Go to full page →

Kutumia Madawa Ya Sumu KN 122

Tendo moja ambalo ni sababu ya magonjwa mengi, na madhara mengi ni kutumia namna za dawa zenye sumu bila kiasi. Kuna watu wengine ambao wakishikwa na ugonjwa fulani, hawajisumbui kupeleleza asili ya ugonjwa. Wanashughulika tu wawezavyo kuyatuliza maumivu na masumbufu yao. KN 122.2

Kwa kutumia dawa zenye sumu, wengine hujiletea magonjwa ya maisha, na watu wengi hufa ambao wangeendelea kuishi kama wangetumia njia halisi za kuponya magonjwa yao. Sumu iliyomo ndani ya namna nyingi za dawa zisizoponya kwa kweli huanzisha tamaa na mazoea yanayoharibu roho na mwili. Namna nyingi za dawa za siri zinazopendwa na wengi, na hata namna nyingine mazoea fulani katika maisha, kama vile kutumia vileo, afyuni, na bangi, ambayo ni mazoea mabaya zaidi yanayokuwa fedheha kwa wanadamu. 20MH 127; KN 122.3

Kuyatibu magonjwa kwa kutumia dawa zile zenye sumu (drugs), kama inavyotumika kwa kawaida, ni laana. Jizoeze kuepukana na dawa hizi zenye sumu. Usizitumie ila kwa nadra sana, na tegemea zaidi juu ya njia kuu za kujipatia afya; ndipo mwili utafaidiwa na dawa za Mungu - hewa safi, maji safi, mazoezi mazuri ya viungo vya mwili, dhamiri safi. Wale wanaoendelea kutumia majani ya chai, kahawa na nyama wataona kuwa inawabidi kupata dawa hizi zenye sumu, lakini wengi waweza kupona pasipo kutumia hata kidonge kimoja cha dawa kama wakizitii kanuni za afya. Dawa zenye sumu zisitumiwe ila kwa nadra tu. 21CH 261. KN 122.4