Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya Kumi na Moja—KUOMBA NI FARADHI YETU

    Mungu hutumia njia nyingi kwa kusema nasi, yaani kwa viumbe vyake kwa kuwafunulia wanadamu mambo yajayo, kwa maongozi yake, na kwa mvuto wa Roho yako Mtakatifu. Lakini hata njia hizi zote hazitoshi; hata na sisi pia imetupasa kumtolea Mungu yote yaliyomo mioyoni mwetu. Imetulazimu kuongea na Baba yetu aliye mbinguni, ili tupate uzima na nguvu za kiroho. Na kama twataka kuongea na Mungu, sharti tuwe na mambo ya kumwambia, hasa juu ya maisha yetu.HUK 42.1

    Katika kuomba tunamfunulia Mungu mioyo yetu na kuongea naye kama tunavyoongea na rafiki wa kweli. Si lazima kufanya hivyo ili kumjulisha Mungu hali yetu ilivyo, bali kuongea naye kunatuwezesha kumpokea Mungu mioyoni mwetu. Sala hazimlazimishi Mungu kushuka kwetu, bali ni sisi ndio tunaoinuliwa mpaka kufika kwake.HUK 42.2

    Yesu alipokuwa hapa duniani, aliwafundisha wanafunzi wake kusali. Aliwaagiza waweke mbele ya Mungu upungufu wao na mahitaji yao ya kila siku, na kumtupia mashaka yao na mahangaiko yao yote, Tena alivyowaahidia wanafunzi wake kwamba maombi yao yatakubaliwa, basi ahadi ile imekuwa yetu pia; yaani, anatuahidi nasi kuwa sala zetu zitakubaliwa.HUK 42.3

    Yesu mwenyewr, alipokaa na wanadamu, aliomba kwa kawaida. Mwokozi wetu alijishirikisha mahitaji yetu na udhaifu wetu; kwa hivi akawa mhitaji na mwombaji, akimwomba Baba yake apate nguvu za kufanya kazi yake na kuyashinda majaribu yatakayompata. Yeye ndiye mfano wetu katika mambo yote. Ni ndugu yotu ashirikiye udhaifu wetu,“alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote;” lakini kwa sababu alikuwa safi bila dhambi, akayaepuka maovu nafsini mwake, Katika hali yake ya kibinadamu, kuomba kulikuwa ni faradhi yake iliyomhusu, nayo tena akapata faraja na furaha katika kuongea na Baba yake. Na ikiwa Mwokozi wetu, nayo Mwana wa Mungu, aliona amehitaji kuomba, basi sisi, tulio wanadamu dhaifu wenye dhambi, tunahitaji zaidi sana kufanya bidii katika kuomba kwa kawaida. Baba yetu aliyo mbinguni huwa anangoja kutubariki. Mungu yu tayari kusikiliza maombi ya kweli ya kila mtoto wake, walakini sisi hatuna moyo sana wa kumwambia Mungu haja yetu.HUK 42.4

    Giza la Shetani huzungusha wale wasiofanya bidii katika kuomba. Adui yao, Shetani, huwashawishi kufanya maovu, nao kwa sababu ya kuacha kuomba hawana nguvu kushindana naye, Mbona watu wa Mungu hutupa mbali faradhi yao ya kuomba, ijapokuwa kuomba ni kama ufunguo nikononi mwa waaminifu wa Mungu kuwafungulia msaada wote na mibaraka yote ya Mungu isiyo na kiasi. Pasipo kuomba siku zote na kukesha kwa uangalifu, tunajitia katika hatari ya kuwa walegevu wa mambo ya kiroho na kupotewa na njia iliyo haki.HUK 42.5

    Kuna masharti mengine juu yetu ambayo ni wajibu wetu, ili tuweze kutumaini ya kuwa Mungu atatusikia na kutujibu mommbi yetu. Sharti moja ni hili; lazima tufahamu jinsi tunavyohitaji msaada wake. Ameahidi, “Nitamimina maji juu yake mwcnye kiu, na mito juu ya pakavu.” Isa.44:5. Wale wenye njaa na kiu ya haki, wamtakao Mungu sana, watashiba. Lakini baraka za Mungu haziwezi kupatikana ila kwanza moyo uwe umefunguliwa na Roho Mtakatifu kuingia. Bwana wetu hujua haja zetu, lakini imetupasa kutambua haja zetu sisi wenyewe na kumwomba Mungu mambo hayo. Asema, “Oubeni na mtapewa.” Mattayo 7:7. Tena “Yeye asiyemwachilia Mwana wake yey, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja naye Warumi 8:32.HUK 43.1

    Tukiwa tunaangalia maovu moyoni na kuyashikilia, Mungu hawezi kutusikia maombi yetu; lakini mwenye kutubia kosa lake, maombi yake yanakubaliwa mara moja. Hatuwezi sisi kujistahilisha machoni pa Mungu kwa matendo mema yetu; ustahilifu wake Yesu ndio utakaotuokoa sisi, na damu yake ndiyo itakayotutakasa; hata hivyo kuna masharti juu yotu pia ili tukubaliwe na Mungu.HUK 43.2

    Sharti jingine juu yetu ni kuwa na imani. “Pasipo imani haiwezekani kumpendeza (Mungu): kwa maana mtu ampendezaye Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Waeb.l1:6. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24. Jo, twayasadiki maneno yake ?HUK 43.3

    Kama tunakosa kupata mambo yale yale tuliyoyaomba, kwa wakati ule ule tuombao, hata hivyo tukubali ya kwamba Mungu hutusikia, tena atatujibu maombi yetu. Kwa ajili ya upungufu wetu, pengine twamwuliza Mungu mambo yasiyotufaa, naye Baba yetu wa mbinguni hutujibu maobi na kutupa sisi mambo yale yanayokuwa bora kwetu, - ambayo sisi wenyewe tungeyataka kama tungeweza kuona mambo yote jinsi yalivyo kama Mungu aonavyo. Hata kama inaonekana kwamba maombi yetu hayajibiwi, tutazidi kuendelea kutumaini ahadi yake; kwa kuwa bila shaka atatujibu baadaye, nasi tutapata mbaraka ule ule unaotupasa. Lakini kusema ya kwamba Mungu hana budi kutujibu maombi tu tunaycomba na kutupa sisi yale yale tunayoyataka, - ni kama kujidai bila haki na kumfanyie Mungu kiburi. Mungu ni mwenye busara asiyeweza kufanya kosa, tena yu mwema; kwa hivyo hawanyini waaminifu wake jambo joma lo lote. Heri tutegenee ahadi yake ya kweli, “Ombeni na mtapewa.”HUK 43.4

    Tunapomwendea Mungu na kumwomba msamaha na mbaraka wake, imetupasa kuwa na moyo wa upondo na kusameho wengine, Twaweza je kuomba hivi,“Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavycwasamehe waliotukosa,” na sisi katika roho zotu tungali hatukubali kuwasameho wengine. Tukitumaini kujibiwa naonbi yotu, sharti tuwe na roho ya kuwasamehe wengine kana vile sisi tunavyotaraji kusamehewa.HUK 43.5

    Kudumu katika kuomba ni sharti jingine juu ya kujibiwa maombi. Kana tunataka kuongeza imani na kuwa watu wazima katika Kristo, imetupasa kuomba siku zote; “katika kusali, mkidumu;” “dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani.” Warumi 12:12; Wake 1.4:2. Petro awausia Wakristo, “Mwe na akili, mkakeshe katika sala.” 1 Petro 4:7. Mtume Paulo awaagiza hivi, “Katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu zijulike kwa Mungu.” Wafil.4:6. Na Yuda pia asema,“Ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu.” Yuda 20,21. Katika kudumu kuomba, roho zetu hufungamana kuwa moja na Mungu, ili tupate uzima utokao kwake; na maisha yetu huwa safi machoni pake.HUK 44.1

    Sharti tufanye bidii katika kuomba; tusikubali kitu cho chote kutuzuia kuomba. Shika kila nafasi ya kwenda mahali ambapo watu huzoea kuomba. Wale watakao kushirikiana na Mungu kweli, wataonekana kila mara kwenye mkutanc wa kusali; watakuwa waaminifu katika kufanya iliyo wajibu wao, pia watakaza mioyo yao kupata msaada wote wa Mungu unaowahusu.HUK 44.2

    Sharti tuombe pamoja na watu wa nyumbani; na zaidi ya yote tusiwe wavivu katika kuomba faraghani peke yetu, maana kufanya hivyo ndio asili ya uzima wa roho. Kusali hadharani mwa watu peke yake hakutoshi. Yatupasa kumfunulia Mungu mioyo yetu katika faragha, ambapo maombi yetu yatasikiwa na Mungu bila shaka; maana hapo tuna nafasi kumwonyesha mambo yetu yote. Katika sala ya upweke roho zetu hupata nguvu ya kustahimili katika kushindana na Shetani. Mungu ndiye nguvu zotu.HUK 44.3

    Omba faraghani; tena katika kufanya kazi yako, umwinulie Mungu moyo wake. Hivyo ndivyo Enoku alivyopata kuendelea pamoja na Mungu. Shetani. hawezi kamwe kumshinda yule ambaye moyo wake humtegemea Mungu hivi.HUK 44.4

    Hakuna wakati wala mahali pasipofaa kumwomba Mungu. Hakuna kinachoweza kutuzuia tusimwinulie mioyo yotu katika kuseli. Kati ya watu njiani, hata katika kufanya kazi yetu, twaweza kumwemba Mungu msaada wake ma uongczi wake, kama alivyofanya Nehemia alipomtolea mfalme Artashashta haja yake. Heri tumkaribishe Yesu aje akae mioyoni mwetu daima. Wale ambao mioyo yao i wazi kwa kupata msaada na mbaraka wa Mungu, hao wamo ulimwenguni kweli, lakini si watu wa ulimwengu sababu hawayapandi kuyafuata mambo na anasa za dunia. Hao nao hupatana na mambo ya mbinguni na kushirikiana na Mungu.HUK 44.5

    Mwonyeshe Mungu mahitaji yako, furaha zako, uzito wako, mashaka yako na hofu zako. Huwezi kumwudhi Mungu wala kumchosha. Yeye ambaye huhesabu nywele za kichwa chako, hawezi kutojali mahitaji ya watoto wake. “Biwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.” Yak.5:11. Moyo wake wa upendo huingiwa na huruma kwa ajili ya huzuni na uzito wetu. Mwambie mambo yote yanayofadhaisha moyo. Hakuna msiba uwezao kumpata hata mtoto wake aliye mdogo, wala jambo linalimhangaisha au kumfurahisha, pia hakuna maombi yatokayo moyoni mwa mmo jawapo wa watu wake, ila Baba yetu aliye mbinguni huyacnna yote na kusikia mara mmoja. Huyaangalia na kuyajali mambo yote yanayohusika na watu wake. “Huwaponya waliopondeka mayo, huziganga jeraha zao.” Zab. 147:3. Mungu humfikiria na kumwangalia kila mtu kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kumshugulikia ila yeye tu ambaye Mwana wake Mpendwa alikufa kwa ajili yake.HUK 45.1

    Yesu alisema, “Mtaomba kwa jina langu wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaomboa Baba: kwa maana Baba. mwenyewe awapenda ninyi.” Yoh.16:26,27. “Mini niliyewachagua ninyi,...ili lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu, awapeni.” Yoh.15:16. Na kuomba kwa jina la. Yesu, maana yake siyo kulitaja tu jina lake katika mwanzo na mwisho wa sala. Maana yako ni hivi: katika kuomba kwetu tuwe na nia na roho ndani yetu iliyokuwaao ndani ya Yesu na kuziamini ahadi zake, kutagemea neoma yako, na kutenda matondo ya nanna yako,HUK 45.2

    Maisha yetu lazima kufanana na maisha yake Kristo, kwa kuomba na kufanya kazi pia. Yeye aombaye tu kila mara bila kufanya kazi yo yote, hatimaye maombi yake yatakuwa. yasiyo maana. Wa1e wasiomtumikia, Yesu aliyewatumikia wao sana, hawana mambo yafaayo kuombwa, wala hawana sababu ya kusali. Watu kama hao hujifikiria nafsi zao wenyewe tu. Hawawezi kuwaombea wengine na kufikiri mahitaji yao, wala kuendesha ufalme wa Kristo na kupata nguvu kumtendea kazi yake ya Injili.HUK 45.3

    Tunaona upungufu kama tunakosa kushirikiana na wengine kwa kujiimarisha mioyo yetu wenyewe kwa wenyewe katika kumtumikia Mungu. Katika kushirikiana na kuongea kwetu sisi Wakristo twapata upungufu mkubwa sana kwa ajili ya kutokuwa na huruma sisi kwa sisi kama inavyotupasa. Katika kuandamana na watu na kufanya urafiki wa kweli nao, na kujua mambo yap, tunapata kuwahurumia wengine katika haja zao na misiba yao; pia ni njia ya kusitawi kiroho na kupata nguvu sisi wenyewe kwa kumtunikia Mungu.HUK 45.4

    Kama Wakristo wangekuwa wanashirikiana sawa sawa, na kuongea juu ya upendo wa Mungu na manbo yanyayohusika na ukombozi, mioyo yao wenyewe ingeburudika pia wangewaburudisha wengine mioyo yao. Kana tungezidi kumfikiri Yesu na kuongea juu yake, na kutofikiri sana nafsi zetu, Yesu angezidi kuwapo pamoja nasi.HUK 45.5

    Kama tungemwaza Mungu kila mara kama vile Mungu anavyotuonyesha uangalifu wake kwetu, angekuwa katika fikara zetu milole. Twazoea kuongea juu ya mambo ya dunia hii kwa kuwa tunahusika nayo na kupendezwa nayo. Twaongea juu ya rafiki zetu sababu twawapenda. Mambo yotu, furaha zetu, huzuni zetu, zatuhusu sote, sisi na rafiki zetu pia. Lakini imekuwa wajibu wetu kumpenda Mungu zaidi, kwa kuwa ametufanyia mema mno; ingefaa kuwa desturi na kawaida yetu kumfikiri Mungu zaidi ya wengine wote, na kuongea juu ya wema wake na uwezo wake.HUK 46.1

    Ni wajibu wetu kumshukuru Mungu zaidi kwa ajili ya “rehema zake na miujiza yake kwa wanadamu.” Zab. 107:8. Asili ya kumwabudu Mungu si kutaka na kupata mahitaji yetu hasa. Tusifikiri juu ya haja zetu tu, bila kufikiri mibaraka tunayoipata. Sisi hatuombi zaidi kupita kiasi, lakini tunakosa kumtoloa Mungu shukrani kwa kiasi ipaswayo. Twapata rehema zake daima, walakini tunamshukuru kwa uchache tu kwa yote anbayo ametutendea.HUK 46.2

    Katika siku za zamani, Waisraeli walipokutana katika mkutano wo dini, Mungu aliwaagiza hivi:“Ndipo mtakapokula mbele ya Bwana Mungu wenu, nanyi mtafurahia kila mtakazotia mikono, ninyi na nyumba zenu, alizokubarikia Bwana Mungu wako.” Kumbu.l2:7. “Yote yatendwayo kwa kumtukuza Mungu yafaa kutendwa kwa furaha, na shangwe, na shukrani, siyo kwa huzuni na moyo mzito.HUK 46.3

    Mungu wetu ndiyo Baba mwenye huruma na rehema. Imewapasa watu wake kumfurahia katika kumwabudu, Mungu na kumtumikia. Yeye, ambaye amewawekea watoto wake wokovu mkuu, hataki wamtumikie kama angekuwa msimamizi wa utumwa, mkali, asiye na huruma. Mungu ndiye rafiki yao aliye bora zaidi; na wanapomwabudu naye hutumaini kuwa pamoja nao, kusudi awabariki na kuwafariji, akijaza mioyo yao furaha na upendo, Mungu ataka watoto wake waburudike moyo katika huduma yake, tena wasione kazi yake kuwa ni ngumu sana, bali wapate kupendezewa katika kumtumikia. Hata na wale wanaokutana kumwabudu, Mungu hutaka wapate kufikiri juu ya uangalifu na upendo wako, ili wachangamshwe moyo katika mambo yote ya maisha yao, na kufanya yote kwa haki na uaminifu.HUK 46.4

    Kristo naye amesulubiwa, na hili ni jambo la kufikiriwa sana, lipasalo kuwa jambo kubwa katika maongezi yetu. Imetupasa kukumbuka mibaraka yote tunayoipata mkononi mwa Mungu; na kama tunafahamu upendo wake mkubwa usio na kifani, basi tukubali kumwekea amana mambo yetu yote, yule aliyosulubiwa kwa ajili yetu.HUK 46.5

    Huko mbinguni Mungu husujudiwa kwa nyimbo na shangwe. Nasi tunapomtolea Mungu shukrani yetu, tunamtukuza kama vile anavyotukuzwa na majeshi ya mbinguni. “Atoaye za kushukuru, ndiyo anitukuzaye.” Zab.50:23. Hivyo tufike mbele zako “kwa zaburi na tenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote.” Soma Isa.51:3; Wae.5:19.HUK 46.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents