Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matengenezo Katika Denmark

  Katika nchi za kaskazini Injili iliingia huko kwa amani. Wanafunzi waliokuwa wakijifunza katika chuo cha Wittenberg waliporudi kwao huko Scandinavia walipeleka ujumbe wa Injili. Hata maandiko ya Luther pia yalieneza nuru ya Injili. Watu wagumu wa kaskazini waligeuka, wakaacha upotovu wa Rumi na kushika ukweli wa Biblia.TU 111.6

  Tausen, Mtengenezaji wa Denmark, alipokuwa kijana mdogo, alijithibitisha kuwa mpenda dini, akaingia na kuishi katika nyumba ya watawa. Mtihani ulikuwa ukimthibitisha kuwa na uwezo na kulitumikia kanisa. Kijana huyu akiwa shuleni alipata nafasi ya kuchagua chuo apendacho; Ujerumani au Uholanzi. Watawa wakamshauri asiende huko Wittenberg au asije akaharibiwa na wazushi.TU 111.7

  Tausen akachagua kwenda Cologne, chuo mashuhuri cha Waroma. Mara akachukizwa, kwa maana alisoma maandiko ya Luther, akayapenda sana na kuyathamini. Lakini kufanya hivyo lazima akosane na wakubwa wake, na anyang'anywe msaada wote. Mara akaamua kwenda kusomea Wittenberg.TU 112.1

  Aliporudi Dernmark hakuweza kufunua siri yake, alijitahidi kuwafundisha watu Neno la kweli na kuwaleta katika nuru ya kweli ya Injili. Aliwafundisha Biblia, na kumhubiri Kristo ambaye ndiye tumaini la mwenye dhambi. Wakuu wake ambao walimtumaini kuwa atakuwa mtetezi wa Warumi, walikasirika sana. Mara moja wakamwondoa katika nyumba yake ya utawa na kumweka kwingine, ambako kulikuwa sawa na kifungo. Mle katika chumba chake aliweza kuzungumza na wenzake walio nje na kuwapa ukweli wote. Wazee hao wa Denmark kama wangalikuwa werevu wa kutosha wangalimkomesha Rausen kabisa, lakini badala yake wakamhamisha tu katika nyumba ya utawa.TU 112.2

  Amri ya serikali ilikuwa kwamba watu hawa wanaohubiri imani ya namna mpya walindwe, wasidhuriwe. Makanisa yakafunguliwa kwake, na watu wakakusanyika kumsikiliza. Agano Jipya katika lugha ya Kidachi lilitawanywa kila mahali. Juhudi iliyofanywa ili kuzuia kazi ya matengenezo ilieneza mpaka nchi nzima ya Denmark ikatangaza kuwa imekubali amani ya matengenezo.TU 112.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents