Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 25—Sheria ya Mungu Isiyobadilika

    “Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake” (Ufunuo 11:19). Sanduku la agano la Mungu liko ndani ya patakatifu pa patakatifu, chumba cha pili cha hekalu. Katika huduma ya hema la duniani, ambalo lilitumika “kama mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni,” chumba hiki kilifunguliwa wakati wa Siku kuu ya Upatanisho kwa ajili ya utakaso wa hema. Kwa hiyo, tangazo kuwa hekalu la Mungu lilifunguliwa mbinguni na sanduku la agano Lake lilionekana huelekeza kwa ufunguaji wa patakatifu pa patakafiu pa hekalu la mbinguni mwaka 1844 wakati Kristo alipoingia pale kutekeleza kazi ya kukamilisha upatanisho. Wale ambao kwa imani walimfuata Kuhani wao Mkuu wa mbinguni wakati akiingia katika huduma Yake ya patakatifu pa patakatifu, waliliona sanduku la Agano Lake. Walipojifunza somo la hekalu takatifu walipata uelewa wa badiliko la Mwokozi la huduma, na waliona kuwa sasa alikuwa akihudumu mbele ya sanduku la Mungu, akitumia damu yake kusihi kwa ajili ya wenye dhambi.PKSw 331.1

    Sanduku katika hema la duniani lilikuwa na mbao mbili za mawe, ambazo juu yake ziliandikwa kanuni za sheria ya Mungu. Sanduku lilikuwa kasha tu la kuhifadhia mbao za sheria, na uwepo wa kanuni hizi za Kimungu ulilipatia sanduku lile thamani yake na utakatifu wake. Wakati hekalu la Mungu lilipofunguliwa mbinguni sanduku la agano Lake lilionekana. Ndani ya patakatifu pa patakatifu, katika hekalu la mbinguni, sheria ya Mungu imehifadhiwa katika hali ya utakatifu—sheria iliyotangazwa na Mungu Mwenyewe katikati ya radi za Sinai na kuandikwa kwa kidole Chake mwenyewe kwenye mbao za mawe.PKSw 331.2

    Sheria ya Mungu katika hekalu la mbinguni ndiyo nakala halisi ya sheria ya Mungu, ambayo kanuni zilizoandikwajuu ya mbao za mawe na kuandikwa na Musa katika Torati ilikuwa hati isiyokosea. Wale waliofikia uelewa wa jambo hili muhimu waliongozwa hivyo kuona tabia takatifu, isiyobadilika ya sheria ya Mungu. Waliona vizuri zaidi, kuliko hata kabla ya hapo, uzito wa maneno ya Mwokozi: “Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka” (Mathayo 5:18). Sheria ya Mungu, kwa kuwa ni ufunuo wa mapenzi Yake, maelezo ya tabia Yake, ni lazima idumu milele, “kama shahidi mwaminifu wa mbinguni.” Hakuna amri hata moja ambayo imefutwa; hakuna yodi wala nukta ambayo imebadilishwa. Mtunga zaburi ameandika: “Ee Bwana, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele.” “Maagizo yake yote ni amini, Yamethibitika milele na milele” (Zaburi 119:89; 111:7, 8).PKSw 331.3

    Katikati ya Amri Kumi kuna amri ya nne, kama ilivyotangazwa kwa mara ya kwanza: “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa” (Kutoka 20:8-11).PKSw 332.1

    Roho wa Mungu aligusa mioyo ya wale wanafunzi wa neno Lake. Ushawishi ulijengeka katika mioyo yao kuwa waliivunja kanuni hii bila kujua kwa kupuuza siku ya mapumziko ya Mwumbaji. Walianza kuchunguza sababu za kuitunza siku ya kwanza ya juma badala ya siku ambayo Mungu aliitakasa. Hawakuweza kupata ushahidi katika Maandiko kuwa amri ya nne ilitanguliwa, au kuwa Sabato ilibadilishwa; mbaraka uliotakasa siku ya saba haujaondolewa. Walikuwa wakitafuta kwa uaminifu kuyajua na kuyafanya mapenzi ya Mungu; sasa, walipojiona wenyewe kuwa wavunjaji wa sheria Yake, huzuni ilijaza mioyo yao, na walionesha utii wao kwa Mungu kwa kuitunza Sabato na kuitakasa.PKSw 332.2

    Juhudi nyingi na za dhati zilifanywa ili kupindua imani yao. Hakuna mtu ambaye angeshindwa kuona kuwa ikiwa hema ya duniani ilikuwa mfano au nakala ya hekalu la mbinguni, sheria iliyohifadhiwa katika sanduku la agano la hema ya duniani ilikuwa ni nakala ya sheria iliyoko katika sanduku la agano la mbinguni; na kuwa kukubali kwa imani ukweli kuhusu hema ya mbinguni kulijumuisha kutambua madai ya sheria ya Mungu na madai ya Sabato ya amri ya nne. Hapa ndipo kulikuwa na siri ya upinzani mkali na wa makusudi dhidi ya ufafanuzi wenye mwafaka wa Maandiko yaliyofunua huduma ya Kristo katika hekalu la mbinguni. Watu walitafuta kufunga mlango ambao Mungu alikuwa ameufungua, na kufungua mlango aliokuwa ameufunga. Lakini “Yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye,” alisema: “Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga” (Ufunuo 3:7, 8). Kristo alikuwa amefungua mlango, au huduma, ya patakatifu pa patakatifu, nuru ilikuwa inang'aa kutoka katika mlango ule uliofunguliwa wa hekalu la mbinguni, na amri ya nne ilioneshwa ikiwa imejuimushwa katika sheria ambayo imehifadhiwa mle; kile ambacho Mungu alikianzisha, hakuna mwanadamu angeweza kukipindua.PKSw 332.3

    Waliokuwa wameipokea nuru kuhusu upatanisho wa Kristo na uendelevu wa sheria ya Mungu waligundua kuwa haya mambo yalikuwa ukweli uliowasilishwa katika Ufunuo 14. Vipengele mbalimbali vya ujumbe wa sura hii huunda onyo lenye sehemu tatu (tazama Kiambatisho) linaloandaa wakazi wa dunia kwa ajili ya ujio wa pili wa Bwana. Tangazo,“Saa ya hukumu Yake imekuja,” huelekeza macho kwa kazi ya kufunga huduma ya Kristo kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Linatoa habari njema za ukweli ambao inapasa uhubiriwe mpaka maombezi ya Mwokozi yatakapokoma na Yeye kurudi duniani awachukue watu Wake na kuwapeleka Kwake Mwenyewe. Kazi ya hukumu iliyoanza mwaka 1844 inapasa iendelee hadi kesi za watu wote ziamriwe, za makundi yote mawili ya walio hai na ya waliokufa; kwa maana hiyo hukumu hiyo itaendelea mpaka kufungwa kwa rehema ya wanadamu. Ili watu waweze kujiandaa kusimama katika hukumu, ujumbe unawaamrisha “mcheni Mungu, na kumtukuza,” “na msujudieni Yeye aliyeziumba mbingu, na nchi, na bahari, na chemchemi za maji.” Matokeo ya kuukubali ujumbe huu yametajwa katika neno: “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ili kujiandaa kwa ajili ya hukumu, ni lazima watu waishike sheria ya Mungu. Sheria ile ndiyo itakuwa kipimo cha tabia katika hukumu. Mtume Paulo anasema: “Na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria....katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.” Na anasema kuwa “waitendao sheria watakaohesabiwa haki” (Warumi 2:12-16). Imani ni ya lazima ili kuitii sheria ya Mungu; kwa kuwa “pasipo imani haiwezekani kumpendeza.” Na “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi” (Waebrania 11:6; Warumi 14:23).PKSw 332.4

    Kwa njia ya malaika wa kwanza, watu wanaalikwa “kumcha Mungu na kumtukuza” na kumsujudia Yeye kama Mwumbaji wa mbingu na nchi. Ili kufanya jambo hili, inawapasa waitii sheria Yake. Alisema mwenye hekima: “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu” (Mhubiri 12:13). Bila utii kwa amri Zake hakuna ibada inayoweza kumpendeza Mungu. “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.” “Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo” (1 Yohana 5:3; Mithali 28:9).PKSw 333.1

    Wajibu wa kumwabudu Mungu umejengwa juu ya ukweli kuwa Yeye ni Mwumbaji na kuwa uwepo wa wenye uhai wengine wote unamtegemea Yeye. Na mahali popote, ndani ya Biblia, dai Lake la kuheshimiwa na kuabudiwa, juu ya miungu ya wapagani, linapowasilishwa, ushahidi unaotolewa kuunga mkono dai hilo ni uwezo Wake wa kuumba. “Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu” (Zaburi 96:5). “Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi.” “Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya: ... Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine” (Isaya 40:25, 26; 45:18). Mtunga zaburi anasema: “Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake.” “Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba” (Zaburi 100:3; 95:6). Na wenye uhai watakatifu wanaomwabudu Mungu mbinguni wanasema, kama sababu ya heshima yao kumstahili Mungu: “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote” (Ufunuo 4:11).PKSw 333.2

    Katika Ufunuo 14, watu wanaitwa kumwabudu Muumbaji; na unabii unatufunulia tabaka la watu ambalo, kama matokeo ya ujumbe wenye sehemu tatu, wanazitunza amri kumi za Mungu. Moja ya amri hizi hutaja moja kwa moja kwa Mungu kama Muumbaji. Amri ya nne inasema: “Siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako: ... kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba: kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato, akaitakasa” (Kutoka 20:10, 11). Kuhusu Sabato, Bwana anasema, zaidi, kuwa ni “ishara, ... mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu” (Ezekieli 20:20). Na sababu inayotolewa ni kuwa: “Kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika (Kutoka 31:17).PKSw 334.1

    “Umuhimu wa Sabato kama kumbukumbu ya uumbaji ni kuwa inadumisha daima uwepo wa sababu ya kweli ya ibada kupaswa iwe kwa Mungu”—kwa sababu Yeye ni Muumbaji, na sisi ni viumbe Wake. “Sabato, hivyo basi, ndiyo msingi wa ibada ya Kimungu, kwani inafundisha ukweli huu mkuu kwa njia yenye mguso mkubwa sana, na hakuna agizo jingine lolote linaloweza kufanya hivyo. Msingi wa kweli wa ibada ya Kimungu sio tu wa siku ya saba peke yake, bali wa ibada zote, upo katika tofauti ya Muumbaji na viumbe Wake. Ukweli huu mkuu hauwezi kupitwa na wakati, na inapasa usisahaliuliwe kamwe.”—J. N. Andrews, History of the Sabbath, sura ya 27. Ilikuwa kwa kusudi la kudumisha ukweli huu daima mbele ya akili za watu Mungu aliiweka Sabato katika Bustani ya Edeni; na kwa kadiri ukweli kuwa Yeye ni Muumbaji wetu utavyoendelea kuwa sababu ya sisi kumwabudu Yeye, ndivyo Sabato itakavyoendelea kuwa ishara na kumbukumbu ya ukweli huo. Ikiwa Sabato ingetunzwa na watu wote ulimwenguni na kwa wakati wote, mawazo na upendo wa watu vingeelekezwa kwa Muumbaji na Yeye peke Yake angeheshimiwa na kuabudiwa, na kusingekuwepo mwabudu sanamu, au mkanamungu, au kafiri. Utunzaji wa Sabato ni ishara ya utii kwa Mungu wa kweli, “Yeye aliyeziumba mbingu, na nchi, na bahari, na chemchemi za maji Him” Maana yake ni kuwa ujumbe unaowaagiza watu kumwabudu Mungu na kuzishika amri Zake utawaita mahsusi watu kuishika amri ya nne.PKSw 334.2

    Kinyume na wale wanaozishika amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu, malaika wa tatu anataja tabaka jingine la watu, ambao dhidi ya makosa yao onyo kali na la kuogofya linatolewa: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu” (Ufunuo 14:9, 10). Tafsiri sahihi ya mifano iliyotumiwa ni ya muhimu ili kuelewa ujumbe huu. Ni nini kinawakilishwa na mnyama, sanamu, na chapa?PKSw 335.1

    Mlolongo wa unabii ambamo mifano hii inapatikana unaanzia katika Ufunuo 12, ukianza kwa kumtaja joka aliyetafuta kumwangamiza Kristo wakati wa kuzaliwa Kwake. Joka anaelezwa kuwa ni Shetani (Ufunuo 12:9); yeye ndiye aliyemfanya Herode achukue hatua ya kumwua Mwokozi. Lakini wakala mkuu wa Shetani katika kupigana vita dhidi ya Kristo na watu Wake katika karne za kwanza za zama za Ukristo alikuwa Himaya ya Kirumi, ambayo upagani ulikuwa dini kuu kuliko zingine zote. Hivyo basi, ingawa, joka, kimsingi, anamwakilisha Shetani, katika maana ya pili, joka ni mfano wa Rumi ya kipagani.PKSw 335.2

    Katika sura ya 13 (aya ya 1-10) anaelezwa mnyama mwingine, “mfano wa chui,” ambaye joka anampa “nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.” Mfano huu, kama Waprotestanti walio wengi wanavyoamini, huwakilisha upapa, ambao ulichukua uwezo na nguvu na mamlaka ambayo awali yalishikiliwa na Himaya ya Rumi ya zamani. Kuhusu mnyama aliye mfano wa chui yanatolewa maelezo haya: “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru.... Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.” Unabii huu, ambao unafanana sana na maelezo ya pembe ndogo ya Danieli 7, bila swali lo lote unazungumzia upapa.PKSw 335.3

    “Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” Na nabii anasema, “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” Na tena: “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga.” Miezi arobaini na mbili ni sawa na “wakati na nyakati na nusu wakati,” miaka mitatu na nusu, au siku 1260, za Danieli 7 - muda ambao upapa ulipewa mamlaka ya kuwatesa watu wa Mungu. Kipindi hiki, kama ilivyokwisha kuelezwa katika sura zilizotangulia, kilianza na utawala wa upapa, mwaka 538 B. K. na kiliisha mwaka 1798. Wakati huo papa alifanywa mateka na jeshi la Kifaransa, utawala wa upapa ulipata jeraha la mauti, na utabiri ulitimia, “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka.”PKSw 335.4

    Katika hatua hii mfano mwingine unatambulishwa. Anasema nabii:“Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo” (Aya ya 11). Kwa mwonekano wake na jinsi anavyotokea hudhihirisha kuwa taifa hili linalowakilishwa hapa ni tofauti na yale yaliowakilishwa na mifano iliyotangulia. Falme kuu zilizowahi kuitawala dunia ziliwasilishwa kwa nabii Danieli kama wanyama wa mawindo, wakiinuka wakati “pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa” (Danieli 7:2). Katika Ufunuo 17 malaika alieleza kuwa maji mengi huwakilisha “jamaa na makutano na mataifa na lugha” (Ufunuo 17:15). Pepo ni mfano wa mashindano. Pepo nne za mbinguni zinazoshindana juu ya bahari kuu huwakilisha mandhari za kutisha za mashindano na mapinduzi ambayo kwayo falme hupata mamlaka.PKSw 336.1

    Lakini mnyama mwenye pembe mbili mfano wa mwanakondoo alionekana “akipanda juu kutoka katika nchi.” Badala ya kushinda falme zingine ili kujipatia mamlaka, taifa linalowakilishwa hapa huinuka katika eneo ambalo awali halikuwa na wakazi na lilikua pole pole na kwa amani. Lisingeweza, hivyo basi, kuinuka miongoni mwa mataifa yenye msongamano na yanayopambana ya Ulimwengu wa Zamani—ile bahari yenye mawimbi ya “jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Inapasa litafutwe katika Bara la Magharibi.PKSw 336.2

    Ni taifa gani la Ulimwengu Mpya mwaka 1798 lilikuwa likipanda juu katika uwezo, likiwa na mwelekeo wa kuwa na nguvu na ukuu, na likivuta usikivu na macho ya ulimwengu? Matumizi ya mfano hayaruhusu uwepo wa swali lolote. Taifa moja, na moja pekee, hutimiza vipengele vya unabii huu; huelekeza bila shaka lolote kwa taifa la Marekani. Tena na tena wazo, karibu maneno yale yale, ya mwandishi mtakatifu yametumiwa na msemaji mahiri na mwanahistoria katika kuelezea kuinuka na kukua kwa taifa hili. Mnyama alionekana “akipanda kutoka katika nchi;” na, kwa mujibu wa watafsiri, neno lililotafsiriwa “akipanda juu” kwa tafsiri sisisi humaanisha “kukua au kuchipuka kama mmea.” Na, kama tulivyoona, taifa liliinuka katika eneo ambalo awali halikukaliwa na watu. Mwandishi mashuhuri, akielezea kuinuka kwa Marekani, anazungumzia juu ya “siri yake ya kupanda juu kutoka mahali pasipo na watu,” na anasema: “Kama mbegu iliyo kimya tulikua na kuwa himaya.”—G. A. Townsend, The New World Compared With the Old, ukurasa 462. Jarida moja la Ulaya mwaka 1850 lilizungumzia juu ya Marekani kama taifa la ajabu, ambalo lilikuwa “likiinuka,” na “katikati ya ukimya wa dunia kila siku likijiongezea nguvu na kiburi.”—The Dublin Nation. Edward Everett, katika hotuba fasaha juu ya waasisi Wasafiri wa taifa hili, alisema: “Si walitafuta mahali palipojificha, palipo huru kwa sababu ya kutokujulikana kwake, na salama kwa sababu ya umbali wake, mahali ambapo kanisa dogo la Leyden lingefurahia uhuru wa dhamiri? Tazama maeneo yenye nguvu ambayo, kwa ushindi wa amani, ... wamebeba bendera za msalaba!”— Speech delivered at Plymouth, Massachusetts, Dec. 22, 1824, ukurasa 11.PKSw 336.3

    “Naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo” Pembe za Mwana-Kondoo huashiria uchanga, kutokuwa na hatia, na upole, kuwakilisha kikamilifu tabia ya taifa la Marekani wakati lilipowasilishwa kwa nabii “likipanda juu” mwaka 1798. Miongoni mwa Wakristo wahamiaji wa kwanza waliokimbilia Marekani kutafuta hifadhi dhidi ya mateso ya mfalme na kukosa uvumilivu kwa makasisi walikuwemo wengi waliodhamiria kuunda serikali juu ya msingi mpana wa uhuru wa kiraia na kidini. Mawazo yao yalijumuishwa katika Azimio la Uhuru, linalobainisha ukweli mkuu kuwa “wanadamu wote wameumbwa sawa” na wamejaliwa haki isiyoachanika ya “uhai, uhuru, na utafutaji wa furaha” Na Katiba ya Marekani inawathibitishia watu uhakika wa kujitawala, ikielekeza kuwa wawakilishi waliochguliwa kwa kura nyingi watatunga na kusimamia sheria. Uhuru wa imani ya kidini ulitolewa, kila mtu akiruhusiwa kuabudu kulingana na misukumo ya dhamiri yake. Ujamhuri na Uprotestanti ukawa kanuni za msingi za taifa. Kanuni hizi ndiyo siri ya nguvu na mafanikio yake. Walioonewa na waliokandamizwa katika Ulimwengu wote wa Kikristo wamegeukia nchi hii kwa shauku na tumaini. Mamilioni wamekimbilia katika fukwe zake, na nchi ya Marekani imeinuka na kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu duniani.PKSw 337.1

    Lakini mnyama mwenye pembe za mwanakondoo “akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi” (Ufunuo 13:11-14).PKSw 337.2

    Pembe za mwakondoo na sauti ya joka za mfano huelekeza kwa ukinzani mkubwa kati ya mwonekano na matendo ya taifa lililowakilishwa. “Kunena” kwa taifa ni tendo la mamlaka zake za kibunge na kimahakama. Kwa tendo hilo taifa litabadilisha zile kanuni za uhuru na amani lililojiwekea kama msingi wa sera yake. Utabiri kuwa litanena “kama joka” na kutumia “uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake” hutabiri wazi wazi ujio wa roho ya kukosa uvumilivu na mateso iliyooneshwa na mataifa yaliyowakilishwa na joka na mnyama kama chui. Na kauli kuwa mnyama mwenye pembe mbili “aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza” huashiria kuwa mamlaka ya taifa hili itatumiwa kushinikiza utekelezaji wa jambo fulani la kiibada ambalo litakuwa tendo la kuheshimu upapa.PKSw 337.3

    Tendo hilo litakuwa kinyume kabisa cha kanuni za serikali hii, kinyume cha msingi wa taasisi zake huru, kinyume na viapo vikuu vya Azimio la Uhuru, na kinyume kabisa na Katiba. Waasisi wa taifa walitafuta kwa busara kutotumia mamlaka za kiserikali kuingilia mambo ya kanisa, pamoja na matokeo yake yasiyoepukika—kukosa uvumilivu na mateso. Katiba huelekeza kuwa “Bunge la Kongresi halitatunga sheria inayohusiana na uanzishaji wa dini, au kuzuia uhuru wa uanzishwaji wake,” na kuwa “dini haitakuwa kigezo kwa mtu ye yote kushika ofisi au wajibu wowote wenye dhamana ya umma chini ya taifa la Marekani.” Ni kwa ukiukwaji wa wazi wa tunu hizi za usalama wa uhuru wa taifa, ambapo inawezekana utekelezaji wa jambo fulani la kidini kushinikizwa na mamlaka za kiserikali. Lakini ubadilikaji wa tendo hilo hauwezi kuwa mkubwa zaidi kuliko ulivyowakilishwa katika mfano. Ni mnyama mwenye pembe mbili—kwa mwonekano yuko safi, mpole, na asiye na madhara—ambaye ananena kama joka.PKSw 337.4

    “Akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama.” Hapa kuna maelezo ya wazi kuhusu mfumo wa serikali ambayo mamlaka ya utungaji wa sheria uko katika mikono ya watu, ambao ni ushahidi madhubuti kabisa kuwa taifa la Marekani ndilo linalomaanishwa katika unabii huu.PKSw 338.1

    Lakini “sanamu ya mnyama” ni nini? Na sanamu inafanyikaje? Sanamu inafanywa na mnyama mwenye pembe mbili, na ni sanamu kwa ajili ya mnyama. Inaitwa pia sanamu ya mnyama. Halafu kujifunza ili kuelewa sanamu hii ikoje na inafanyikaje inatupasa kujifunza sifa za mnyama mwenyewe—upapa.PKSw 338.2

    Wakati kanisa la awali lilipochafuka kwa kuacha usahili wa injili na kupokea kaida na desturi za kipagani, kanisa lilipoteza Roho na nguvu ya Mungu; na ili kutawala dhamiri za watu, lilitafuta msaada wa mamlaka za kidunia. Matokeo yake yalikuwa kuzaliwa kwa mfumo wa upapa, mfumo wa kanisa uliotawala mamlaka ya kiserikali na uliotumia serikali kutekeleza maslahi ya kanisa, hususani kupambana na “uzushi.” Ili Marekani ifanye sanamu ya mnyama, inapasa mamlaka ya kidini itawale serikali ya kiraia kwa namna ambayo mamlaka ya kiserikali itatumiwa pia na kanisa kutimiza mtakwa ya kanisa.PKSw 338.3

    Wakati wowote kanisa lilipopata mamlaka ya kiserikali lilitumia mamlaka hayo kuwaadhibu wanaotofautiana na mafundisho yake. Makanisa ya Kiprotestanti yaliyofuata nyayo za Rumi kwa kuungana mamlaka za kidunia yamedhihirisha shauku ile ile ya kudhibiti uhuru wa dhamiri. Mfano wa jambo hili umeonekana katika mateso yaliyodumu kwa muda mrefu dhidi ya watu wanaotofautiana na Kanisa la Anglikana. Katika karne ya kumi na sita na ya kumi na saba, maelfu ya wachungaji wasiofungamana na upande wowote walilazimishwa kuyakimbia makanisa yao na wengi, wakiwa wachungaji na waumini, walilazimishwa kulipa faini, kufungwa, kuteswa, na kuuawa. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote;,;, mwana wa uharibifu;PKSw 338.4

    Ulikuwa uasi uliolifanya kanisa kutafuta msaada wa serikali ya kiraia, na jambo hili liliandaa njia ya uanzishwaji wa upapa—mnyama. Alisema Paulo: “Maana haiji usipokuja kwanza ule ukengeufu ... akafunuliwa yule mtu wa kuasi” (2 Wathesalonike 2:3). Kwa hiyo uasi ndani ya kanisa utaandaa njia kwa ajili ya sanamu ya mnyama.PKSw 339.1

    Biblia inaeleza kuwa kabla ya ujio wa Bwana kutakuwepo hali ya kurudi nyuma katika mambo ya dini kama ilivyokuwa katika karne za kwanza. “Katika siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake” (2 Timotheo 3:1-5). “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” (1 Timotheo 4:1). Shetani atafanya kazi “kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea.” Na wale wote ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,” wataachwa wapokee “nguvu ya upotevu, wauamini uongo” (2 Wathesalonike 2:9-11). Wakati hali hii ya uasi itakapofikiwa, matokeo yale yale yatafuata kama ilivyokuwa katika karne za kwanza.PKSw 339.2

    Tofauti nyingi za imani katika makanisa ya Kiprotestanti huchukuliwa na wengi kuwa uthibitisho wa hakika kuwa hakuna juhudi zinazoweza kufanyika kuleta muungano wa kulazimisha miongoni mwao. Lakini kumekuwepo kwa miaka mingi, katika makanisa ya imani ya Kiprotestanti, wazo lenye nguvu na linalokua linalounga mkono muungano uliojengwa juu ya vipengele vinavyofanana vya mafundisho. Ili kufanikisha muungano huo, mjadala juu ya mada ambazo hawakubaliani wote—hata kama ni muhimu kiasi gani kutokana na mtazamo wa Biblia—ni lazima kwa vyo vyote vile uepukwe.PKSw 339.3

    Charles Beecher, katika hubiri mwaka 1846, alitangaza kuwa huduma ya “madhehebu ya Waprotestanti wainjilisti siyo tu kuwa yameundwa kuanzia chini mpaka juu chini ya shinikizo kubwa la hofu ya kibinadamu, bali pia wanaishi, na wanatembea, na wanapumua katika hali ya mambo ambayo ni ya kifisadi sana, na kila saa wakitumia kila jambo dhaifu la asili zao kunyamazisha ukweli, na kupiga magoti kwa mamlaka ya uasi. Je, si ndivyo mambo yalivyokwenda kwa upande wa Rumi? Je, haturudii kuishi maisha ya Rumi kwa mara nyingine tena? Na tunaona nini huko mbele? Baraza Kuu jingine! Mkutano Mkuu wa ulimwengu! Muungano wa wainjilisti, na imani moja ya ulimwengu wote!”—Sermon on “The Bible a Sufficient Creed,” delivered at Fort Wayne, Indiana, Feb. 22, 1846. Wakati lengo hili litakapofikiwa, ndipo, katika bidii ya kupata umoja kamili, itakuwa hatua moja tu kufikia matumizi ya nguvu.PKSw 339.4

    Wakati makanisa makubwa ya Marekani, yakiungana juu ya vipengele vya mafundisho vinavyoshikiliwa na wote, yatakaposhawishi serikali kulazimisha utekelezaji wa amri zao na kutegemeza taasisi zao, ndipo Marekani ya Kiprotestanti itakuwa imefanya sanamu ya Kanisa la Rumi, na utoaji adhabu za kiraia kwa wanaotofautiana nao lazima utafuata mara moja.PKSw 340.1

    Mnyama mwenye pembe mbili “awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake” (Ufunuo 13:16, 17). Onyo la malaika wa tatu ni: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu.” “Mnyama” anayetajwa katika ujumbe huu, ambaye ibada yake inalazimishwa na mnyama mwenye pembe mbili, ni yule wa kwanza, mnyama anayefanana na chui wa Ufunuo 13—upapa. “Sanamu ya mnyama” huwakilisha mfumo wa Uprotestanti ulioasi utakaojengeka wakati makanisa ya Kiprotestanti yatakapotafuta msaada wa mamlaka ya kiserikali ili kusimamia utekelezaji wa mafundisho yake. “Alama ya mnyama” ndiyo bado haijafasiliwa.PKSw 340.2

    Baada ya onyo dhidi ya kumwabudu mnyama na sanamu yake unabii unaeleza: “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Kwa kuwa wale wanaozishika amri za Mungu wamewekwa kinyume na wale wanaomwabudu mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake, ina maana kuwa kushika amri ya Mungu, kwa upande mmoja, na kuivunja, kwa upande mwingine, kutakuwa ndiyo tofauti kati wanaomwabudu Mungu na wanaomwabudu mnyama.PKSw 340.3

    Sifa mahsusi ya mnyama, na hivyo sanamu yake, ni kuzivunja amri za Mungu. Danieli anasema, kuhusu pembe ndogo, upapa: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria” (Danieli 7:25). Na Paulo aliita mamlaka hiyo kuwa ni “mtu wa kuasi,” ambaye angejiinua juu ya Mungu. Unabii mmoja unaongezea kwa unabii mwingine. Ni kwa kubadili sheria ya Mungu pekee ndiko kungeufanya upapa kujiinua juu ya Mungu; na ye yote ambaye, huku akijua, angeshika amri iliyobadilishwa, angekuwa anatoa heshimu kuu kwa mamlaka iliyofanya badiliko hilo. Tendo hilo kwa sheria za kipapa lingekuwa alama ya utii kwa papa badala ya utii kwa Mungu.PKSw 340.4

    Upapa umejaribu kubadili sheria ya Mungu. Amri ya pili inayokataza kuabudu sanamu, imeondolewa katika sheria, na amri ya nne imebadilishwa ili kuidhinisha utunzaji wa siku ya kwanza badala ya siku ya saba ya juma kama Sabato. Lakini waumini wa upapa wanadai, kama sababu ya kuiondoa amri ya pili, kuwa ni kwa sababu siyo ya muhimu, kwa kuwa imejumuishwa katika ya kwanza, na kwamba wanaitoa sheria sawasawa kabisa na jinsi Mungu alivyopanga ieleweke. Hili haliwezi kuwa badiliko lililotabiriwa na nabii. Badiliko la kimataifa, la kukusudia limewasilishwa: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria” Badiliko katika amri ya nne linatimiza kikamilifu unabii huu. Hapa mamlaka pekee inayodaiwa ni ile ya kanisa. Hapa mamlaka ya upapa inajiweka juu ya Mungu.PKSw 341.1

    Wakati ambapo watu wanaomwabudu Mungu watatambulishwa hasa hasa kwa heshima yao kwa amri ya nne,—kwa kuwa hii ni ishara ya uwezo Wake wa uumbaji na ushuhuda wa madai Yake kwa ajili ya kicho na heshima kutoka kwa mwanadamu,—watu wanaomwabudu mnyama watatambulishwa kwa juhudi zao za kuchana-chana kumbukumbu ya Muumbaji, na kuinua agizo la Roma. Ilikuwa ni kwa ajili ya Jumapili ambapo upapa kwanza ulionesha madai ya kiburi chake (tazama Kiambatisho); na hitaji la kwanza la msaada wa mamlaka ya kiserikali ilikuwa ni kwa ajili ya kulazimisha utunzaji wa Jumapili kama “siku ya Bwana” Lakini Biblia huelekeza kuwa siku ya saba, na sio siku ya kwanza, kama siku ya Bwana. Kristo alisema: “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.” Amri ya nne inaeleza: “Siku ya saba ni Sabato ya Bwana.” Na kwa njia ya nabii Isaya Bwana anaiita: “siku ya utakatifu wangu” (Marko 2:28; Kutoka 20:10; Isaya 58:13).PKSw 341.2

    Dai linalotolewa mara nyingi kuwa Kristo alibadilisha Sabato linakanushwa na maneno Yake mwenyewe. Katika hubiri Lake juu ya Mlima alisema: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:17-19).PKSw 341.3

    Ni ukweli ambao kwa jumla unakubaliwa na Waprotestanti kuwa Maandiko hayatoi mamlaka kwa ajili ya kubadilisha Sabato. Jambo hili limeelezwa hasa hasa katika machapisho yanayotolewa na Muungano wa Shule ya Jumapili wa Amerika. Moja ya kazi hizi hukiri kuwa “kuna ukimya kamili katika Agano Jipya kuhusu amri ya moja kwa moja kuhusu Sabato (Jumapili), siku ya kwanza ya juma], au kanuni mahsusi kwa ajili ya utunzaji wake.”—George Elliott, The Abiding Sabbath, ukurasa 184.PKSw 341.4

    Mwingine anasema: “Mpaka wakati wa kifo cha Kristo, hakuna badiliko lo lote limewahi kufanywa katika siku;” na, “kwa kadiri kumbukumbu zinavyoonesha, wao [mitume]... hawakutoa amri mahsusi inayoagiza kutupilia mbali Sabato ya siku ya saba, na kuweka utunzaji wake siku ya kwanza ya juma.”—A. E. Waffle, The Lord’s Day, ukurasa 186-188.PKSw 342.1

    Wakatoliki wa Rumi wanakiri kuwa badiliko la Sabato lilifanywa na kanisa lao, na wanasema kuwa Waprotestanti kwa kushika Jumapili wanakiri mamlaka ya Kanisa la Rumi. Katika Catholic Catechism of Christian Religion, katika kujibu swali kuhusu siku inayopaswa kutunzwa ili kutii amri ya nne, kauli hii inatolewa: “Katika sheria ya zamani, Jumamosi ilikuwa siku iliyotakaswa; lakini kanisa, likielekezwa na Yesu na Kristo, na likiongozwa na Roho wa Mungu, limeweka Jumapili badala ya Jumamosi; kwa hiyo sasa tunaitakasa siku ya kwanza ya juma, na sio siku ya saba ya juma. Jumapili inamaanisha, na sasa ni, siku ya Bwana.”PKSw 342.2

    Kama ishara ya mamlaka ya Kanisa Katoliki, waandishi ambao ni waumini wa upapa wanatumia dondoo hii: “tendo lenyewe la kubadili Sabato kuwa Jumapili, ambalo Waprotestanti wanakubaliana nalo; ... kwa sababu kwa kuishika Jumapili, wanakiri mamlaka ya kanisa kuamuru siku kuu na kuwaamrisha chini ya dhambi.”— Henry Tuberville, An Abridgment of the Christian Doctrine, ukurasa 58. Badiliko hili la Sabato, hivyo basi, ni nini kama siyo ishara, au chapa, ya mamlaka ya Kanisa la Rumi—“chapa ya mnyama”?PKSw 342.3

    Kanisa la Rumi halijaacha dai lake la ukuu; na wakati ulimwengu na makanisa ya Kiprotestanti unapokubali sabato iliyoanzishwa na kanisa hilo, wanapoikataa Sabato ya Biblia, kimsingi wanakubaliana na dai hilo. Wanaweza kudai mamlaka ya mapokeo na ya Mababa kwa ajili ya badiliko; lakini kwa kufanya hivyo wanapuuza kanuni ya msingi inayowatenga na Roma—kuwa “Biblia, na Biblia pekee, ndiyo dini ya Waprotestanti.” Waumini wa mfumo wa upapa wanaweza kuona kuwa wanajidanganya wenyewe, wakifumba macho kwa kupenda wenyewe wasione ukweli katika suala hili. Harakati kwa ajili ya utunzaji wa lazima wa Jumapili inavyozidi kukubalika kwa kasi, wanafurahia, wakihisi kuwa hatimaye itauleta ulimwengu wote wa Waprotestanti chini ya bendera ya Roma.PKSw 342.4

    Waumini wa Uroma wanasema kuwa “utunzaji wa Jumapili wa Waprotestanti ni heshima kubwa wanayoitoa, kwa kujua au kutokujua, kwa mamlaka ya Kanisa [Katoliki].”—Mgr. Segur, Plain Talk About the Protestantism of Today, ukurasa 213. Ulazimishaji wa utunzaji wa Jumapili kwa upande wa makanisa ya Kiprotestanti ni ulazimishaji wa ibada ya upapa—ya mnyama. Wale ambao, kwa kutambua madai ya amri ya nne, huchagua kushika sabato ya uongo badala ya Sabato ya kweli, na kwa njia hiyo, wanaheshimu mamlaka ambayo kwa amri yake ilianzishwa. Lakini kwa tendo hilohilo la kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia mamlaka ya serikali ya kiraia, makanisa ya Kiprotestanti, kwa upande wao, yatafanya sanamu ya mnyama; kwa hiyo, ulazimishaji wa utunzaji wa Jumapili katika nchi ya Marekani utakuwa ulazimishaji wa ibada ya mnyama na sanamu yake.PKSw 342.5

    Lakini Wakristo wa vizazi vilivyopita waliishika Jumapili, wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo walitunza Sabato ya Biblia; na hata sasa wapo Wakristo wa kweli katika kila kanisa, ikiwa ni pamoja na jumuia ya Kanisa la Roma, ambao kwa moyo wa dhati huamini kuwa Jumapili ni Sabato iliyowekwa na Mungu. Mungu anaukubali udhati wa kusudi na uadilifu wao mbele Yake. Lakini wakati ushikaji wa Jumapili utakapolazimishwa kwa sheria, na ulimwengu kuangaziwa kuhusu madai ya Sabato ya kweli, ndipo ye yote atakayevunja amri ya Mungu, ili aitii amri ambayo haina mamlaka makubwa zaidi ya yale ya Roma, atakuwa kwa njia hiyo, ameheshimu upapa zaidi kuliko Mungu. Anatoa heshima kwa Roma na kwa mamlaka inayoshinikiza agizo lililoagizwa na Roma. Anaabudu mnyama na sanamu yake. Watu wanapotupilia mbali Sabato ambayo Mungu alitangaza kuwa ishara ya mamlaka Yake, na kuheshimu badala yake ile ambayo Rumi ilichagua kuwa alama ya ukuu wake, watakuwa kwa njia hiyo, wamepokea alama ya utii kwa—“chapa ya mnyama.” Na ni mpaka pale tu suala hili litakapokuwa limewekwa wazi, kama ilivyoelezwa, mbele ya watu, na watu kufikishwa mahali ambapo wataweza kuchagua kati ya amri za Mungu na amri za watu, ambapo wale watakaochagua kuendelea kutenda makosa watapokea “chapa ya mnyama.”PKSw 343.1

    Tishio la kuogofya lililowahi kutolewa kwa wanadamu walio na hali ya kufa linapatikana katika ujumbe wa malaika wa tatu. Hiyo lazima iwe dhambi ya kutisha inayosababisha ghadhabu ya Mungu isiyochanganywa na rehema. Watu hawapaswi kuachwa gizani kuhusiana na suala hili muhimu; onyo dhidi ya dhambi hii lipaswa kutolewa kwa ulimwengu kabla ya kujiliwa na hukumu za Mungu, ili kwamba wote wajue kwa nini hukumu hizi zitatolewa, na wawe na fursa ya kuziepuka. Unabii hutangaza kuwa malaika wa kwanza angetoa tangazo lake kwa “kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa.” Onyo la malaika wa tatu, ambalo ni sehemu ya ujumbe ule ule wenye sehemu tatu, nalo litatolewa kwa “kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa.” Limewakilishwa katika unabii kuwa litatangazwa kwa sauti kuu, likitolewa na malaika anayeruka katikati ya mbingu; na litavuta usikivu wa ulimwengu.PKSw 343.2

    Katika shindano hili ulimwengu wote wa Wakrito utagawanyika katika matabaka mawili makubwa—wale wanaozishika amri za Mungu na imani ya Yesu kwa upande mmoja, na wale wanaomwabudu mnayama na sanamu yake na kupokea chapa ya mnyama kwa upande wa pili. Hata kama kanisa na serikali wataunganisha nguvu zao kuwalazimisha “wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” (Ufunuo 13:16), wapokee “chapa ya mnyama,” hata hivyo watu wa Mungu hawataipokea. Nabii wa Patmo aliona “wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu” na wakiimba wimbo wa Musa na wa Mwana-Kondoo (Ufunuo 15:2, 3). PKSw 344.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents