Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya Tano—KUJITOA KUWA WA MUNGU

    Mungu ameahidi hivi: “Nanyi mtanitafuta, na kuona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” Yer.29:13.HUK 18.1

    Isipokuwa moyo mzima umetolewa kuwa wake Mungu, mtu hawezi kugeuzwa kuwa katika hali ya kufanana naye Mungu. Kwa hali yetu ya ubinadamu tumetengwa mbali na Mungu, Roho Mtakatifu ameeleza hali yetu kuwa ni hii: “wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zenu;” “kichwa chote kigonjwa, moyo wote umezimia;” “hamna uzima.” Waef.2:1 Isa.1:5,6. Mungu hutaka kutuponya na kutuweka huru. Kufanya hivyo ni kugeuza hali yetu kabisa, na kuifanya dhamiri yetu yote kuwa mpya; tena hayawezekani hayo ila sisi tukijitoa kabisa kuwa wake Mungu.HUK 18.2

    Kupigana kule ambako mtu hupigana na nafsi yake mwenywe, ni vita kubwa kuliko zote. Kujitoa hivyo na kujisalimisha mkononi mwa Mungu, hakuwezekani bila kushindana moyoni; lakini isipokuwa mtu anajitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu, hawezi kabisa kusafishwa moyo na kuwa katika hali ya utakatifu.HUK 18.3

    Mungu hawashurutishi watu wamtii, bila kwanza kuwaonyesha sababu na maana yake, ili tupime kwa akili zetu jinsi ilivyo na kuchagua sisi wenyewe namna ya kufanya. “Njooni, tufanyane huja, asema Bwana.” Isa.1:18. Mungu halazimishi watu. Anataka tumtii na kumcha kwa hiari yetu wenyewe, si kwa lazima. Anataka tujitoe kwake sisi wenyewe, ili kwa Roho yake afanye kusudi lake mioyoni mwetu. Inekuwa juu yetu sisi kuchagua kwa hiari yetu ili tuondolewe katika utumwa wa dhambi, na kuwekwa huru kuwa wana wa Mungu.HUK 18.4

    Na pia, tukijitoa kwa Mungu, hivyo imetupasa kuacha vyote vinavyotaka kututenga mbali na Mungu. Mwokozi asema, “Kila mmo ja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Luka 14:33. Hata jambo gani, liwalo lo lote, linalotuvuta macho toka kwa Mungu, lazima tuliache kabisa. Kupenda mali, kutaka fedha, ni kama minyororo inayofunga wengine kwa Shetani. Wengine hupenda sifa na heshina ya watu, na mambo na anasa ya dunia. Imekuwa ni lazima kuikatakata minyororo hiyo yote. Hatuwezi kumpenda Mungu kwa moyo nusu, na kwa nusu kuipenda dunia na mambo yake. Sisis si watoto wa Mungu ila tumekuwa wake kabisa. Kuna wengine wanaosema kwamba wanamtumikia Mungu, na huku hujitegemea nguvu yao wenyewe kwa kufuata sheria za Mungu na kujipatia sifa njema na wokovu. Hawawi wakiamshwa mioyoni na kufahamu upendo wake Kristo kama inavyopasa; bali hujaribu kufuata mambo ya kikristo wakidhani kwamba kwa njia hiyo wataweza kujipatia mahali mbinguni. Dini ya namna hiyo haifai kitu.HUK 18.5

    Inapokuwa Kristo anakaa moyoni, roho inajaa upendo wake, hupenda kuongea naye, huambatana naye; hivyo pia mtu anajisahau nafsi yake kabisa na natanani yako yote. Wale ambao hubidishwa moyoni kwa ajili ya upendo wa Kristo jinsi alivyojitoa kabisa kwa ajili yao, hawafikiri kumtii Mungu kwa kadiri tu kutosha kukubaliwa na Mungu; bali hutaka kufika kile kipeo cha Kristo kwa kufuata matakwa yake yote na Mwokozi wao.HUK 18.6

    Je, umeona kwamba kujitoa kwa Kristo ni kujinyima kupita kiasi Jiulize hivi, “Kristo amefanya nini kwa ajili yangu ?” Mwana wa Mungu alijitoa kabisa - maisha yake, kupendwa kwake, na kupata maumivu - apate kutukomboa. Na sisi je, wabaya wasiofaa kupendwa sana hivi, twawezaje kumkataza mioyoni mwetu ? Tangu mwanzo wa maisha yetu tumepata mibaraka yake. Tungewezaje kumwangalia Yule aliyeumizwa kwa ajili ya dhambi zetu, na huku kutokubali upendo wake na dhabihu yake ? Tukifikiri na kufahamu jinsi Yesu alivyojishusha kwa ajili yetu, sisi tungewezaje kunung unika kupata uzima kwa njia ya kushindana na kujinyima na kujishusha mioyo ?HUK 19.1

    Kosa la wengi wanaojisifu mioyoni mwao ni kusema hivi: “Mbona imenipasa kutubu na kujishusha moyo ili ni jue kwa yakini kwamba nimekubaliwa na Mungu ?” Mtazame Kristo. Yeye alikuwa mahali pasipo dhambi kabisa, tena zaidi ya hayo, alikuwa Mfalme wa mbinguni; lakini kwa ajili ya binadamu alihesabiwa kuwa ni mwenyo dhambi. Alihesabika “pamoja na wakosao: ila dhambi za wengi akazichukua yeye, akawaombea wakosao.” Isa.53:12.HUK 19.2

    Lakini sisi je, hata tuna jitoa kabisa kwa ajili ya Kristo, tume jitoa nini ? Moyo uliochafuka kwa dhambi, ili Yesu autengeneze na kuusafisha kwa damu yake, na kutuokoa kwa upendo wake kuu. Hata hivyo wanadamu huona kwamba ni vigumu kujitoa kwake kabisa. Kusema hivyo ni haya tupu.HUK 19.3

    Mungu hataki tuache kitu cho chote ambacho kingkuwa na faida kwetu. Katika mambo yote, Mungu anataka tu ili tuwe na hali njema. Wote ambao hawa jamchagua Kristo bado, laiti wangefahamu ya kwamba mambo ya dunia wanayoyataka hayafai kitu yakilinganishwa na vitu vizuri ambavyo Kristo anataka kuwapa. Yule afuataye njia iliyokatazwa na Mungu, hawezi kabisa kupata furaha ya kweli. Njia ya kufanya dhambi ni njia ya taabu na uharibifu.HUK 19.4

    Si vizuri kufikiri kwamba Mungu hupenda kuona watoto wake wakipata kuumizwa na kuona uchungu. Anataka ili watoto wake wapate furaha tu. Baba yetu aliye mbinguni anataka tuache kujaribu kujifurahisha na anasa za dunia, ambazo huleta maumivu na kulegea moyo kwa ajili ya kutopata raha na furaha jinsi inavyotazamiwa; na pia anasa zile zitatufungia mlango wa furaha wa mbinguni. Mwokozi hukubali watu jinsi walivyo, pamoja na mahitaji yao, upungufu wao, na udhaifu wao; tena pamoja na kuwasafisha moyo na kuwakomboa kwa damu yake, pia ataridhisha mioyo ya wote watakaomjia kwa mkata wa uzima. Matakwa yake ni haya; tufanye mambo hayo tu yatakayotuongoza katika njia ya kweli, ili tufikilie kipeo cha furaha kisichoweza kufikiliwa na wale wasiomtii Mungu. Na kama Kristo anakaa ndani, hivyo ndivyo moyo huwa na furaha ya kweli.HUK 19.5

    Wengi wanauliza hivi: “Nawezaje kujitoa kwake Mungu ?” Kweli umetaka kujitoa kwake, lakini umekuwa dhaifu katika dhamiri yako, una mashaka moyoni, umefungwa na mazoezi na matendo ya dhambi. Huwezi kutimiza ahadi na maazimio yako. Huwezi kutawala fikara zako, nia yako, wala mapenzi yako. Tena kama unafikiria hayo yote, unashuka moyo na kudhani kwamba hutakubaliwa na Mungu; lakini usikate tamaa. Jambo kubwa la kufahamu ni hili: Mungu ametupa sisi uwezo wa kuchagua kwa hiari zetu jinsi tutakavyofanya. Wewe mwenyewe huwezi kugeuza moyo wako; huwezi kwa nguvu zako kumpa Mungu upendo wa moyo wako; lakini waweza kuchagua kama unataka kumtii Mungu na kufanya mapenzi yake. Mpe nia yako na dhamiri yako ili apate kuitawala; ndipo Mungu ataweza kufanya kazi yake moyoni mwako, ili kutaka kwako na kutenda kwako kupatane na kusudi lake njema. Hivyo utajiweka chini ya mamlaka yake Kristo; upendo wako utavutwa kwake, utapatana naye Kristo katika fikara zako.HUK 20.1

    Kutaka mema na usafi ni vizuri; lakini kutaka tu haifai kitu. Wengi watapotea wakiwa wanatamani tu kuwa Wakristo, kwa kuwa wanakosa kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu katika dhamiri zao; huchelewa kuchagua kabisa kwamba watakuwa Wakristo sasa.HUK 20.2

    Ukitumia nia na dhamiri yako kwa njia ya kweli, hali ya maisha yako itageuka kabisa. Kama unajiweka chini ya mamlaka yake Kristo, unajiunga na uwezo wa kupita uwezo mwingine wo wote. Utakuwa na nguvu itokayo juu iwezayo kukuimarisha kabisa; tena kwa njia ya kujitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu kila siku, utajaliwa kuishi maisha mapya, maisha ya kumwamini Mungu daima.HUK 20.3

    Naendea msalaba, miye mnyonge na mpofu,
    Yapitayo naacha, nipone msalabani.

    Nakulilia sana: nalemewa na dhambi;
    Pole Yesu asema: “Nitazifuta zote.”

    Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
    Roho yangu na mwili viwe vyako milele.

    Kwa damu yake sasa nimegeuka roho,
    Nikaziacha tamaa, nimtafute Yesu tu.

    Nakutumaini tu Ewe Mwana wa Mungu;
    Nainamia kwako; niponye Mponya wangu.

    Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake,
    Kile chembo kamili; msifuni yeye Mponya.
    HUK 20.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents