Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura ya 15—Mwanzo Mpya

  Ki sha n ikaona mbingu mpy a na nchi mpy a; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita.” Ufunuo 21:1. Moto ule unaowaangamiza waovu unaitakasa dunia. Kila alama ya laana inafagiliwa mbali. Hakuna kuzimu kunakowaka moto milele kutakakodumisha kumbukumbu ya matokeo ya kutisha ya dhambi mbele ya waliokombolewa. Kuna kumbukumbu moja tu itakayobakia: Daima Mkombozi wetu atabeba alama za kusulibiwa kwake. Juu ya kichwa chake kilichojeruhiwa, mikono na miguu yake, kuna alama pekee za kazi ya ukatili ambayo dhambi imeitenda.PLK 148.1

  “Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja.” Mika 4:8. Ufalme uliopotezwa kwa sababu ya dhambi, Kristo ameutwaa tena, na waliokombolewa wataumiliki pamoja naye. “Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29. Hofu ya kufanya urithi wa watakatifu kuonekana kuwa ni wa vitu halisi imewaongoza wengi kufanya za kiroho kweli zile hasa ambazo zilituongoza kuitazama nchi mpya kama maskani yetu. Kristo aliwahakikishia wanafunzi wake kuwa alikuwa anakwenda kuandaa mahali kwa ajili yao. Wale wanaokubali mafundisho ya neno la Mungu hawatakosa kabisa kujua kuhusu maskani yao ya mbinguni. Na bado mtume Paulo anatangaza kuwa, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” lWakorintho 2:9. Lugha ya wanadamu haitoshi kuelezea thawabu ya wenye haki. Itafahamika tu kwa wale ambao wataiona halisi. Hakuna akili yenye ukomo inayoweza kuuelewa utukufu wa Paradiso ya Mungu.PLK 148.2

  Katika Biblia urithi wa waliokombolewa unaitwa nchi. (Waebrania 11:14-16.) Pale Mchungaji mkuu anaongoza kondoo wake kwenye chemchemi za maji ya uzima. Mti wa uzima huzaa matunda yake kila mwezi, na majani ya mti huo ni kwa ajili ya huduma kwa mataifa. Kuna vijito vinavyotiririka daima, safi kama kioo, na kando yake miti yenye kutikisika inarusha vivuli vyake juu ya njia zilizotayarishwa kwa ajili ya waliokombolewa wa Bwana. Pale uwanda mpana unatanuka ili kutengeneza vilima vizuri, na milima ya Mungu huinua juu sana vilele vyao virefu. Juu ya uwanda ule wenye amani, kando ya vijito vile vilivyo hai, watu wa Mungu, ambao kwa muda mrefu sana wamekuwa wasafiri na wahamaji, watapata makao.PLK 149.1

  Yerusalemu Mpya-Pale kuna Yerusalemu mpya, “wenye utukufu wa Mungu.” mwangaza wake “ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri.” Ufunuo 21:11. Anasema Bwana, “Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu.” Isaya 65:19. “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.PLK 149.2

  Katika mji wa Mungu “hakutakuwa na usiku.” Hakuna atakayehitaji au kutamani pumziko. Hapatakuwapo na uchovu katika kutenda mapenzi ya Mungu na kutoa sifa kwa ajili ya jina lake. Siku zote tutahisi nguvu mpya kama za asubuhi, na daima tutakuwa mbali na ukomo wake. “Hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru.” Ufunuo 22:5. Nuru ya jua itazidiwa na mwangaza usioumiza macho, lakini ambao unazidi kwa mbali uangavu wa adhuhuri. Utukufu wa Mungu na wa Mwana-Kondoo unalijaza jiji takatifu kwa nuru isiyofifia. Waliokombolewa wanatembea katika utukufu usio na jua wa mchana ya milele.PLK 149.3

  “Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.” Ufunuo 21:22. Watu wa Mungu wamependelewa kufanya ushirika na Baba na Mwana. Sasa “tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo” 1 Wakorintho 13:12. Tunaona sura ya Mungu ikiakisiwa, kama kwa kioo, katika kazi za asili na katika kushughulika kwake na wanadamu, lakini wakati huo tutamwona uso kwa uso, bila kuwapo na utaji unaohafifisha katikati. Tutasimama katika uwapo wake na kuangalia utukufu wa uso wake.PLK 150.1

  Akili za hawa wasioweza kufa tena zitajifunza kwa furaha ya kudumu maajabu ya uweza wa kuumba, na siri za upendo unaookoa. Hakuna adui katili na mdanganyifu wa kutujaribu ili tumsahau Mungu. Kila uwezo wa kufanya tendo lo lote utakuzwa, kila uwezo wa kujifunza na kukumbuka utazidishwa. Kuongeza maarifa hakutachosha akili au kumaliza nguvu. Pale, kazi kubwa kabisa inaweza kufanywa, shauku ya kupata kitu bora kabisa inaweza kufikiwa, malengo ya juu kabisa yanaweza kufikiwa, na bado kutakuwapo na vimo vya kupanda, maajabu mapya ya kuonea shauku, kweli mpya za kuzielewa, na malengo mapya ya kutumia nguvu za akili na roho na mwili.PLK 150.2

  Na kadiri miaka ya umilele inavyosonga mbele, italeta mafunuo bora na yenye utukufu zaidi na zaidi kuhusu Mungu na Kristo. Kama vile maarifa yanavyokuwa ya kuongezeka hatua kwa hatua, ndivyo ambavyo upendo, kicho, na furaha vitaongezeka. Kadiri watu watakavyozidi kujifunza kuhusu Mungu, ndivyo watakavyozidi kutazama na kupendezwa na tabia yake. Kadiri Yesu anavyofungua kwao utajiri wa ukombozi na mafanikio ya kushangaza katika pambano kuu na Shetani, mioyo ya waliokombolewa inadunda kwa upendo mkuu zaidi, na wanavipiga vinubi vya dhahabu kwa nguvu zaidi; na elfu kumi mara elfu kumi na maelfu ya maelfu ya sauti zinaungana kuvumisha wimbo mkuu wa sifa.PLK 150.3

  “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13.PLK 151.1

  Dhambi na watenda dhambi hawapo tena. Ulimwengu wote wa Mungu ni safi, na pambano kuu limekoma milele.PLK 151.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents