Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ishara ya Maangamizo

  Utabiri wowote Yesu aliotabiri kuhusu uangamizo wa Yerusalemu ulikuwa unatimia moja kwa moja. Ishara na vioja vilionekana. Kwa muda wa miaka saba mtu fulani alikuwa akitembeatembea katika barabara za Yerusalemu huku akitangaza ole utakaoujia mji. Mtu huyu ambaye hajulikani alikotoka aliteswa na kufunga na kutendwa mabaya lakini kwa dharau na jeuri yeye alijibu, “Ole Ole, wa Yerusalemu”. Baadaye aliuawa katika kuuzingira Yerusalemu. Katika maangamizo ya Yerusalemu hakuna hata mkristo mmoja aliyepotea. Baada ya majeshi ya Kirumi chini ya jemadari Cestius kuuzingira mji,ghafla waliondoka bila kutazamiwa, wakati kila jambo lilikuwa tayari kwa mashambulio. Jemadari wa Kirumi aliamuru majeshi yake yaondoke bila sababu maalum. Dalili iliyoahidiwa na Kristo kwa wafuasi wake imefika. Luka 21:20-21.TU 5.1

  Mambo yalitayarishwa kabisa ili kuwezesha wakristo kukimbia, ambavyo hayakuwezekana kuzuilika. Wayahudi au Warumi hawakuweza kuyazuia. Wakati majeshi ya jemadari Cestius yalipoondika, Wayahudi nao walitoka kuwafukuza, na wakati walipokuwa katika kupambana, wakristo walipata nafasi ya kukimbilia mahali pa usalama. Walikimbilia mji wa Pella.TU 5.2

  Majeshi ya Wayahudi yaliyowafuatia Warumi yalishambulia majeshi ya nyuma. Hivyo Warumi walifaulu kwa shida sana kuendelea. Wayahudi walirudi Yerusalemu wakifurahi, wakiwa na vitu walivyoteka. Ushindi mdogo huu uliwaletea maafa makubwa. Walizidi kuwa wakaidi zaidi wasitake kujisalimisha kwa Warumi, hivyo maafa makubwa yasiyoelezeka, bila kipimo yalifuata baadaye.TU 5.3

  Mabaya ya kutisha yaliujiaYerusalemu wakati jemadari Titus aliporudi na kuuzingira mji mara ya pili. Mji ulizingirwa wakati wa Pasaka, wakati Wayahudi kwa mamilioni walikuwa wamekusanyika ndani yake. Maghala ya vyakula yalikuwa yameharibiwa na watu wenye fitina, na sasa hali ya njaa iliwaingilia. Watu walikula ngozi za mishipi yao na viatu vyao. Watu wengi sana walikuwa wakipenya usiku na kutoka nje ya mji kutafuta matunda mwitu. Wengi walikuwa wakikamatwa na kuuawa kikatili. Mara nyingi hata wale waliowahi kurudi salama, walinyanganywa na wenzao kile walichopata huko nje. Waume waliwanyang'anya wake zao chakula na wake vivyohivyo waliwanyanga'nya waume zao. Watoto walipokonya chakula kutoka vinywani mwa wazee wao.TU 6.1

  Viongozi wa majeshi ya Kirumi walikusudia kutoa kipigo kizito kwa Wayahudi ambacho kingewafanya wasalimu amri mara moja. Mateka walipigwa, wakateswa sana na kutundikwa mitini, mbele ya kuta za mji. Kufuata bonde la Yeoshafati na kuendelea mpaka mlima wa Golgota, misalaba mingi sana, ambako watu walikuwa wametundikwa ilijazana tena. Hapakuwako na nafasi ya kupita kati yake. Kwa hiyo matamshi yaliyotamkwa mbele ya kiti cha hukumu cha Pilato kwamba: “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu” yalikuwa yanatimia. Mathayo 27:25.TU 6.2

  Jemadari Titus alijawa na hofu ya mshangao wa kuchukiza alipoona maiti za Wayahudi zimejazana bondeni humo. Alilitazama Hekalu; akaamuru kuwa mtu asiliguse. Aliwasihi viongozi wa Wayahudi wasalimu amri, asije akalazimika kuwaharibu, na kupaharibu mahali patakatifu kwa kumwaga damu; yaani wasiingize vita hekaluni. Kama Wayahudi wangalipigania mahali pengine, hakuna Mrumi hata mmoja angelithubutu kuharibu hekalu takatifu! Josephus aliwasihi sana wasalimu amri ili wajiokoe, na kuokoa mji wao, pamoja na hekalu lao takatifu. Lakini alijibiwa kwa matusi mabaya na kushambuliwa kwa ghafla. Hivyo ndiyo ilikuwa nafasi yao ya mwisho na Josephus alikuwa mwombezi wao wa mwisho. Titus alijaribu kuliokoa hekalu, lakini ilikuwa kazi bure. Mkuu kuliko yeye alikuwa ametamka kuwa, halitasalia jiwe juu ya jiwe.TU 6.3

  Baada ya kuliteketeza hekalu, mji wote ukaangukia mikononi mwa Warumi. Viongozi wa Wayahudi waliziacha ngome zao. Titus alisema kuwa Mungu ndiye amezitia katika mikono yake, maana hakuwa na uwezo wa aina yoyote ile ambao ungaliweza kuzibomoa ngome hizo. Mji na hekalu pia vilibomolewa mpaka na misingi yake yote; na mahali pale hekalu takatifu lilipojengwa palilimwa kwa jembe na kusawazishwa kama shamba. Yeremia 26:18. Watu zaidi ya milioni moja waliangamia, na waliobakia wengine walitekwa na kupelea utumwani; wengine waliuzwa kama watumwa wengine walitawanyika wakaishi mahali pengine katika hali ya ukimbizi na wengine walitupwa katika matundu ya simba na wanyama wakali wakawa sinema ya kutazamwa na watu wakiangamizwa.TU 6.4

  Wayahudi walikuwa wamekijaza kikombe chao cha kulipizwa kisasi. Katika misiba iliyowafuata baadaye ilikuwa na mavuno ya mambo waliyoyapanda kwa mikono yao wenyewe. “Ee Israeli, umejiangamiza mwenyewe;…. Kwa maana umeanguka kwa sababu ya maovu yako”. Hosea13:9; 14:1. Taabu yao ilitajwa kila mara kama adhabu iliyoagizwa na Mungu. Kwa njia hii mdanganyaji mkuu hufunika kazi yake na kuitupa kwa Mungu. Wayahudi kwa ajili ya ukaidi wao wa kukataa rehema na upendo wa Mungu walijiondolea ulinzi wa Mungu wakabakia wazi.TU 7.1

  Hatujui kiasi gani tunawiwa na Kristo kwa ajili ya amani na ulinzi tulivyo navyo. Mkono wa Mungu wa kuulinda humzuia Shetani asituharibu. Kutotii na kutoshukuru ni deni kubwa tulilo nalo kwa Mungu. Lakini mtu anapovuka mpaka wa Mungu ulinzi wake huondolewa. Mungu hamtetei mtu huyu kama mshitakiwa. Huwaacha hao wakaidi wavune kile walichopanda. Kila cheche ya nuru iliyokataliwa ni mbegu iliyopandwa, nayo italeta mavuno. Roho wa Mungu anayesihi akipingwa daima, mwisho ataondoka. Ndipo mtu atabaki bila uwezo wa kuzuia tama mbaya kwake, hakuna kinga kwa madanganyo ya mwovu Shetani.TU 7.2

  Uharibifu wa Yerusalemu ni onyo kuu kwa watu wote wanaokataa rehema za Mungu. Unabii wa Mwokozi kuhusu hukumu ya Yerusalemu utatimia kwa njia nyingine. Katika ajali ya mji mteule, tunaona msiba utakaowapata walimwengu waliokataa rehema za Mungu na kukanyaga sheria yake takatifu. Huzuni kuu ambayo haijatokea ulimwenguni. Iliwapata watu wapotovu. Kukataa mamlaka ya mbinguni kumekuwa jambo la kutisha sana. Lakini wakati ujao utakuwa wa huzuni kuu zaidi. Wakati roho wa Mungu atakapoondolea kabisa ulimwenguni, hakuna kitu kitakachozuia hali ya kinyama, na hasira za kishetani na udanganyifu wake wa kikatili.TU 8.1

  Katika siku hiyo, sawa na ulivyokuwa kwa Yerusalemu, watu wa Mungu wataokolewa. Soma Isaya 4:3; Mathayo 24:30-31. Kristo atakuja mara ya pili ili kuwakusanya watu wake. “Ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni, pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu” Mathayo 24:30-32.TU 8.2

  Hebu watu na waangalie sana, wasije wakasahau maneno ya Kristo. Kama vile alivyowaonya wanafunzi wake kuhusu uharibifu wa Yerusalemu, juu ya kukimbia kwao, ndivyo pia ameonya ulimwengu kuhusu uharibifu wa mwisho. Wale wapendao wanaweza kukimbia ghadhabu ijayo. “Tena kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa” Luka 21:25. Soma pia Mathayo 24:29; Marko 13:24-26; Ufunuo 6:12-17. Maneno ya Kristo ya maonyo ni kwamba, “Kesheni basi” Marko 13:35. Wale watakaojali maonyo hawataachwa wakae gizani.TU 8.3

  Sasa ulimwengu hauko tayari kupokea maneno ya ujumbe wa Kristo kwa wakati huu, kuliko Wayahudi walivyopokea maonyo ya Kristo kuhusu uharibifu wa Yerusalemu. Njoo, maadamu ni leo. Siku ya Mungu itawaghafilisha wote, wasiomcha Mungu. Wakati maisha yatakapokuwa yanaendelea kama kawaida; wakati watu watakapozama kabisa katika anasa; katika shughuli, na katika uchumi; wakati waongozi wa dini watakaposifia maendeleo ya ulimwengu na watu wakijitumainisha kuwa na amani na usalama, ndipo, kama vile mwizi aibavyo usiku, ndivyo uharibifu utakavyowajia wote wasiomcha Mungu, “Wala hakika hawataokolewa”. 1Thes. 5:2-5.TU 8.4

  Marejeo: TU 8.5

  Milman — History of the Jews. Book 13TU 8.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents