Go to full page →

Vyombo vya Nyumbani Viwe Vyepesi Visivyo vya Bei Kubwa KN 170

Weka nyumbani mwako vyombo vyepesi, rahisi kutengenezwa, vitu ambavyo vitastahimili kutumiwa, viwezavyo kusafishwa kwa urahisi, na rahisi kupatikana, visivyo vya bei kubwa. Kwa kujaribujaribu, waweza kuifanya nyumba isiyo na vitu vya bei kubwa kuwa ya kupendeza na kuvutia macho, kama pakiwako upendo na moyo wa kuridhika. Raha haipatikani katika mambo ya kujionyesha tu. Utaratibu wa mambo ya watu wa nyumbani ukiwa mwepesi ndivyo nyumba hiyo itakavyozidi kuwa ya furaha. Si lazima kuwa na mastakimu na vyombo vya gharama kubwa kusudi kuwaridhisha watoto na kuwapendeza nyumbani kwao, lakini ni jambo la muhimu kuwaonyesha upendo na malezi mazuri. 1131-155; KN 170.5

Mnapaswa siku zote kushirikikiana mali nyumbani mwenu. Kumbukeni kuwa mbinguni hakuna machafuko, na ya kuwa nyumba yenu ingekuwa kama mbinguni mkiwa bado mngali hapa chini. Kumbukeni kuwa kwa kufanya kwa uaminifu siku kwa siku mambo yale madogo madogo ya kufanywa nyumbani, mwatenda kazi pamoja na Mungu, mkithibitisha tabia ya Kikristo. Kumbukeni wazazi, kwamba mnauhudumia wokovu wa watoto wenu. Ikiwa mazoea yenu ni safi, yasiyo na makosa, kama mwaonyesha umaridadi na utaratibu, sifa nzuri na haki, utakaso wa roho, mwili na moyo, mwayatii maneno ya Mkombozi, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” KN 171.1