Sura ya Tisa—KAZI NA MAISHA, JINSI VINAVYOHUSIANA
Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo
- Contents- YALJYOMO
- Sura ya Kwanza—JINSI MUNGU ANAVYOWAPENDA WANADAMU
- Sura ya Pili—JINSI MWENYE DHMABI ANAVYOMHITAJI KRISTO
- Sura ya Tatu—KUTUBU
- Sura ya Nne—KUUNGAMA DHAMBI
- Sura ya Tano—KUJITOA KUWA WA MUNGU
- Sura ya Sita—KUMWAMINI MUNGU NA KUKUBALIWA NAYE
- Sura ya Saba—DALILI YA KUWA WANAFUNZI WAKE KRISTO
- Sura ya Nane—KUKUA KATIKA KRISTO NA KUWA WATU WAKAMILIFU WAKE
- Sura ya Tisa—KAZI NA MAISHA, JINSI VINAVYOHUSIANA
- Sura ya Kumi—KUMJUA MUNGU
- Sura ya Kumi na Moja—KUOMBA NI FARADHI YETU
- Sura ya Kumi ya Mbili—YATUPASAYO KUFANYA TUNAPOKUWA NA MASHAKA MOYONI
- Sura ya Kumi na Tatu—KUFURAHTA MUNGU
Search Results
- Results
- Related
- Featured
- Weighted Relevancy
- Content Sequence
- Relevancy
- Earliest First
- Latest First
- Exact Match First, Root Words Second
- Exact word match
- Root word match
- EGW Collections
- All collections
- Lifetime Works (1845-1917)
- Compilations (1918-present)
- Adventist Pioneer Library
- My Bible
- Dictionary
- Reference
- Short
- Long
- Paragraph
No results.
EGW Extras
Directory
Sura ya Tisa—KAZI NA MAISHA, JINSI VINAVYOHUSIANA
Mungu ndiye asili ya uzima na mwanga na furaha kwa ulimwengu wote. Mibaraka inatoka kwake kwa viumbe vyake vyote. Na mahali po pote ukiwapo uzima wa Mungu mioyoni mwa wanadamu, itakuwa kama mi to ya maji ya uzima ulo, kuwatokea na kuwasaidia na kuwabariki wengine. Ilikuwa furaha ya Mwokozi wetu kuwainua na kuwakomboa wanadamu wapotevu. Kwa hiyo hakuyahesabu maisha yake kuwa ni kitu cha thamni kwake, lakini “kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu.” Waeb.12:2. Hivyo pia malaika hushugulika katika kazi ya kufurahisha wengine. Hiyo ndiyo furaha yao. Kazi ile ambayo wengine hudhani ni kazi ya namna ya kuwavunjia heshina na cheo, yaani kuwahudumia na kuwasaidia walio wa chini yao na wenye hali mbaya, ndiyo kazi wenayoifanya malaika wakaao mahali pasipo dhambi kabisa. Ile nia ya Kristo ya kutojipendeza nafsi yake, bali kufikiria na kusaidia wengine, ndiyo nia inayoenea kote mbinguni, tena ni asili ya furaha yao wa mbinguni. Hiyo ndiyo nia watakayokuwa nayo wafuasi wa Kristo, na namna ya kazi watakayoifanya.HUK 35.1
Upendo wa Kristo ukiwamo moyoni, hauwezi kufunikika, bali utatambulika kwao wote tunaokutana nao. Kumpenda Yesu kutabainishwa katika kutamani kutenda kama alivyotenda yeye, kwa kusaidia na kubariki walimwengu wengine. Tutakuwa na moyo wa upendo, na huruma, na kushiriki katika hali ya wemgine wote walio viumbe wa Baba yetu aliye mbinguni.HUK 35.2
Mwokozi alipokuwa hapa duniani, hakukaa raha mustarehe na kujipendeza mwenyewe; bali alifanya bidii kuwaokoa wanadamu wapotevu. Tangu kuzaliwa kwake mpaka kusulubiwa kwake Kalwari, alifuata njia ya kujinyima. Alisema ya kwamba Mwana wa Adamu hakuja “kuhudumiwa, bali kuhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.” Mattayo 20:28. Hilo ndilo kusudi kuu la maisha yake, kufanya mapenzi ya Mungu na kumaliza kazi yako. Hakufikiri kamwe juu ya kujipendeza nafsi yake mwenyewe.HUK 35.3
Vivyo hivyo wale wanaomshiriki Kristo watakuwa tayari kujinyima ili wengine wapate kujua jinsi Yesu alivyokufa kwa ajili yao, nao pia washirikiane naye. Hiyo ndiyo roho inayoonekana kwa yule anayeongoka kweli. Mara anapomjua Kristo, husikia moyoni kwamba ameshurutishwa kuwajulisha wengine kuwa Yesu ni rafiki mwema wake. Ikiwa tumesikia wema wa Bwana wetu, basi, tuwaonyeshe wenzetu, ili wao pia wavutwe kwake Yesu, na kumjua “Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuayo dhambi ya ulimwengu.”Yoh.1:29.HUK 35.4
Tukijitahidi hivyo kusaidia wengine tutabarikiwa sisi pia. Mungu alikusudia hivi alipotupa sisi sehemu ya kazi ya kuokoa watu. Kuwa watenda kazi pamoja na Mungu ni heshima iliyo kuu na furaha iliyo kubwa zaidi ya yote wanayoweza wanadamu kupewa na Mungu.HUK 35.5
Mungu angaliweza kuwapa malaika kazi ya kuwahubiria wanadamu Injili. Lakini kwa upendo wake alichagua sisi tuwe watenda kazi pamoja naye, pamoja na Kristo na malaika, ili tushiriki mibaraka, furaha, na kuchangamshwa roho kwa jinsi inavyopatikana katika hudumu hii. Tena kila tendo la kujinyima kwa kuwasaidia wengine, humzidiehia moyo wa ukarimu yule mwenye kujinyima, naye hszidi kuputana na kushirikiana na Mwokozi; “maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, ili ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” 2 Wakor.8:9. Tena kwa kadiri tunavyotimiza kusudi la Mungu juu yetu, ndivyo tutakavyopata furaha na baraka katika maisha yetu.HUK 36.1
Kama utafanya kazi kama Kristo alivyokusudia wafuasi wake wafanye, na kuwavuta Watu kwake, utaona haja ya kuzidi kumjua Mungu moyoni mwako, na kuzidisha maarifa katika mambo ya Mungu, nawe utaona “njaa na kiu ya haki.” Utaendelea kumwomba Mungu, tena kuamini kwako kutazidi kuthibitika. Kama unapata kujaribiwa utashurutishwa kusoma Neno la Mungu na kumwomba zaidi. Hivyo utazidi kumjua Kristo, na kupata neema yako na kuwa mwaminifu wake katika maisha yake; hasa utazidi kufanana na Kristo, tena utapata raha na furaha zaidi moyoni mwako.HUK 36.2
Wale wanaojaribu kuwa Wakristo na kupata mibaraka yake bila kumfanyia Kristo kazi yo yote, hufanana na watu wanaotaka kupata chakula na kukaa bure bila kufanya kazi. Mtu anayekataa kuvinyosha viungo vyake kwa kutenda kazi, atapotewa na nguvu ile aliyo hayo. Vivyo hivyo Mkristo anayekataa kuutumia uwezo ule aliopewa na Mungu, hukosa kukua na kuwa kama mtu mzima katika Kristo, hata na yeye pia atapotewa na uwezo wa kiroho aliokuwa nao zamani.HUK 36.3
Mungu ameweka kanisa la Kristo kuwa kama wakili wake kwa kuwaokoa watu. Kazi yake ni kueneza Injili duniani kote. Sharti hiyo imekuwa juu ya Wakristo wote. Kama tumejua upendo wa Kristo, basi tunawiwa deni na wote wasiomjua Kristo. Mungu ametupa sisi nuru, si kwa kujisaidia sisi wenyewe tu, ila pia umulikie wale wengine wasiomjua.HUK 36.4
Wafuasi wa Kristo wangaliamka na kufanya wajibu wao, kungalikuwako watu elfu wa kuhubiri Injili mahali palipo mhubiri mmoja tu sasa. Na hata wale wasioweza kuwa watenda kazi ya Mungu wenyewe, wangesaidia kazi kwa fedha zao na maombi yao. Tena kazi ya kueneza Injili na kuwajulisha watu kuwa Kristo ndiye Msokozi wao, ingeendelea na kufanywa kwa moyo wa bidii sana.HUK 36.5
Si lazima twende katika nchi ngeni za makafiri, kumfanyi. Kristo kazi, ikiwa wajibu wetu uko huko kwetu. Twaweza kumtumikia Kristo nyumbani mwetu, kanisani kwetu, kwa wenzetu, majirani zetu, hata na wale tunaokutana nao katika kazi yetu.HUK 36.6
Katika maisha yake hapa duniani, Yesu alipitisha miaka mingi katika kufanya kazi ya useramala pamoja na babake mjini Nazareti. Tona alimwamini Mungu katika kufanya kazi ile kama alivyokuwa alipowaponya wagonjwa na kutembea juu ya maji ya Galilaya. Hivyo na sisi pia, hata ikiwa tumehesabiwa kuwa ni watu duni na kufanya kazi iliyo chini, twaweza kutembea na Yesu na kumtumikia.HUK 36.7
Mtume Paulo asema, “Kila mtu...na akae katika hali hiyo hiyo aliyoitwa.” 1 Wakor.7:24. Mfanyi biashara anaweza kufanya kazi yake kwa namna awezavyo kumtukuza Mungu kwa ajili ya uaminifu wake. Ikiwa yu mfuasi wa kweli wa Kristo, dini yake itaonekana katika mambo yake yote, anye atawadhihirishia watu namna ya roho ya Kristo. Mwashi, au mfanyi kazi yo yote, inampasa kuwa mwenye bidii tena mwaminifu katika kazi yake, na hivyo atakuwa mjumbe mwaminifu wa Kristo. Kila mtu anayejiita kwa jina la Kristo inampasa kutenda kazi kwa namna iliyo sawa, ili wengine wapata kuyaona matendo yake mema, wakamtukuze Mungu aliye Muumba tena Mwokozi wetu.HUK 37.1
Wengi hujisingizia wasitumio akili zao katika kufanya kazi ya Kristo, kwa sababu wengine wana akili iliyo bora zaidi. Watu wengi hudhani kwamba wale tu wenye akili nyingi ndio ambao wametakiwa kujitoa na akili zao katika kumtumikia Mungu. Pia wengi hudhani kwamba ni baadhi tu ya watu, yaani wanaopondelewa zaidi na kuwa katika hali nzuri, ambao hupewa akili na talanta, na wengine wametengwa mbali, hao hao hawapati kuitwa kushiriki kazi ya Mungu na neena yake. Lakini haikuelezwa hivyo katika mfano uliotolewa na Kristo. Bwana wa nyumba alipowaita watumishi wake, alimpa kila mmoja kazi yake.HUK 37.2
Kwa moyo wa kupenda, twaweza kuifanya hata kazi iliyo chini kabisa na kuifanya “kama kwa Bwana,” Wakol.3:23, Upendo wa Mungu ukiwano moyoni, utaonekana katika maisha.HUK 37.3
Usingojee jambo lililo kuu wala kutumaini kupata akili nyingi kabla ya kumtumikia Mungu. Tona usifikiri juu ya wengine jinsi watakavyokudhania. Kama maisha yako na matendo yako ya sikuzote huushuhudia wema wako na uaminifu wako, na kuwasadikisha wengine kwamba unataka kuwatendea yaliyo mema, kazi yako haitapotea bure. Hata na wafuasi wa Yesu wanaohesabiwa kuwa ni watu duni, wanaweza kusaidia wengine na kuwaletea baraka. Kama wanaendelea kufanya kwa uaminifu kazi ile wanayopewa na Mungu, maisha yao hayatakuwa bure. Watazidi kufanana na Kristo mioyoni mwao; huwa wafanyi kazi pamoja na Mungu katika maisha ya sasa, na vivyo hivyo wanatayarishwa kumhudunia Mungu mbinguni na kupata furaha kuu katika uzima ujao.HUK 37.4
Karibu na Wewe, Mungu wangu; Karibu zaidi, Bwana wangu.
Siku zote niwe karibu na Wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Nikifufuliwa kaburini,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.HUK 37.5