Sura hii imejengwa katika Kutoka 19, 20, 25-40.
Kutangazwa kwa Sheria ya Mungu Mlimani Sinai-Baada ya Bwana kuwapatia watu wa Israeli ushahidi wa jinsi hiyo wa uwezo wake, aliwaambia kuwa yeye ni nani: “Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa..” Mungu yule yule aliyedhihirisha uwezo wakemiongoni mwa Wamisri sasa alitamka sheria yake: PLK 43.1
“Usiwe na miungu mingine ila mimi.” “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. PLK 43.2
“Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. PLK 43.3
“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. PLK 43.4
“Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. PLK 44.1
“Usiue. PLK 44.2
“Usizini. PLK 44.3
“Usiibe. PLK 44.4
“Usimshuhudie jirani yako uongo. PLK 44.5
“Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.” PLK 44.6
Amri ya kwanza na ya pili ambazo Yehova alizitamka zinakataza ibada ya sanamu, kwa sababu kuabudu sanamu kungewaongoza watu katika kujaribu dhambi nyingi na kuwa na matokeo ya kutoa kafara za wanadamu. Mungu anapenda kuzuia hata uwezekano mdogo kabisa wa kuyakaribia machukizo kama hayo. Amri nne za mwanzo zilitolewa ili kuwaonesha watu wajibu wao kwa Mungu. Amri ya nne ni kiungo cha muhimu baina ya Mungu mkuu na wanadamu. Sabato ilitolewa mahususi kwa ajili ya manufaa ya wanadamu na heshima ya Mungu. Amri sita za mwisho zinaonesha wajibu wetu mtu kila mmoja kwa mwenzake. PLK 44.7
Sabato ilikuwa iwe ni ishara baina ya Mungu na watu wake milele. Kwa jinsi hii ilikuwa iwe ni ishara- wote ambao wangeishika Sabato kwa kufanya hivyo wangeonesha kuwa walikuwa ni wacha Mungu aliye hai, muumbaji wa mbingu na dunia. Sabato ilikuwa iwe ni ishara baina ya Mungu na watu wake maadamu angekuwa na watu duniani wanaomtumikia. PLK 44.8
“Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima ukitoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. Wakamwambia Musa, ‘Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa.’ PLK 44.9
“Musa akawaambia watu, ‘Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.’ Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo. PLK 45.1
“Bwana akamwambia Musa, ‘Waambie wana wa Israeli hivi: “Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.” ‘ ” Kuwepo kwa Mungu kwa utukufu pale Sinai, na ghasia katika nchi iliyosababishwa na kuwepo kwake, ngurumo za kutisha na radi zilizoambatana na ziara hii ya Mungu, ziliathiri sana akili za watu kwa hofu na kicho kutokana na ukuu wake mtakatifu kiasi kwamba walirudi nyuma bila kufikiri kutoka eneo la kuwepo kwa Mungu wa kuogofya, wakiogopa kwamba wasingeweza kustahimili utukufu wake wa kutisha. PLK 45.2
Hatari ya Kuabudu Sanamu-Kwa mara nyingine, Mungu, alitaka kuwalinda Waisraeli kutokana na ibada ya sanamu. Aliwaambia, “Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.” Walikuwa katika hatari ya kuiga mfano wa Wamisri, wakijitengenezea sanamu za kumwakilisha Mungu. PLK 45.3
Mungu alitaka watu wake wafahamu kwamba yeye peke yake yapasa awe shabaha ya ibada yao. Pale ambapo wangewashinda mataifa ya waabudu sanamu waliowazunguka, hawakutakiwa kuhifadhi hata moja ya sanamu walizoziabudu, bali kuziharibu kabisa. Miongoni mwa miungu hii ya wapagani mingi ilikuwa ya gharama kubwa sana na kazi nzuri za ustadi, ambazo zingeweza kuwavutia waliowahi kushuhudia ibada ya sanamu, iliyokuwa ya kawaida mno kule Misri, hata kuwafanya wavizingatie vitu hivi visivyo na akili kwa kiwango fulani cha kicho. Bwana alitaka watu wake wafahamu kuwa ilikuwa ni kwa sababu ya ibada ya sanamu ya mataifa haya, ambayo iliwaongoza katika kila kiwango cha uovu, angewatumia Waisraeli kama vyombo vyake vya kuwaadhibu na kuiangamiza miungu yao. Baada ya Musa kupokea hukumu kutoka kwa Bwana na kuziandika kwa ajili ya watu, pamoja na ahadi kwa sharti la utii, Bwana alimwambia, ” ‘Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikilie Bwana; mkasujudie kwa mbali; na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na Bwana; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye.’ PLK 45.4
“Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, ‘Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda.’” Kutoka 24:1-3. PLK 46.1
Musa aliandika, si Amri Kumi, bali hukumu ambazo Mungu alitaka wazitunze na ahadi zilizokuwa na sharti katika utii wao kwake. Alisoma hizi kwa watu, nao waliahidi wao wenyewe kutii maneno yote Bwana aliyoyasema. Musa kisha aliandika ahadi yao ya dhati katika kitabu na kutoa dhabihu kwa Mungu kwa ajili ya watu. “Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, ‘Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.’ Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, ‘Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.’” Watu walirudia ahadi yao kwa Bwana ya kufanya yote ambayo alikuwa ameyasema na kwamba watatii. Kutoka 24:7, 8. PLK 46.2
Sheria ya Mungu ya Milele-Sheria ya Mungu ilikuwapo kabla wanadamu hawajaumbwa. Malaika waliongozwa nayo. Shetani alianguka kwa sababu alihalifu kanuni za serikali ya Mungu. Baada ya Mungu kumwumba Adamu na Hawa, aliwajulisha sheria yake. Bado ilikuwa haijaandikwa, lakini Yehova aliifiindisha kwao. PLK 46.3
Katika Edeni Mungu alianzisha Sabato ya siku ya amri ya nne. Baada ya Mungu kuumba ulimwengu na kuwaumba wanadamu juu ya nchi, aliwafanyia Sabato. Baada ya dhambi na anguko la Adamu katika dhambi hakuna hata kitu kimoja kilichoondolewa katika sheria ya Mungu. Kanuni za Amri Kumi zilikuwapo kabla ya anguko na zilifaa kwa ajili ya utaratibu mtakatifu wa viumbe. Baada ya anguko kanuni za amri zile hazikubadilishwa, bali Mungu alitoa sheria za nyongeza ili kuwafaa watu katika hali yao ya anguko. PLK 46.4
Mungu alianzisha mfumo unaohitaji kuwatoa wanyama kuwa kafara, ili kuweka mbele ya wanadamu walioanguka ukweli ambao nyoka alimfanya Hawa asiuamini: kwamba mshahara wa kutokutii ni mauti. Uvunjaji wa sheria ya Mungu ulifanya iwe lazima Kristo kufa kama kafara na hivyo kufanya njia ya uwezekano wa wenye dhambi kuokoka na adhabu hiyo na bado kudumisha heshima ya sheria ya Mungu. Mfumo wa kafara ulikuwa uwafundishe wenye dhambi unyenyekevu, katika hali yao ya anguko, na kuwaongoza katika toba na kumtumainia Mungu peke yake, kupitia kwa Mkombozi aliyeahidiwa, kwa ajili ya msamaha kwa kuhusu uhalifu uliopita wa sheria yake. Kama kusingekuwapo na uvunjaji wa sheria ya Mungu, kamwe kusingekuwapo mauti, na kusingekuwapo na hitaji la sheria za ziada za kukabiliana na hali ya mwanadamu ya anguko. PLK 47.1
Adamu aliwafundisha uzao wake sheria ya Mungu, ambayo ilirithishwa kwa waaminifu kupitia katika vizazi vilivyofuatana. Uhalifu wa daima wa sheria ya Mungu ulisababisha gharika ya maji juu ya nchi. Nuhu na familia yake waliihifadhi sheria ile, na kwa sababu ya matendo yao mema waliokolewa ndani ya safina kwa muujiza wa Mungu. Nuhu aliwafundisha uzao wake Amri Kumi. Kuanzia kwa Adamu na kuendelea, Bwana aliwahifadhi watu kwa ajili yake, ambao katika mioyo yao mlikuwamo sheria yake. Kuhusu Ibrahimu alisema, “Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.” Mwanzo 26:5. PLK 47.2
Bwana alimtokea Ibrahimu na kumwambia: “Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu ukawe mkamilifu. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.” Mwanzo 17:1,2. “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.” Mwanzo 17:7. PLK 48.1
Ndipo alipohitaji tohara kwa Ibrahimu na uzao wake, ambayo ilikuwa ni mduara uliokatwa katika nyama, kama ishara kwamba Mungu alikuwa amewakata na kuwatenganisha kutoka katika mataifa yote kama tunu yake ya pekee. Kwa ishara hii walikuwa wanaahidi kwa dhati kwamba wasingeoana na mataifa mengine, kwa sababu kwa kufanya hivyo wangepoteza kicho chao kwa Mungu na sheria yake takatifu na wangekuwa kama mataifa ya waabudu sanamu waliowazunguka. PLK 48.2
Kwa tendo la tohara, walikuwa wamekubali kwa dhati kutimiza kwa upande wao masharti ya agano lililofanywa na Ibrahimu, la kutengana kutoka kwa mataifa yote na kuwa wakamilifu. Iwapo uzao wa Ibrahimu wangedumu kujitenga kutoka kwa mataifa mengine, wasingeweza kushawishiwa kuingia katika ibada ya sanamu. Kwa kujitenga kutoka kwa mataifa mengine, wangeweza kuliondoa jaribu kubwa la kujiingiza katika mazoea ya dhambi ya mataifa yale na hivyo kuasi dhidi ya Mungu. Kwa kiasi kikubwa, walipoteza tabia yao iliyokuwa tofauti na takatifu kwa kujichanganya na mataifa yaliyowazunguka. Katika kuwaadhibu, Bwana alileta njaa juu ya nchi, iliyowalazimisha kwenda Misri ili kuhifadhi maisha yao. Lakini kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Mungu hakuwaacha walipokuwa katika Misri. Aliruhusu waonewe na Wamisri, ili wapate kumgeukia Mungu katika dhiki yao, kuchagua haki yake na serikali yake ya rehema, na kutii masharti yake. PLK 48.3
Kulikuwako na familia chache tu ambazo kwanza zilikwenda Misri. Familia hizi ziliongezeka kwa idadi. Baadhi ya familia walikuwa waangalifu katika kuwaelekeza watoto wao katika sheria ya Mungu, lakini Waisraeli wengi walikuwa wameshuhudia mno ibada ya sanamu hata fikira zao kuhusu sheria ya Mungu zikakanganyika. Wale waliomheshimu Mungu walimlilia kwa uchungu wa roho ili apate kukomesha utumwa wao na kuwatoa katika nchi ya kutumikishwa kwao ili wapate kuwa huru kumtumikia yeye. Mungu alisikia vilio vyao na kumwinua Musa kama chombo chake cha kuwakomboa watu wake. Baada ya kuondoka Misri na Mungu kuwa amegawanya maji ya Bahari ya Shamu mbele yao, Bwana aliwapa jaribio kuona kama wangeweza kumtumainia yeye aliyewachukua kama taifa kutoka katika taifa lingine, kwa ishara majaribio, na maajabu. Lakini walishindwa mtihani. Walinung’unika dhidi ya Mungu kwa sababu ya magumu njiani, na walitaka kurudi Misri. PLK 49.1
Iliyoandikwa katika Mbao za Mawe-lli kuwaacha bila udhuru wo wote, Bwana mwenyewe alijishusha akaja juu ya Mlima Sinai, akiwa amefunikwa katika utukufij na kuzungukwa na malaika zake. Kwa utukufu na namna ya kuvutia sana aliwajulisha sheria yake ya Amri Kumi. Hakuruhusu zifundishwe na mwanadamu ye yote, wala hata malaika zake, bali alitamka sheria yake yeye mwenyewe kwa sauti ambayo watu wote wangeweza kusikia. Hata hapo, hakuweza kuzikabidhi ili zitunzwe katika kumbukumbu za muda mfupi za watu ambao walielekea kusahau masharti yake, bali aliziandika kwa kidole chake mwenyewe katika mbao za mawe. Alitaka kuzuia uwezekano wo wote kwamba wangechanganya mapokeo yo yote na sheria yake takatifu au kukanganya masharti yake na mazoea ya wanadamu. Kisha akaja karibu zaidi na watu, ambao walikuwa rahisi sana kupotoshwa, na asingewaacha na kanuni za Amri Kumi peke yake. Akamwamuru Musa kuandika hukumu na amri kwa maelekezo ya Mungu, akitoa maelekezo kinaganaga kuhusu kile alichotaka watende. Kwa njia hii alizilinda amri zile kumi alizozichora katika mbao za mawe. Alitoa maelekezo na masharti haya mahususi ili kuwavuta wanadamu wanaokosea kutii sheria ya maadili, ambayo huwa wana mwelekeo mkubwa wa kuivunja. PLK 49.2
Kama wanadamu wangeishika sheria ya Mungu, kama ilivyotolewa kwa Adamu baada ya anguko lake, ikatunzwa katika safina na Nuhu, na kutunzwa na Ibrahimu, kusingelikuwapo na hitaji la kaida ya tohara. Na iwapo uzao wa Ibrahimu wangelitunza agano ambalo tohara iliwakilisha, kamwe wasingelikwenda katika ibada ya sanamu au kuruhusiwa kwenda Misri, na kusingelikuwapo haja ya Mungu kutangaza sheria yake kutoka Sinai, kuichora juu ya mbao za mawe, na kuitunza kwa maelekezo mahususi katika hukumu na amri za Musa. PLK 50.1
Hukumu na Amri-Musa aliziandika hukumu na amri zilizotoka katika kinywa cha Mungu wakati alipokuwa pamoja naye juu ya Mlima Sinai. Ikiwa watu wa Mungu wangetii kanuni za Amri Kumi, wasingehitaji maelekezo mahususi ambayo Mungu alimpatia Musa kuhusu wajibu wao kwa Mungu na mtu kwa mwenzake, ambayo aliyaandika katika kitabu. Maelekezo ya wazi ambayo Bwana alimpa Musa kuhusu wajibu wa watu wake kila mtu kwa mwenzake na kwa mgeni ndio kanuni za Amri Kumi, zikiwa zimerahisishwa na kutolewa katika namna ya waziwazi, ili wasije wakazikosea. PLK 50.2
Bwana alimwelekeza Musa wazi kuhusu taratibu za kafara ambazo zilikuwa zikome wakati wa kifo cha Kristo. Mfumo wa kafara ulionesha kwa ishara kafara ya Kristo kama Mwanakondoo asiye na waa. PLK 50.3
Kwanza Bwana alianzisha mfumo wa dhabihu za kafara kwa Adamu baada ya anguko lake, na Adamu aliwafundisha uzao wake. Mfumo huu ulipotoshwa kabla ya Gharika, na pia na wale waliojitenga kutoka kwa wafuasi waaminifii wa Mungu na kujenga mnara wa Babeli. Walitoa kafara kwa miungu waliojitengenezea wao wenyewe badala ya kwa Mungu wa mbinguni. Wal i toa dhabihu zao si kwa sababu walikuwa na imani kwa Mkombozi ajaye bali kwa sababu walidhani iliwapasa kuwapendeza miungu yao kwa kutoa kafara nyingi sana za wanyama juu ya madhabahu yao yaliyonajisiwa ya ibada za sanamu. Ushirikina wao uliwaongoza katika ubadhirifu mkubwa mno. Waliwafundisha watu kwamba kadiri thamani ya dhabihu ilivyokuwa kubwa ndivyo ambavyo ingezipendeza sanamu za miungu na ndivyo ambavyo mafanikio na utajiri wa taifa lao yangekuwa. Kwa hiyo, wanadamu mara kwa mara walitolewa kama kafara kwa hizi sanamu zisizo na akili. Ili kutawala matendo ya watu, mataifa yale yalikuwa na sheria na kanuni zilizokuwa za kikatili mno. Viongozi ambao mioyo yao haikulainishwa kwa neema ndio waliokuwa watengenezaji wa sheria zao. Wakati ambapo wangepuuza makosa yenye kushusha hadhi mno, kosa dogo lingetokezea katika adhabu ya kikatili mno kutoka kwa wale walio katika madaraka. PLK 51.1
Musa alikuwa na haya akilini mwake alipowaambia Israeli, “Bali ninyi mlioambatana na Bwana, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo. Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki. Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.” Kumbukumbu la Torati 4:5-8. PLK 51.2