Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  13/Huko Uholanzi

  Katika nchi ya Uholanzi udhalimu wa papa ulipingwa mapema sana. Miaka mia saba kabla Luther hajatokea askofu wa Rumi alishutumiwa wazi bila hofu na makasisi wawili Warumi waliotumwa kama mabalozi huko Rumi, ambao walikuwa wamejifunza ukweli. Walimwambia, “Wewe waketi hekaluni mwa Mungu. Badala ya kuwa mchungaji wewe umekuwa mbwa wa mwitu katika kondoo. Inapokupasa kuwa mtumishi wa watumishi, wewe wajitahidi kuwa bwana wa mabwana, na kulidharau jina la Mungu na amri zake”TU 110.1

  Wengine waliinuka toka karne hata karne, wakaendeleza upinzani huo. Katika tafsiri ya Biblia kwa lugha ya Kidachi iliyotafsiriwa na Waldenses, kuna usemi usemao, “Kulikuwa na mafanikio makubwa ndani yake. Hakuna mzaha, hadithi, upuuzi, udanganyifu au jingine kama hayo; ila ukweli tu ndio uliomo” Huo ulikuwa usemi wa marafiki wa imani wa zamani, katika karne ya kumi na mbili.TU 110.2

  Sasa mateso ya Warumi yalianza, lakini waumini walizidi kuwa wengi, huku wakitangaza kuwa Biblia ndiyo isiyo na kasoro wala kosa lolote, katika kuingoza dini na kwamba mtu hashututishwi kuamini, ila mtu huaminishwa na mafundisho yake.TU 110.3

  Mafundisho ya Luther yalipata watu waaminifu katika Uholanzi, ambao walikwenda kulihubiri neno la Mungu. Menno Simons, mtu msomi hasa, wa dhehebu ya Kirumi, ambaye aliwekewa mikono kuwa padri, hakufahamu cho chote kuhusu Biblia. Naye aliogopa kuisoma kwa hofu asidhaniwe kuwa mzushi. Alipoingia katika maisha ya ufedhuli, akijaribu kuzima sauti ya dhamira yake, hakufaulu. Baada ya muda alianza kusoma Agano Jipya. Masomo hayo pamoja na maandiko ya Luther yalimwongoa akajiunga na imani ya watengenezaji.TU 110.4

  Baada ya kushuhudia kwa muda mtu mmoja akiuawa kwa ajili ya kubatizwa mara ya pili. Jambo hili likamfanya asome Biblia kuhusu ubatizo wa watoto wachanga. Akagundua kuwa kutubu na kuamini ndiyo vilivyotakiwa ili mtu abatizwe.TU 110.5

  Menno akatoka katika kanisa la Rumi, akajishughulisha na kazi ya kufundisha ukweli alioupata katika Biblia. Katika nchi ya Ujerumani na Uholanzi vikundi vya dini kali vilikuwa vimepatikana. Vikundi hivyo vilikuwa viovu, visivyokuwa na heshima wala adabu, visivyo na utaratibu, vikawa na fitina na maasi. Menno akapigana nao na mafundisho yao mapotofu. Kwa muda wa miaka ishirini na mitano alizungukazunguka katika Uholanzi na Ujerumani ya kaskazini akiendeza mvuto mzuri pamoja na mafundisho yake.TU 110.6

  Alikuwa mtu mwongofu, mnyenyekevu na mpole na mwenye bidii. Watu wengi waliongoka katika kazi yake.TU 111.1

  Katika Ujerumani Charles V alikuwa amepiga marufuku mambo hayo maovu. Katika Uholanzi uwezo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Hivyo tangazo la kuanza mateso lilifuata mara kwa mara. Mambo kama vile, kusoma Biblia, kuhubiri habari za Biblia, kumwomba Mungu kwa siri, kutokuinamia sanamu, na kuimba Zaburi vyote hivyo, mtu akionekana anafanya hivyo, adhabu yake ni kifo. Watu maelfu walipoteza maisha yao chini ya utawala wa Charles V. na Philip IITU 111.2

  Wakati mwingine jamaa nzima waliletwa kuhojiwa barazani kwamba hawakuhudhuria misa, au kwamba waliabudia nyumbani. Katika tukio moja la namna hiyo kijana mdogo alijibu: “Tulipiga magoti, tukamsihi Mungu atuangazie nuru ya mbinguni na kusamehe dhambi zetu, Tulimwombea mfalme wetu, ili ufalme wake ufanikiwe, na awe na furaha. Tuliwaombea watawala wetu, ili Mungu awalinde” katika tukio hili baba na mwana wake mmoja walihukumiwa kuchomwa moto.TU 111.3

  Sio wanaume tu walioonyesha ujasiri wao, ila hata wanawake na wasichana wengi walionyesha ushujaa mkubwa. Wanawake wengi walisimama kishujaa kando ya waume wao walipokuwa wakichomwa moto, na kuwafariji. Wasichana wengi walikuwa wakikabili moto wamevalia maridadi kama kwamba wanakwenda arusini.TU 111.4

  Mateso yaliongeza waumini zaidi katika ukweli. Mwaka kwa mwaka mfalme alijitahidi kuwatendea ukatili wa kila namna, lakini ilikuwa kazi bure. Baadaye William wa Orange aliletauhuru katika Uholanzi wa kuabudu Mungu bila wasiwasi.TU 111.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents