Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura 6—Kumwamini Mungu na Kukubaliwa Naye

    KWA jinsi dhamiri na roho yako vilivyohuishwa na Roho Mtakatifu, hivyo unazidi kufahamu ubaya wa dhambi, nguvu zake, na jinsi inavyoleta taabu; tena unazidi kuchukizwa nayo moyoni. Huona kwamba kwa ajili ya dhambi umepata kutengwa na Mungu, nawe umekuwa umefungwa na uovu. Huwezi kamwe kujisaidia mwenyewe. Nia yako si safi, tena moyo wako huwa najisi. Umefahamu kwamba maisha yako hujaa dhambi na mambo ya kujipendeza nafsi yako mwenyewe. Wataka sana kusamehewa makosa yako, ili upate kutakaswa na kuwekwa huru kutoka utumwa wa Shetani. Kupatana na Mungu, na kufanana naye, na kuwa salama moyoni,—waweza kufanya nini ili uwe katika hali hiyo?KY 52.1

    Hali hii haiwezi kununuliwa kwa fedha, pia haipatikani kwa ajili ya akili wala elimu; tena huwezi kutumaini kuwa katika hali hiyo kwa juhudi yako mwenyewe. Bali utaipata bure mkononi mwa Mungu kama karama yake, “pasipo fedha na pasipo thamani.” Isa. 55:1. Ni juu yako tu kuichukua. Mungu asema, “Dhambi zenu zikiwa kama bendera (nyekundu), zitakuwa nyeupe kama theluji; zikiwa nyekundu nyekundu mno, zitakuwa kama sufu.” Isa. 1:18. “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, roho mpya nitatia ndani yenu.” Ezek. 36:26.KY 52.2

    Basi, umeziungama dhambi zako na kuziweka mbali na moyo wako. Pia umeazimia kujitoa kuwa mtu wa Mungu. Sasa nenda kwake, na kumwomba ili akusafishe dhambi zako zote, akupe moyo mpya. Ndipo usadiki kwamba amefanya hivyo kwa kuwa ndivyo alivyoahidi. Yesu alipokuwa hapa duniani, alitoa fundisho lile, kwamba imetulazimu kusadiki ya kuwa tumepata upaji wa Mungu aliotuahidi, ndivyo utakavyokuwa wetu. Yesu aliwaponya watu maradhi yao walipouamini uwezo wake. Aliwasaidia katika mambo waliyoweza kuyaona na macho ya kimwili, ili wapate kumtumainia juu ya mambo wasiyoweza kuyaona, yaani, wapate kusadiki uwezo wake katika kuwasamehe dhambi zao. Hivyo ndivyo alivyosema dhahiri katika kumponya yule mgonjwa wa kupooza: “Ili mjue ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza), Ondoka, ujitwike kita- nda chako, ukaende nyumbani kwako.” Mattayo 9: 6. Mtume Yohana pia, aliposema juu ya miujiza ya Kristo, alisema hivi: “Hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Yoh. 20: 31.KY 53.1

    Hivyo tukisoma habari katika Biblia jinsi Yesu alivyoponya wagonjwa wa kimwili, twaweza kufundishwa na kufahamu namna ya kumsadiki kuwa kweli anaweza kuachilia na kuondoa dhambi. Tusome juu ya yule mgonjwa wa kupooza. Alikuwa hoi kwa ugonjwa tangu miaka thelathini na minane, asiweze kwenda kwa miguu. Walakini Yesu alimwambia, “Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende.” Yule mgonjwa angaliweza kusema: “Bwana, kama utaniponya, nitafanya usemavyo.” Lakini sivyo. Alikubali neno la Kristo, alisadiki kwamba amepona, akajitahidi mara moja; alifanya jinsi Kristo alivyomwamuru, ndipo Mungu akamtolea nguvu zake, naye mgonjwa akapona mara, akawa mtu mzima.KY 54.1

    Hivyo ndivyo ilivyo kwako mwenye dhambi. Huwezi kulipia ukosefu wako, huwezi kugeuza moyo wako na kujitakasa mwenyewe kuwa safi. Lakini Mungu ameahidi kwamba atakufanyia hivyo katika Kristo. Unakubali hivyo? Na kwa jinsi unavyoziungama dhambi zako, na kujitoa kwa Mungu na kuazimia kumtumikia, ndivyo Mungu atakavyotekeleza ahadi yake, nawe utaachiliwa dhambi na kutakaswa; na utakuwa mtu mzima jinsi yule mgonjwa wa kupooza alivyowezeshwa na Kristo kwenda kwa miguu mara aliposadiki kwamba amepona. Ikiwa unaamini kama yule, ndivyo utakavyopata kupona katika dhambi.KY 54.2

    Yesu asema, “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24. Lakini kuna masharti juu yetu ili ahadi hii itimizwe,—tuombe kama vile apendavyo Mungu. Tena ni mapenzi ya Mungu kutuondolea dhambi zetu na kututakasa, ili tuwe watoto wake na kuishi maisha yaliyo safi kwa uwezo wake Mungu. Kwa hivyo twaweza kumwomba Mungu mibaraka hii, na kuamini kwamba tumeipata, na kumshukuru Mungu kwa kuwa kweli tumeipata mibaraka yake. Ni jambo linalotuhusu, kwenda kwake Yesu na kutakaswa, na kuhesabiwa kuwa ni safi bila lawama, na pasipo kuaibishwa “Sasa, basi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya Roho. “Warumi 8:1.KY 55.1

    Toka sasa mwili wako si wako mwenyewe; umenunuliwa na bei kubwa. “Hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, . . . bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asiye na hila, na asiye na waa, ya Kristo, aliyejuliwa tangu zamani.” 1 Petro 1: 18-20. Kwa kumwamini Mungu tu, Roho Mtakatifu ameanzisha, uzima mpya moyoni mwako. Sasa umekuwa kama mtoto aliyezaliwa kwa kiroho kuwa katika watu wa nyumba ya Mungu, naye anakupenda namna ampendavyo Mwana wake.KY 55.2

    Sasa kama umejitoa kuwa wa Yesu, usirudi nyuma tena kutoka mkononi mwake. Kila siku heri useme, “Mimi ndimi wake Kristo; nimejitoa kwake;” tena umwombe Roho yake akulinde kwa neema yake. Ulipata kuwa mtoto wa Mungu kwa njia ya kujitoa kwake na kumwamini; hivyo ndivyo utakavyofanya kila siku ili uishi katika Kristo. “Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye.” Wakol. 2:6.KY 56.1

    Wengine hufikiri kwamba ni lazima kuwa na wakati wa kujaribiwa na kumdhihirishia Mungu ya kuwa wameongoka kabla ya kuweza kupata mibaraka yake. Lakini sivyo. Waweza kupata mbaraka wa Mungu mara. Lazima wawe na Roho ya Kristo mioyoni mwao, kuwasaidia udhaifu wao katika kushindana na maovu. Yesu apenda ili tumwendee jinsi tulivyo,—wenye dhambi, wadhaifu, wasioweza kujiokoa wenyewe. Hata kama tumefanya mabaya ya namna gani, tusiogope kufika kwake. Atatupokea kwa moyo wa upendo, naye anakubali kututakasa makosa na unajisi wo wote.KY 56.2

    Wengi huanguka katika neno hili; hawaamini kwamba Yesu anawasamehe wao wenye- we hasa. Hawakubali ya kuwa jinsi Mungu asemavyo, ndivyo ilivyo. Ni haki ya watu wote wanaoyatimiza masharti ya Mungu, kujua kwa hakika kwamba kuna masamaha kwa kila dhambi. Ahadi za Mungu ni kwa kila mkosaji mwenye kutubu. Hata mwenye kufanya dhambi iwayo yote, hakuna asiyeweza kupata nguvu, na usafi, na kuwa mwenye haki katika Kristo Yesu aliyekufa kwa ajili yetu. Huwaambia waishi, na wasife.KY 56.3

    Mungu hatutendei jinsi binadamu wanavyowatendea wenzao. Yu mwenye rehema, upendo, na huruma. Asema, “Aache mwovu njia yake, na mtu mbaya mawazo yake; akamrudie BWANA, naye atawarehemu; na kwa Mungu wetu, kwani mkarimu kuachilia.” “Nimefuta, kama wingu zito, makosa yako, na, kama wingu, dhambi zako.” Isa. 55:7; 44:22.KY 57.1

    “Kwani sikifurahii kifo chake afaye, anena Bwana Mungu: basi geukeni, mkaishi.” Ezek. 18:32. Shetani yu tayari kila mara kutudanganya ya kwamba ahadi za Mungu si kwa watu kama sisi. Lakini tusisikilize maneno yake, bali tuseme hivi moyoni: Yesu alikufa kwa ajili yangu, niwe na uzima. Anipenda mimi; ataka nisife. Baba yangu aliye mbinguni ni mwenye huruma; na ingawa nimemtendea vibaya, na ingawa nimepoteza mibaraka yake kwa siku zilizopita, kwa vile anavyonipenda nitaondoka na kwenda kwa Baba na kusema, “Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo; unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishi wako.” Mfano ule wa Mwana Mpotevu kuonyesha namna Mungu anavyowapokea wanaokuja kwake; “Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana.” Luka 15: 18-20.KY 57.2

    Na hata mfano huu umepungukiwa kuonyesha sawa namna ya upendo na huruma ya Baba aliye mbinguni, kwa kuwa huruma yake haina kifani. Mungu asema, “Kupenda nimekupenda mapenzi ya milele; kwa hiyo na wema nimekuvutia.” Yer. 31:3. Mwenye dhambi ingawa angali mbali na Baba yake, yule Babaanamhurumia moyoni mwake na kumtaka sana. Na kila mpotevu asikiaye moyoni mwake kwamba anataka kumrudia Mungu, ameona hivyo kwa kuwa Roho Mtakatifu anamvuta kwa Baba ampendaye sana.KY 58.1

    Kama umezijua ahadi njema za Mungu zilizoandikwa katika Biblia, wawezaje kuona mashaka moyoni? Wawezaje kudhani kwamba Mungu angemkataa mwenye kumfikilia na kutubu? Fikara kama hizi ziondolewe mbali kabisa! Katika kumdhania Baba yetu hivi, unajihatarisha moyo wako mwenyewe. Ni kweli kama Mungu huchukizwa na maovu, lakini humpenda mwanadamu mpotevu, hata akajitoa pamoja na Kristo, ili aliye yote amwaminiye apate kuokoka na kurithi urithi wa milele katika ufalme wake mtukufu. Angeweza kusema nini tena zaidi ya hayo aliyoyasema kwa kuonyesha jinsi anavyotupenda sisi? Asema, “Aweza mwanamke kusahau mtoto wake anyonyaye, asimrehemu mwana wa tumbo lake? hata waweza hawa kusahau, ila siwezi mimi kukusahau wewe.” Isa. 49:15.KY 58.2

    Inueni macho, ninyi mlio na mashaka na wenye kuogopa; Yesu ndiye Mwombezi wetu. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mwanawe Mpendwa, na kumwomba msaada wake ili isionekane kwamba kufa kwa Yesu kumekuwa bure kwako. Roho Mtakatifu anakuita hivi leo. Mtolee Yesu moyo wako mzima, ili upate mbaraka wake.KY 59.1

    Nawe ukisoma ahadi zake, kumbuka kwamba yote husemwa kwa upendo na huruma. “Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi kwa wingi wa neema yake.” Waef. 1:7. Ndiyo, usadiki tu ya kuwa Mungu ni msaidizi wako. Anataka kuwarudisha wanadamu katika hali yao ya kwanza, kwa jinsi alivyowaumba kwa mfano wa Mungu. Nawe ukimkaribia Mungu na kuziungama dhambi zako na kutubu, yeye pia atakukaribia kwa moyo wa rehema na masamaha.KY 59.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents