Go to full page →

Haifai Lugha Yetu ya Asili Kudharauliwa KN 238

Katika kila sehemu ya mafundisho yako mambo ambayo yapasa kuonekana kuwa ni yenye faida zaidi ya yale yapatikanayo kwa elimu ya ufundi mtupu. Mathalan, mtu kuweza kuandika na kusema lugha ya kwao kwa urahisi na ufasaha ni jambo la maana zaidi ya elimu ya lugha za kigeni, zinazotumika au zile zilizokwisha kufa; lakini, hakuna elimu inayopatikana kwa njia ya sarufi iwezayo kulinganishwa thamani yake na mafundisho ya lugha kama ubora wake uonekanavyo. Hali njema ama hali nyonge kabisa hufungamana sana na mafundisho hayo. 39ED.234 ; KN 238.6