Go to full page →

Majani ya Chai na Kahawa Haviutii Mwili Afya KN 121

Chai (kinywaji kinachotengenezwa kwa majani ya chai hasa) hufanya kazi mwilini kama kileo, nayo ikitumiwa zaidi inaleta kulewa. Kahawa na vinywaji vingine vipendwavyo na watu wengi vinaleta matokeo ya jinsi hii. Kwanza matokeo yake ni kufurahisha. Mishipa ya fahamu inashtuliwa tumboni; nayo inafikisha mchocheo wake mpaka kwenye ubongo, nao huamshwa na kuongeza mapigo ya moyo, na mwili mzima huwa kama ukizidishiwa nguvu, lakini siyo nguvu halisi, nayo inadumu muda mfupi tu. Uchovu unasahauliwa, na inaonekana kana kwamba nguvu za mwili zimeongezeka. Akili zinaamshwa na mambo yale yasiyoelekea kuwa kweli, yanakuwa kana kwamba ni kweli. KN 121.4

Kwa sababu matokeo ya namna hii watu wengi wanadhani kwamba chai au kahawa inawafaa sana. Lakini hili ni kosa. Chai na kahawa hazisadii kuuulisha mwili hata kidogo. Matokeo yao huwa kabla ya kuyeyushwa na kutulia tumboni, na hali inayoonekana kuwa na nguvu ni mshtuo wa neva tu. Nguvu za kileo zinapomalizika ndipo nguvu za mwili zisizokuwa za kawaida zinapungua, na matokeo yake ni uchovu na udhaifu mwingi. KN 121.5

Kuendelea kuvitumia vileo hivi kunaleta maumivu ya kichwa, kukosa usingizi, kiherehere cha moyo, maumivu ya tumbo, kutetemeka, na mabaya mengi mengineyo; kwa kuwa vinadhoofisha nguvu mwilini. Mishipa ya fahamu (neva) ikichoka inahitaji kupumzishwa badala ya kuchochewa na kutumikishwa kupita kiasi. 18MH 326, 327; KN 121.6

Wengi wameasi dini na kuzizimua nguvu za mwili kwa chai na kahawa. Wale wazivunjao kanuni za afya watapofushwa akilini mwao na kuivunja sheria ya Mungu. 19Te 80; KN 122.1