Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maendeleo Katika Swideni

  Katika Sweden pia, vijana waliokuwa wakisomea Wittenberg waliporudi kwao walikwenda na ujumbe ambao ni maji ya uzima, wakawapelekea watu wa kwao. Watangulizi katika matengenezo ya Sweden, ambao ni Olaf na Laurentius Petri, walifundishwa ukweli huo na Luther na Melanchthon. Olaf aliwaamsha watu na ukweli huo wa Injili kama watengenezaji wengine kwa njia ya mahubiri. Lakini Laurentius alikuwa mtulivu sawa na Melanchthon. Wote wawili walikuwa mashujaa. Mara kadhaa Olaf aliponyoka asife kwa bahati. Walakini watengenezaji hawa walikuwa wakilindwa na mfalme, aliyekuwa anapendelea matengenezo, na aliyekuwa anapenda watu hawa wapigane na ufedhuli wa Rumi.TU 112.4

  Olaf alitetea imani ya matengenezo kwa nguvu sana mbele ya mfalme na waku wake. Akadai kwamba mafundisho ya mapadri wa Rumi yangekubaliwa tu kama yanakwenda sawa na Biblia. Kwamba kanuni za imani zote zinaongozwa na Biblia, na ziko wazi za kufahamika na watu wote.TU 113.1

  Tofauti hii hutudhihirishia baina ya ukweli na uongo kati ya mahaba na watengenezaji. Hawa sio wajinga, wenye fujo, wabishi, wao ni watu waliolisoma neno la Mungu, na wanajua jinsi ya kutumia silaha ambazo neno la Mungu linazitengeneza. Wao ni Wasomi kamili na wenye elimu ya Neno la Mungu, wanaoufahamu ukweli kamili, ambao wanafaulu katika ubishi na hila za Rumi.TU 113.2

  Mfalme wa Sweden aliikubali imani ya matengenezo na bunge la taifa likapitisha ukubali wake. Ndugu wawili hao wakashika kazi ya kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kiswedish kwa utashi wa ufalme. Ikapitishwa na wakuu kwamba wachungaji wako huru kufundisha Biblia katika nchi nzima, na kwamba watoto wanaosoma katika shule zote wafundishwe Biblia.TU 113.3

  Taifa hilo baada ya kufunguliwa kutoka katika udhalimu wa Rumi, likastawi na kufanikiwa, ambavyo haijawa hivyo wakati wowote. Baada ya karne moja kupita, taifa hili dhaifu katika Ulaya nzima, likaingia kuisaidia ujerumani katika vita vilivyodumu miaka thelathini. Ulaya ya Kaskazini yote ikaonekana kuwa chini ya mamlaka ya Rumi. Majeshi ya Sweden ambayo hayakuweza kuifanya Ujerumani ishinde, ili ifanye Uprotestanti uendelee na kufanya uhuru wa dini udumu katika nchi zilizoyapokea matengenezo.TU 113.4

  Marejeo: TU 113.5

  Gerard Brandt — History of Reformation in and About the Low Countries, bk.1 p. 6 TU 113.6

  Ibid. p. 14 TU 113.7

  Martyn, Vol. 2 p. 87 TU 113.8

  Wylie, bk. 18 ch. 6 Ibid. TU 113.9

  Ibid. bk. 10 ch. 4TU 113.10

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents