Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ngurumo za Laana

  Ngurumo za papa zilielekezwa huko Geneva. Sasa mji huu mdogo utawezaje kushindana na uwezo mkuu huu ambao huwatetemesha wafalme na wafalme wakuu?TU 108.1

  Ushindi wa watengenezaji umekwisha kupita, na Rumi ikakusanya nguvu mpya ili ikamilishe kazi ya kuangamiza hawa watengenezaji. Kanuni ya hawa Warumi wa Jesuits walikuwa wakatili na wenye uwezo mkuu wa kutisha. Waliangamiza kabisa bila kujali lolote, ila tu kutimiza agizo lao.TU 108.2

  Injili ya Kristo imesababisha na kuwezesha watu kuvumilia mateso, baridi, njaa, kazi ngumu na umaskini. Walishikilia ukweli wa Injili bila kuogopa aibu, vifungo, na kifo cha kuchomwa moto. Warumi wa Jesuit walileta mtindo mpya. Kusudi lao lilikuwa kuung'oa Uprotestant, na kuusimamisha utawala wa upapa.TU 108.3

  Walivaa mavazi ya utawala na kutembelea magereza na hosipitali, wakiwahudumia wagonjwa na maskini wakijifananisha na Yesu aliyekwenda huko na huko akitenda kazi njema. Lakini katika kifuniko hiki cha utawa, ulifichika uovu na makusudi ya uasi.TU 108.4

  Kanuni ya mambo yao ilikuwa kuhalalisha mambo yao huko wakiongopa, wakiiba, wakiua, kana kwamba mambo hayo ni halali kufanyika wakiwa wanalihudumia kanisa. Katika hali hiyo yao ya hila walipata nafasi ya kufikia hata vyeo vya serikali vilivyo vikuu. Walikuwa kama watumishi waaminifu sana huku wakiwa majasusi. Walifungua skuli na vyuo vikuu vya kufundishia wana wa kifalme, na watu wote. Waprotestanti walivutwa kijanja hata wakaingizwa na kufuata kanuni za kipapa. Kwa kuwa watoto walizoezwa kufuata kanuni za Kirumi, hivyo wakausaliti uhuru ambao baba zao waliupigania na kumwaga damu. Popote hawa Jesuits walipokwenda walizidi kuimarisha ukatoliki.TU 108.5

  Ili kuwatia nguvu papa alitoa tangazo la kuanzisha kikosi cha ujasusi. Watu wengi sana sana wenye ujuzi na utaalamu waliuawa na kukimbia nchi nyingine.TU 109.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents