Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya Kwanza—JINSI MUNGU ANAVYOWAPENDA WANADAMU

    Viumbe vya ulimwengu na jinsi Mungu alivyowafunulia wanadamu mambo ya jayo, vyote huonyesha upendo wake Mungu. Baba yetu aliye mbinguni ndiye asili ya uhai, hekima, na furaha. Vitazame viumbe vyote jinsi vilivyo vizuri na vya a jabu. Fikiri jinsi vifaavyo kwa mahitaji na furaha siyo ya wanadamu tu, bali ya viumbe vyote vilivyo hai. Jua na mvua, vinavyofurenisna na kuburudisha nchi, pamo ja na vilima, bahari na mabonoo, yote hutuonyesha upendo wa Muumba wetu. Mungu ndiye anayeviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao ya kila siku. Katika naneno nazuri ya Mtunga Zaburi twasoma haya,-HUK 1.1

    “Macho yao wote yakutazamia wewe;
    Nawe huwapa chakula chao majira yake.
    Hufunua mkono wako,
    Humshibisha kila hai uradhi.” Zaburi 145:15,16.
    HUK 1.2

    Mungu alimwumba mwanadamu katika hali ya furaha na utakatifu kamili; na wakati ilipotoka mkononi mwa Muumba, nchi ilikuwa nzuri kabisa; haikuwa na dalili ya uharibifu wala ya laana la Mungu. Taabu na mauti viliingia kwa ajili ya kuharibu amri za Mungu. Walakini upendo wake Mungu huonyeshwa hata kwa maumivu yaliyokuja kwa ajili ya dhambi. Imeandikwa kwamba Mungu aliilaani ardhi kwa ajili ya mwanadamu. Mwanzo 3:17. Miti yenye miiba na magugu - yaani shida na majaribu yanayompata mwanadamu katika uzima wake - yaliwekwa kuwa msaada wake, kuwa ni namna mo jawapo ya mafundisho yake yanayotakiwa katika mpango wa Mungu juu ya mwanadamu, apate kumtoa katika hali mbaya ya dhambi na kumrudisha katika hali njema jinsi alivyokuwa mara ya kwanza.HUK 1.3

    Ingawa dunia imeanguka katika hali mbaya kwa ajili ya dhambi, lakini yote yaliyomo si huzuni na mashaka tupu. Viumbe vimekuwa kama mitume wa Mungu kutuletea maneno ya kututia faraja na kututuliza roho zetu. Kila mti wa miiba una maua yake; yaani, katika kila shida twaweza kupata baraka za Mungu.HUK 1.4

    “Mungu ni upendo” imeandikwa kila mahali. Ndege waimbao vizuri, kila aina ya maua na miti,yote hutushuhudia upendo na uangalifu wa Mungu, jinsi atakavyo kuwafurahisha watoto wake.HUK 1.5

    Neno la Mungu huonyesha tabia zake. Yeye mwenyewe ametangaza upendo na huruma vyake visivyo na kiasi. Musa alipoomba, “Nionyeshe basi utukufu wako,” Bwana alimjibu akanena, “Nitapitisha mimi wema wangu wote mbele yako.” Huu ndio utukufu wake. Bwana alipita mbele ya Musa, akatamka, “Bwana, Bwana Mungu, mwenye rehema na neema, si mpesi kwa hasira, na mwingi wa huruma na kweli; awawekeaye elfu huruma, mvenye kusamehe uovu, na kosa, na dhambi.” Kutoka 33:18,19; 34:6,7. Naye “mvumilivu, na mwenye wema mwingi,” “kwa sababu apendezwa na huruma huyu.” Yona 4:2; Mika 7:18.HUK 1.6

    Mungu amejifungia mioyo yetu kwake kwa namna nyingi zinazotuonyesha upendo wake; katika viumbe vya ulimwengu, na kwa upendano ulio wema wa wanadamu, Mungu ame jaribu kutuonyesha wema wake. Lakini hayo yote hayawezi kutudhihirishia barabara upendo wake jinsi ulivyo, kwa kuwa adui, yaani Shetani, amepofusha macho ya kiroho ya wanadamu ili wawe na hofu ya Mungu; nao humwona Mungu kama ni mkali asiye na huruma. Shetani aliwapoteza wanadamu ili wamdhanie Mungu kuwa ni mkali kabisa - kama jaji aliye na roho ngumu asiyeweza kumwachia mtu. Aliwatilia wanadamu fikara kama Muumba wetu huwachunguachungua watu ili apate kujua makosa yao na kuwalipa kisasi. Bwana Yesu alikuja hapa duniani na kuishi kati ya wanadamu kwa kusudi kuziondolea mbali fikara mbaya hizo, na kutuoryesLa upendo wa Mungu jinsi ulivyo.HUK 1.7

    Mwana wa Mungu alitoka mbinguni ili awaonyeshe wanadamu Baba aliye mbinguni. “Hakuna mtu allyemwona Mungu wakati wo wote; Mwana wa pekee aliye katika kifua aha Baba, huyu ndiye aliyefasiri habari yake.” “Wala hakuna mtu amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.” Yoh.l:18; Matt.11:27. Mmo ja wa wanafunzi wake alipomwambia,“Tuonyeshe Baba,” Yesu alimjibu,“Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukuni jua, Filipo ? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba ?” Yoh.l4:8,9.HUK 2.1

    Yesu alipoeleza namna ya kazi yake aliyokuja kuifanya hapa duniani, alisema hivi,-HUK 2.2

    “Roho ya Bwana ni juu yangu,
    Kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.
    Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo,
    Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa,
    na vipofu kupata kuona tena,
    Kuwaacha wa huru waliosetwa.” Luka 4:18.
    HUK 2.3

    Hiyo ndiyo kazi yake. “Naye akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani.” Mat.10:38. Katika matendo yake yote alionyesha upendo, rehema na huruma. Alikuwa katika hali ya kibinadamu ili apate kujua mahitaji ya wanadamu. Hakuna hata maskini kabisa aliyeogopa kumfikilia karibu. Watoto pia wakavutwa kwake.HUK 2.4

    Yesu hakuficha hata neno lo lote la kweli, lakini aliyasema yote katika moyo wa upendo. Alitumia busara sana na uangalifu na huruma katika maongezi yake na watu. Hakuwafanyia watu jeuri kamwe, hakusema maneno yo yote makali yasipohusu, hakuwahuzunisha watu kupita kiasi. Hakuulaumu udhaifu wa kibinadamu. Alisema kweli tupu, lakini alisema yote katika moyo wa upendo. Alichukia sana na hali ya unafiki, na kutokuamini, na uovu; lakini kila aliposema maneno ya lawama na mashtaka, aliyasema kwa masikitiko makubwa. Aliulilia Yerusalemi, mji alioupenda, ambao ulikataa kumpokea yeye aliye Njia Kweli, na Uzima. Walimkana yeye aliye Mwokozi, lakini hata hivyo ‘ akazidi kuwahurumia. Maisha yake yalikuwa ya kujinyima mwenywe na kuwafikiria wengine. Kila mtu alikuwa na thamani kubwa machoni pake. Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, hakumdharau mwanadamu ye yote; bali aliwaona wote kuwa ni wenye dhambi ambao alikuja kuwaokoa. HUK 2.5

    Hizo ndizo tabia zake Kristo kama zilivyofunuliwa katika maisha yake. Tena hizi ndizo tabia za Mungu mwenyewe pia. Yesu, Mwokozi aliye mwema, mwenye huruma, ndiye Mungu hasa aliyedhihirishwa katika mwili wa kibinadamu. 1 Tim.3:16.HUK 3.1

    Yesu aliishi, akateswa, akafa ili atukomboe. Akawa “mtu wa huzuni,” ili tuwe washirikia pamoja naye katika furaha ya milele. Naye Mwana Mpendwa wa Mungu, aliye jaa noema na kweli, Mungu alimwacha atoke katika mahali pa utukufu na kutika hapa duniani palipoharibika kwa ajili ya dhambi, penye giza la mauti na laana. Alimkubali atoke mahali anapopendwa na Babaye na kusifiwa na malaika, a je kuaibika, kudhiliwa, kuchukizwa, na kuuawe., “Adhabu ya amani yetu juu yako.” Isa.53:5. Mwangalie jinsi alivyo jangwani, katika bustani ya Gethsemane, tena juu ya msalaba, Mwona Mtakatifu wa Mungu akachukua mwenyewe uzito wa dhambi ya wanadamu. Yeye aliyekuwa na uno ja kwa Mungu, akaona mwenyewe moyoni mwake ubaya wa hali ya kutengane na Mungu, ndiyo hali ya wanadamu kwa ajili ya dhambi, kwa ajill ya matengano hayo akaona uchungu moyoni naye akalia, “Mungu Wungu, Mungu wangu, mbona umeniacha ?” Matt.27:46. Uzito wa dhambi, jinsi ulivyo mbaya kupita kiasi, na jinsi unavyoleta kutengana na Mungu - huu ndio uliouvunja moyo wa Mwana wa Mungu.HUK 3.2

    Lakini Yesu hakujitoa kuwa dhabihu kubwa hivi maksudi kumtilia Baba yake moyo wa kuwapenda wanadamu na kuwaokoa. Sivyo! “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hate akampeleka Mwana wake wa pekee, ili mtu aliye yote amwaminiye asepotee, bali apate uzima wa milele.” Yoh.3:16. Tangu zamani Baba yetu aliye mbinguni ametupenda, si kwa ajili ya mapatanisho aliyoyafanya Yesu, ila kwa kuwa Mungu mwenyewe alitupenda naye akamkubali Yesu afanye mapatanisho hayo. Kristo ndiye njia ambayo kwayo Mungu hutuonyesha upendo wake kwetu. “Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakor.5:19. Mungu alipata maumivu pamoja na Mwanawe. Huko Gethsemane, na kwa kufa kwake Kalwari, Mungu alijitoa kwa ajili ya wokovu wetu.HUK 3.3

    Yesu alisema, “Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu ili niutwae tena,” Yeh-10 17. Yaani, ni kama Yesu angesema hivi; “Baba yangu amewapendeni sana hata anazidi kunipenda mimi kwa sababu ya kujitoa maisha yangu kwa ajili yenu. Mimi. nikawa ninajitoa badala yenu tena kuwa kama dhamana yenu. na kwa jinsi nilivyoehukua makosa yenu na adhabu ambayo miliwapasiwa ninyi, kwa hayo Baba yangu huzidi kunipenda mimi; kwa sababu yu Dhabihu yangu, Mungu aweza kuwa mwenye haki tena kumhesabia haki yule amsadikiye Yesu.”HUK 3.4

    Hapana awezaye kutuokoa, ila Mwana wa Mungu tu; kwa kuwa yeye pekee aliyekuwa pamoja na Baba ndiye awezaye kumsifu na kueleza tabia zake. Yeye tu aliyeujua upendo wa Mungu ndiye awezaye kuudhihirisha upendo ule barabara. Hakuna njia nyingine ya kutuonyesha jinsi Mungu anavyowapenda wanadamu waliopotea, ila kwa njia hii mo ja tu, yaani ya Kristo alivyojitoa na kufa badala yao.HUK 3.5

    “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akampeleka Mwana wake wa pekee.” Yoh.3:15. Mungu alimtoa Mwanawe aishi kati ya wanadamu ili azichukue dhambi zao, apate kuadhibiwa badala yao, na kuwatolea maisha yake kama dhabihu; pia Mungu akamtoa awe katika hali moja na wanadamu ambao wamepotoa, na kushirikiana nao katika mambo ya maisha yao na ha ja zao zote. Yeye aliyekuwa mmo ja na Mungu ame jiunga na wanadamu kwa namna isiyoweza kuvunjwa. Yesu “haoni haya kuwaita ndugu zake;” (Waeb.2:ll); yeye ndiye Dhabihu yetu, Mwombeaji wetu mbele ya Mungu, Ndugu yetu aliye katika mfano wa kibinadamu na kushirikiana nao hao ambao ameku ja kuwaokoa - Yeye ndiye Mwana wa mwanadamu. Alifanya hayo yote ili awakomboe wanadamu katika dhambi na hali yake mbaya, naye mwanadamu apate kujua upendo wake Mungu na kushirikiana naye katika hali ya furaha na usafi.HUK 3.6

    Tukifahamu kima cha wokovu wetu, jinsi Mwana wa Mungu alivyokufa kwa ajili yetu, imetulazimu kutambua jinsi tunavyoweza kuwa watu walio bora katika Kristo. Mtume Yohana alipofahamu upendo wa Mungu jinsi ulivyo mkubwa mno, aliona hana budi kumcha Mungu na kumsujudu moyoni mwake. Upendo huo, jinsi ulivyo wa huruma na rehema, ni upendo mkubwa usioweza kusemeka; naye Yohana alisema, “Fahamuni, ni pendo la namna gani alilotupa Bwana, kuitwa wana wa Mungu.” 1 Yoh.3:l. Mungu amewaona wanadamu kuwa ni wenye themani kubwa wa namna gani; Kwa kuanguka katika kufanya dhambi, wanadamu wakawa chini ya mamlaka ya Shetani. Lakini kwa kumwamini Kristo na kutolewa kwake, wawoza kuwa wana wa Mungu. Kristo alikuwa katika hali ya kibinadamu ili apate kuwasaidia wanadamu. Nao wenye dhambi wakiwa wanashirikiana naye Kristo, watageuzwa hali yao, na kustahili kuitwa “wana wa Mungu.”HUK 4.1

    Upendo wa ajabu huo, hauwezi kulinganishwa na kitu cho chote! Wana wa Mfalme aliye mbinguni! Ahadi ya kupendwa sana! Jambo la maana sana lifaalo kufikiriwa! Upendo usio na kifani, jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu usiompenda! Fikara hiyo huutiisha moyo na kuutuliza ili ufungwe kwake Mungu na kufanye mapenzi yake. Na jinsi tunavyozidi kuzichungua tabia za Mungu, na kufahamu jinsi alivyotufanyia kwa kufa kwake Kristo msalabani, ndivyo tunavyozidi kuona kama Mungu ndiye mwenye rehema na huruma, na ndiye awezaye kuwasamaha wenye makosa, naye ni mwenye haki, naye huwapenda wanadamu kwa upendo mkubwa upitao kiasi cha upendo wa mama kwa watoto wake.HUK 4.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents