Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wakati wa Taabu ya Yakobo

    Watakatifu waliondoka mijini na vijijini na kujikusanya pamoja katika makundi makundi, na kuishi katika sehemu pweke kabisa. Malaika waliwapatia chakula na maji, wakati ambapo waovu walikuwa wakiteseka kwa njaa na kiu. Watu wakuu wa dunia walishauriana pamoja, na Shetani na malaika zake walishughulika kuwazunguka. Nakala za andiko zilitawanywa katika sehemu mbali mbali za nchi, zikitoa agizo kuwa isipokuwa watakatifu wanaachana na imani yao thabiti, wanaachana na Sabato, na kuitunza siku ya kwanza ya juma, watu walikuwa huru kuwaua baada ya kupita muda fulani. Lakini katika saa hii ya kujaribiwa, watakatifu walikuwa ni wenye amani na watulivu, wakimtumaini Mungu na kutegemea ahadi yake kwamba njia ya kutokea ingetengenezwa kwa ajili yao.PLK 128.1

    Katika sehemu zingine, hata kabla ya wakati wa amri ile kuanza kutekelezwa, waovu waliwakimbilia watakatifu ili wawaue, lakini Yesu aliwaamuru malaika zake kuwalinda. Mungu angetukuzwa kwa kufanya agano na wale ambao walikuwa wameitunza sheria yake, mbele ya macho ya maadui zao waliowazunguka; na Yesu angetukuzwa kwa kuwahamisha waaminifu, waliokuwa wakimngoja, waliomtarajia kwa muda mrefu, bila kuonja mauti.PLK 128.2

    Watakatifu walikuwa wakiteseka kwa maumivu makali ya kiakili. Walionekana kwamba wamezingirwa na wakazi waovu wa dunia. Kila kitu kilionekana kuwa kinyume chao. Baadhi walianza kuhofu kuwa hatimaye Mungu alikuwa amewaacha wafe mikononi mwa waovu. Lakini iwapo macho yao yangefunguliwa, wangeliona kuwa walikuwa wamezungukwa na malaika wa Mungu. Likafuata kundi la watu waovu wenye hasira, na kisha wingi wa malaika waovu, wakiwaharakisha waovu kwenda kuwaua watakatifu. Lakini kabla hawajawakaribia watu wa Mungu, ni lazima kwanza waovu walipite lile jeshi lenye nguvu la malaika watakatifu. Hili halikuwezekana kabisa. Malaika wa Mungu walisababisha waovu kurudi nyuma na pia kusababisha wale malaika waovu waliokuwa wakiwachochea kurudi nyuma.PLK 128.3

    Kilio kwa Ajili ya Kuokolewa-Ulikuwa ni wakati wa maumivu ya kutisha na kuogofya kwa watakatifu. Mchana na usiku walimlilia Mungu kwa ajili ya kuokolewa. Kwa mwonekano wa nje, hakukuwa na uwezekano wa wao kuokoka. Waovu tayari walishaanza kushangilia wakiwadhihaki kwa kusema: “Mbona Mungu wenu hawaokoi kutoka mikononi mwetu? Kwa nini msiende juu na kuyaokoa maisha yenu?” Lakini watakatifu hawakuwasikiliza. Kama Yakobo, walikuwa wakishindana na Mungu (Mwanzo 32:22-32). Malaika walitamani kuwaokoa, lakini hawana budi kusubiri kitambo kidogo. Watu wa Mungu ni lazima wakinywee kikombe na kubatizwa kwa ubatizo wa jaribio kuu. Malaika walidumu katika ulinzi wao, wakiwa waaminifu kwa wajibu wao. Mungu asingeruhusu jina lake kudharauliwa miongoni mwa wapagani. Wakati ulikuwa umekaribia ambapo angeonesha uweza wake mkuu na kuwaokoa watakatifu kwa utukufu. Kwa ajili ya utukufu wa jina lake angemwokoa kila mmoja wa wale waliokuwa wamemngoja kwa subira na ambao majina yao yalikuwa yameandikwa kitabuni.PLK 129.1

    Ilikuwa sawa na uzoefu wa Nuhu mwaminifu. Wakati mvua iliponyesha na Gharika kuja, Nuhu na familia yake waliingia ndani ya safina, na Mungu aliwafungia ndani. Kwa uaminifu Nuhu alikuwa amewaonya wakazi wa ulimwengu uliokuwapo kabla ya Gharika, wakiwa wanamdhihaki na kumkej eli. Na kadiri maj i yalivy oshuka chini duniani, na mmoja baada ya mwingine alivyokuwa akizama, waliiona safina, waliyoidhihaki, ikiwa inaelea kwa usalama katika maji yale, na kumhifadhi Nuhu mwaminifu na familia yake. Wala hakuna mashaka kuwa mwisho wa wakati, watu wa Mungu ambao kwa uaminifu kabisa waliuonya ulimwengu juu ya ghadhabu yake inayokuja, wataokolewa Mungu asingeruhusu waovu wawaangamize wale waliokuwa wanasubiri kuhamishwa na ambao hawakuisujudia amri ya mnyama au kupokea alama yake. Iwapo waovu wangeliruhusiwa kuwaua watakatifu, Shetani na malaika zake waovu wote, na wale wote wanaomchukia Mungu, wangefurahishwa sana. Na lo! ungekuwa ushindi wa jinsi gani katika pambano la mwisho la kuhitimishia kwa ukuu wake wa kishetani kuweza kuwa na uwezo juu ya wale ambao kwa muda mrefu kiasi kile walimsubiri Yesu, ambaye walimpenda! Wale ambao wamedhihaki wazo la watakatifu kwenda juu watashuhudia utunzaji ambao Mungu anao juu ya watu wake na kuona ukombozi wao mtukufu.PLK 129.2

    Wakati watakatifu walipoondoka mijini na vijijini, walifuatiwa na waovu waliojaribu kuwaua. Lakini silaha zao zilizoinuliwa ili kuwaua watu wa Mungu zilivunjika na kuanguka chini zikiwa dhaifu kama vile majani makavu. Malaika wa Mungu waliwakinga watakatifu. Walipolia mchana na usiku kwa ajili ya wokovu, vilio vyao vilipanda juu kwa Bwana.PLK 130.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents