Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura 7—Dalili ya Kuwa Wanafunzi wa Kristo

    MTU akiwa ndani ya Kristo, ni kiumbe kipya; vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.” 2 Wakor. 5:17.KY 61.1

    Pengine mtu hawezi kutaja siku wala mahali hasa alipoongoka kuwa mfuasi wa Kristo; lakini kukosa kufanya hivyo si kama kusema kwamba yule hakuongoka kweli. Kristo alimwambia Nikodemo, “Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Yoh. 3:8. Upepo hauwezi kuonekana, lakini twasikia na kuona matendo yake; na vilevile Roho ya Mungu inajulikana kwa namna ya matendo yake mioyoni mwa wanadamu. Uwezo wake, usionekane na macho ya kibinadamu, huanzisha maisha mapya moyoni; humwumba mtu kuwa mpya kwa mfano wa Mungu. Ijapokuwa kazi ya Roho inatendeka kwa kimya, tena haionekani; matokeo yake yamekuwa waziwazi. Kama Roho Mtakatifu ametengeneza moyo kuwa mpya, jambo hilo litaonekana katika maisha yake aliyeongoka moyo. Ingawa sisi wenyewe hatuwezi kugeuza mioyo yetu, ama kuzifanyiza nia zetu kupatana na Mungu; tena haifai kabisa kujitegemea wenyewe kwa matendo yetu yaliyo mema; walakini, kwa namna ya maisha yetu, itajulikana kama tunayo neema ya Mungu mioyoni mwetu. Itaonekana kwamba tabia zetu, desturi zetu, mazoea yetu, na mambo yetu yote yamegeuka kuwa mbalimbali na yale ya zamani. Tabia na desturi za mtu fulani zinajulikana si kwa matendo mema au mabaya ya siku moja moja tu, ila kwa maelekezo ya matendo yake na maneno yake, na mazoea yake ya siku zote.KY 61.2

    Ni kweli ya kuwa kuna watu ambao mienendo yao ni myema machoni pa wenzao, bila kuongoka moyo kwa ajili ya Kristo. Kwa sababu ya kupenda kusifiwa na kuwa kama waongozi kati ya wengine, hivyo hujilinda ili waonekane kuwa ni wenye adabu. Kwa ajili ya kujistahi nafsi zao, huyaepuka matendo mabaya ya nje. Hata mwenye kuzoea kujifikiria nafsi yake mwenyewe na kujipendeza, pengine anafanya mema. Ikiwa ni hivyo, twawezaje kuyakinisha kama tumekuwa upande wa Kristo, au sivyo?KY 62.1

    Ni nani anayeutawala moyo? Fikara zetu ni juu ya nini? Tunazoea kuzungumza juu ya nani? Ni nani ambaye tunampenda zaidi na kumtumikia? Ikiwa tu watu wa Kristo, fikara zetu ni juu yake. Tunajitoa kwake pamoja na vyote tulivyo navyo. Twataka kufanana naye, kuwa na Roho yake mioyoni, kufanya mapenzi yake na kumpendeza kwa mambo yote.KY 62.2

    Wale wanaokuwa wapya katika Kristo Yesu, hao nao watazaa matunda ya Roho, yaani, “upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” Wagal. 5:22, 23. Hawatafuata tamaa zao za zamani, bali watamwamini Mwana wa Mungu na kufuata nyayo zake; tabia zake zitaonekana katika maisha yao, watatakaswa kuwa safi kama yeye alivyo mtakatifu. Mambo waliyochukizwa nayo zamani, sasa wanayapenda; na vile walivyopenda zamani, sasa huchukizwa navyo. Yule aliyefanya kiburi, sasa huwa mpole na mnyenyekevu. Mlevi huacha ulevi wake, mwasherati na mzinzi huachana na matendo yao ya zamani, na kuwa watu safi. Mkristo hafuati anasa na mvao na mambo ya kidunia. Hataki kufanana na watu wa dunia kwa “kujipamba kwa nje,” “ila mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu iliyo ya thamani kuu mbele ya Mungu.” 1 Petro 3:3, 4.KY 63.1

    Toba si ya kweli isipokuwa imeonekana dhahiri kwamba mtu huongoka moyo na kufanya yaliyo mema. Kama mtu anarudisha amana yake, na kutoa tena aliyoitwaa kwa unyang’anyi, kuziungama dhambi zake, kumpenda Mungu na wenziwe, yule aliye mwenye dhambi anaweza kutumaini kwamba “amepita toka mauti hata uzima.” Yoh. 5:24.KY 63.2

    Sisi wanadamu ambao tungali wabaya, tukimfikilia Kristo na kupata kusamehewa dhambi zetu, hali yetu inageuka kabisa. Upendo huonekana moyoni. Twapata furaha katika kufanya yaliyo wajibu wetu sisi Wakristo; twapenda kujinyima kwa ajili yake Kristo. Zamani tulikuwa gizani, na sasa tuko katika nuru yake aliye “Jua la haki.”KY 64.1

    Tabia za Kristo zitaonekana katika wafuasi wake. Yeye alijitoa kufanya mapenzi ya Mungu kwa kuwa alimpenda Mungu. Mungu ni upendo. Upendo wa kweli hutoka kwa Mungu; pia unapatikana katika moyo ule tu ambao Yesu huutawala. Haupatikani kamwe katika moyo usioongoka na kujitoa kuwa wa Mungu. “Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.” 1 Yoh. 4:19. Upendo wa Mungu ukiwa humo mioyoni mwetu, maisha yetu yatakuwa safi, hata wengine katika jirani zetu watavutwa moyo na kutaka kutengeneza maisha yao kuwa safi, hasa kwa ajili ya mfano mwema wao walio Wakristo wema.KY 64.2

    Kuna makosa mawili ambayo watu wa Mungu hawana budi kujihadhari nayo. La kwanza, kujitumainia matendo mema yao wenyewe ili wapatane na Mungu. Hakuna awezaye kujitakasa mwenyewe ila kwa njia ya kuamini neema na msaada wa Kristo.KY 64.3

    Kosa la pili litupasalo sisi kuwa na hadhari nalo ni kinyume cha lile la kwanza, ndilo kufikiri kwamba hatuna haja kuzishika sheria za Mungu; wengine hufikiri ya kuwa kama tumewekwa haki kwa neema ya Kristo tu, basi hakuna inayotakiwa juu yetu ili tupate wokovu katika Kristo. Lakini sivyo kabisa.KY 65.1

    Angalia ya kwamba kumtii Mungu siyo kwa matendo ya nje yanayoonekana tu, bali kwa mambo ya moyo na upendo. Kumpenda Mungu ni asili ya kumtii. Mwanadamu awapo na upendo moyoni na kuwa katika mfano wa Yule aliyemwumba, ndipo inapotimizwa ahadi ya Agano Jipya ya Mungu jinsi inavyoandikwa, “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika.” Waeb. 10:16. Na sheria ikiwamo moyoni, itakuwa inaongoza katika mambo yote ya maisha ya mwanadamu. Kumtii Mungu kwa sababu ya kumpenda, hiyo ndiyo dalili ya kweli kama mtu fulani ni mfuasi wake, Imeandikwa hivi katika Biblia, “Huku ndiko kumpenda Mungu, kuzishika amri zake.” “yeye asemaye, Nimemjua, naye hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake. 1 Yoh. 5:3;2:4, Hivyo twaona ya kwamba imetakiwa ili tumtii Mungu na kuzishika amri zake; lakini kwa kumwamini Kristo tu tutaweza kumtii kwa njia ya kweli.KY 65.2

    Hatuwezi kustahili wokovu kwa ajili ya utii wetu; wokovu ni thawabu ya Mungu iliyotolewa bure, nasi tunaipokea kwa kumwamini Mungu. Na kumtii Mungu hufuatana na kumwamini. “Mnajua ya kuwa yeye alidhihiri ili aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona, wala hakumtambua.” 1 Yoh. 3:5, 6. Hiyo ndiyo dalili ya kweli inayodhihirisha kama mwanadamu ni mfuasi wa Kristo. Kama tunakaa ndani ya Kristo, na upendo wa Mungu hukaa mioyoni mwetu, ndipo mawazo na matendo yetu yatakapopatana na mapenzi ya Mungu jinsi yanavyonenwa katika amri zake takatifu. “Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyaye haki yuna haki; kama yeye alivyo na haki.” 1 Yoh. 3:7. Namna ya haki inayotakiwa na Mungu imeelezwa kwa kipimo cha sheria yake, jinsi inavyonenwa katika zile amri kumi zilizotolewa na Mungu katika mlima wa Sinai.KY 66.1

    Kusema ya kuwa tunamwamini Kristo, na huku kusema kwamba hatuna haja kumtii Mungu kwa mambo ya amri zake, hiyo si kuamini kwa kweli, bali ni kama kufanya kiburi tu, maana “mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani.” Waef. 2:8. Lakini “imani isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake.” Yak. 2:17. Na Yesu, kabla ya kuja kwake duniani, alisema, “Kufanya mapensi yako, Ee Mungu wangu, ndio furaha yangu; na sheria yako imo ndani ya moyo wangu.” Zab. 40:8. Tena kabla ya kurudi kwake mbinguni alisema, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.” Yoh. 15:10. Tena katika Maandiko imeandikwa hivi: “Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake. . . Hivi twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda.” “Maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake.” 1 Yoh. 2:3-6; 1 Petro 2:21.KY 66.2

    Sharti la kupata uzima wa milele limekuwa moja tangu zamani,—jinsi lilivyokuwa katika bustani ya Aden kabla Adamu na Hawa hawajaanguka na kufanya dhambi,—ndilo hili, kumtii Mungu kwa ukamilifu katika mambo yote ya amri zake, kuwa na haki kamilifu katika Kristo. Sisi peke yetu hatuna haki kabisa, ila kwa Kristo tu. Yesu alikaa hapa duniani, akajaribiwa kama sisi. Akaishi maisha yaliyo makamilifu pasipo dhambi. Akafa kwa ajili yetu; akajitoa badala yetu; alikubali kuzichu- kua dhambi zetu ili sisi tupate kupewa haki kwake. Kama unajitoa kwake, ua kumkubali kuwa ni Mwokozi wako, ijapokuwa umekuwa mwenye dhambi kabisa, utahesabiwa kuwa mwenye haki katika Kristo. Sifa njema ya Kristo itahesabiwa kuwa ni yako, nawe utakuwa katika hali ya kukubaliwa na Mungu kana kwamba hukufanya dhambi kabisa.KY 67.1

    Zaidi ya hayo, Kristo huigeuza hali ya moyo jinsi ilivyo. Hukaa ndani ya moyo wako kwa njia ya kuamini. Nawe imekupasa kuendelea kumwamini Kristo na kumtolea nia yako siku zote ili upate kumshiriki Kristo daima; na kwa kadiri unavyoendelea kufanya hivyo, ndivyo atakavyotenda kazi ndani yako, ili kutaka kwako na kutenda kwako vipatane na kusudi lake jema. Ndipo utaweza kusema, ‘‘Uhai nilio nasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Wagal. 2:20. Ndivyo Kristo alivyowaambia wanafunzi wake: “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemaye ndani yenu.” Mattayo 10:20. Na kama Kristo atenda kazi ndani yako, utakuwa na nia sawa na nia iliyokuwamo ndani ya Kristo na kutenda matendo kama vile alivyotenda yeye—matendo yaliyo ya kaki, na kumtii Mungu.KY 68.1

    Basi, hatuna kitu chema ndani yetu cha kujisifu nacho. Hatuna sababu ya kujitukuza. Tumaini letu pekee ni katika haki ya Kristo: ya kwamba itahesabiwa kwetu kama ni yetu wenyewe: tena katika haki hiyo, ikitendeka ndani yetu kwa kazi ya Roho Mtakatifu.KY 68.2

    Tukisema juu ya imani, lazima tufahamu ya kwamba kuna tofauti kati ya kusadiki tu ya kuwa Mungu yu hai, na kumwamini kabisa katika moyo. Hata Shetani na malaika wabaya huamini ya kuwa Mungu yuko; huamini uwezo wake, na maneno yake jinsi yalivyo ya kweli: ni mambo wasiyoweza kuyakana. Biblia inasema, “Mashetani nao waamini na kutetemeka,” Yak. 2:19; lakini hiyo siyo imani ya kweli. Mwarninifu wa kweli hujitoa kabisa kuwa wa Mungu na kufanya mapenzi yake. Kwa imani ya kweli moyo unatengenezwa kuwa mpya kwa mfano wa Mungu. Moyo na nia ya mwili, iliyo katika hali ya zamani, haitii sheria ya Mungu wala haiwezi; bali yule aliyeongoka moyo, sasa hupata furaha katika amri zake, na kusema “Nimeipendaje sheria yako! Ndio fikara yangu mchana kuchwa.” Zab. 119:97. Na hivyo “wema uagizwao na torati unatimizwa ndani yetu,” tusioenenda “kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” Warumi 8:4,1.KY 69.1

    Kuna wengine ambao wamejua upendo wa Kristo na jinsi anavyowasamehe dhambi zao, nao wanataka sana kuwa watoto wa Mungu; walakini wanaona ya kwamba sifa yao si kamili, na maisha yao si sawa. Hao wamekaribia kuona shaka kama kweli mioyo yao imefanywa mipya na Roho Mtakatifu. Na wote wa namna hiyo nawaambia hivi: Msife moyo ninyi, wala kurudi nyuma. Mara kwa mara tutalazimishwa kumwendea Yesu tukihuzunika kwa ajili ya makosa yetu; lakini haifai kushushwa moyo. Ingawa tumeshindwa na adui, Mungu hatatuacha na kututupilia mbali. Sivyo; mtume Yohana aliandika, “Na ijapo mtu akatenda dhambi, tuna Mwombezi kwa Baba, Yesu Kaisto mwenye haki.” 1 Yoh. 2:1. Tena tusisahau maneno yake Kristo: “Baba mwenyewe awapenda ninyi.” Yoh. 16:27. Mungu anataka kukurudisha kwake mwenyewe, na kuona mfano wake ndani yako jinsi Yeye alivyo safi na mtakatifu. Endelea kuomba kwa moyo wa bidii zaidi; na kumwamini Mungu kabisa. Na kwa jinsi tunavyopungua kujitegemea uwezo wetu wenyewe, tuzidi kutegemea na kutumainia uwezo wa Mwokozi wetu na kumsifu.KY 69.2

    Na kwa vile unavyozidi kumkaribia Yesu, hivyo utazidi kujiona mwenyewe kuwa u mwenye makosa zaidi; kwa kuwa macho ya kiroho yatazidi kuwa safi ya kufahamu namna ya ukosefu na upungufu wako, kwa vile unavyomtazama Yesu na kujilinganisha naye jinsi alivyo mkamilifu.KY 70.1

    Mtu asiyefahamu hali yake jinsi alivyo mbaya na mwenye dhambi, yule hawezi kumpenda Yesu sana moyoni mwake; bali yule ambaye ameongoka moyo kwa neema ya Kristo, yeye atamheshimu Kristo kwaajili ya sifa yake njema. Lakini isipokuwa tumefahamu hali yetu katika dhambi, tunabainisha ya kwamba hatujaona bado uzuri na ubora wa Kristo.KY 70.2

    Kwa jinsi tunavyopungua kujiona tu bora wenyewe, ndivyo tutakavyozidi kumheshimu Mwokozi wetu kwa wema na utakatifu wake. Mtu anapofahamu udhaifu wake na kumtaka Kristo, Kristo naye atamsaidia na kumjulisha uwezo wake. Na kwa vile tunavyozidi kuona ubora na sifa ya Kristo, ndivyo tutakavyozidi kuwa katika mfano wake.KY 71.1

    Yesu kwetu ni Rafiki, hwambia haja pia;
    Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia;
    Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
    Kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.

    Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia?
    Haifai kufa moyo, dua atasikia.
    Hakuna mwingine M wema, wa kutuhurumia;
    Atujua tu dhaifu; maombi asikia.

    Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
    Uja podharauliwa, ujaporushwa pia.
    Watu wangekudharau, wapendao dunia,
    Hukwambata mikononi, dua atasikia.

    Bwana Yesu unitazame sasa,
    Unifanye niwe dhabihu hai;
    Najitoa kwako, moyo, na vyote
    Unioshe sasa niwe mweupe.
    KY 71.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents