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents