Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Forement, Mwalimu

  Forement alianza kazi kama mwalimu. Ukweli ule aliofundisha watoto katika skuli, watoto waliukiri walipofika nyumbani kwao. Hivyo wazazi nao wakaupata ukweli wa Biblia. Agano jipya pamoja na vijizuu viligawiwa bure kwa watu. Baada ya kupita muda Forement pia akafukuzwa nchini. Ingawa aliondoka lakini ukweli alioupanda mioyoni mwa watu uliota. Imani ya matengenezo umepandwa nchini. Wahubiri walirudi na ibada ya kiprotestant ikaanzishwa Geneva.TU 107.3

  Wakati Calvin alipoingia Geneva mji ulikuwa umetangazwa kwamba unafuata imani ya matengenezo. Alikuwa akienda Basel wakati alipolazimika kuzungukia Geneva.TU 107.4

  Katika matembezi haya Farel alitambua uongozi wa Mungu. Ijapokuwa Geneva ulikuwa umeipokea imani ya matengenezo hata hivyo nguvu ya uongofu kamili lazima itokane na Roho Mtakatifu; wala siyo agizo la Baraza. Ijapokuwa Geneva imekataa mambo ya Rumi, ilikuwa bado inaambatana na makosa yaliyotapakazwa na Rumi.TU 107.5

  Farel alimsihi mwinjilist Calvin akae hapo na kufanya kazi hapo. Lakini Calvin aliondoka kwa ajili ya hadhari. Aliogopa kukabiliana na watu wa Geneva waliokuwa wagumu na wakaidi. Alitafuta mahali patulivu ili apate kujifunza. Hapo akaandika mafundisho na kuyachapisha. Na kwa njia hiyo akasaidia kujenga makanisa. Hakuweza kukataa. Ilionekana kwake kana kwamba mkono wa Mungu umemwangalia mahali ambapo ataishi bila kubadilika.TU 107.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents