Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 35—Uhuru wa Dhamiri Watishwa

    Ukatoliki sasa unaangaliwa na Waprotestanti kwa kukubalika zaidi kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Katika nchi ambazo Ukatoliki hauendelei kukua, na viongozi wa kipapa wanafanya kazi ya upatanisho ili kuwa na mvuto, kuna ongezeko la kutojali mafundisho yanayotenganisha makanisa yaliyofanya matengenezo na kanisa la kipapa; maoni yanaendelea kushika kasi kubwa, hata hivyo, hatutofautiani sana katika mambo ya msingi kama ambavyo imekuwa ikidhaniwa, na kuwa kupunguza kidogo upande wetu kutatuwezesha kuelewana vizuri zaidi na Rumi. Wakati ulikuwepo ambapo Waprotestanti walithamini sana uhuru wa dhamiri ambao ulikuwa umenunuliwa kwa gharama kubwa mno. Waliwafundisha watoto wao kuuchukia upapa na walishikilia kuwa kutafuta mapatano na Rumi ni kukosa utii kwa Mungu. Lakini ni mawazo tofauti sana yanayotolewa sasa!PKSw 430.1

    Watetezi wa upapa wanatangaza kuwa kanisa limeharibika, na ulimwengu wa Uprotestanti una mwelekeo wa kukubali kauli hiyo. Wengi wanasisitiza kuwa siyo haki kulihukumu kanisa leo kwa machukizo na upuuzi uliofanywa na kanisa katika karne za kutokujua na giza. Wanatoa udhuru kwa ukatili wake kama matokeo ya ujinga wa nyakati zile na wanadai kuwa ustaarabu wa kisasa umebadilisha mawazo yake.PKSw 430.2

    Je, watu hawa wamesahau madai ya kutokukosea yaliyotolewa kwa miaka mia nane na mamlaka hii yenye kiburi? Mbali kabisa na kuachwa, si dai hili lilithibitishwa katika karne ya kumi na tisa kwa mkazo mkubwa zaidi kuliko kabla ya hapo? Kama Rumi inavyodai kuwa “kanisa halijawahi kukosea; wala, kwa mujibu wa Maandiko, halitakosea kamwe” (John L. von Mosheim, Institutes of Ecclesiastical History, book 3, century II, part 2, chapter 2, section 9, note 17), linawezaje kuacha kanuni zilizoliongoza zama zilizopita?PKSw 430.3

    Kanisa la kipapa halitaacha kamwe dai lake la kutokukosea. Yote ambayo limewahi kufanya katika mateso yake kwa watu wanaokataa mafundisho yake ya imani yasiyobadilika linayachukulia kuwa sahihi kabisa; na je, halitarudia matendo yake yale yale, ikiwa fursa itajitokeza? Hebu ngoja vizuizi vinavyowekwa sasa na serikali zisizokuwa za kidini viondolewe na Rumi irudi katika mamlaka yake ya awali, ndipo kutakuwa na uamsho wa haraka wa ukatili na mateso yake.PKSw 430.4

    Mwandishi mashuhuri anasema hivyo kuhusiana na mtazamo wa kanisa la kipapa kuhusu uhuru wa dhamiri, na hatari zinazotishia hasa Marekani kutokana na mafanikio ya sera yake:“Kuna watu wengi wenye mwelekeo wa kutokuwa na hofu dhidi ya Ukatoliki wa Rumi ndani ya Marekani kuhusiana na ubaguzi wenye chuki na utoto. Watu kama hao hawaoni chochote katika tabia na mtazamo wa Urumi ambacho ni cha chuki dhidi ya taasisi zetu huru, au wala hawaoni cho chote kinachotisha katika ukuaji wake. Hebu, basi, kwanza tulinganishe baadhi ya kanuni za msingi za serikali ya Marekani na zile za Kanisa Katoliki.PKSw 430.5

    “Katiba ya Marekani inatoa uhakika wa uhuru wa dhamiri. Hakuna jambo jingine linapendwa au la msingi zaidi kuliko hili. Papa Pius IX, katika Barua yake aliyoituma kwa Maaskofu wote wa Kanisa la Rumi ya Agosti 15, 1854, alisema: ‘Mafundisho au matamko ya kipuuzi na yenye makosa yanayotetea uhuru wa dhamiri ni moja ya makosa makubwa sana—ni mdudu mharibifu, miongoni mwa wengine, anayepaswa kuogopwa kuliko wengine wote katika dola.’ Papa huyo huyo, katika Barua yake kwa Maaskofu wote ya Desemba 8, 1864, aliwakemea ‘wale wanaodai uhuru wa dhamiri na uhuru wa ibada ya kidini,’ pia ‘wote wanaodai kuwa kanisa halipaswi kutumia nguvu.’PKSw 431.1

    “Mwelekeo wa amani wa Roma katika nchi ya Marekani haumaanishi kuwa moyo wa Urumi umebadilika. Kanisa la Rumi limekuwa stahimilivu kwa kutokuwa na uwezo wa kufanya vinginevyo. Askofu O'Connor anasema: ‘Uhuru wa dini unavumiliwa tu mpaka pale ambapo kinyume chake kinaweza kutekelezwa bila kuhatarisha ulimwengu wa Kikatoliki.'... Askofu Mkuu wa St. Louis alisema wakati mmoja: ‘Uzushi na kukosa imani ni uhalifu; na katika nchi za Kikristo, kama ilivyo katika nchi za Italia na Hispania, kwa mfano, ambapo watu wote ni Wakatoliki, na mahali ambapo dini ya Kikatoliki ni sehemu muhimu ya sheria ya nchi, uzushi na kutoamini vinaadhibiwa kama uhalifu mwingine.'...PKSw 431.2

    “Kila kadinali, askofu mkuu, na askofu katika Kanisa Katoliki anakula kiapo cha utii kwa papa, ambapo maneno haya hutokea: ‘Uzushi, watenganishaji, na waasi kwa bwana wetu aliyetajwa (papa), au wafuasi wake waliokwisha kutajwa, nitawatesa na kuwapinga kwa nguvu zangu zote.'”—Josiah Strong, Our Country, ch. 5, pars. 2-4. [Tazama Kiambatanisho kwa ajili ya Rejea zilizosahihishwa.]PKSw 431.3

    Ni kweli kuwa kuna Wakristo halisi katika jumuia ya Kanisa Katoliki la Rumi. Maelfu katika kanisa wanamtukia Mungu kulingana na nuru yote waliyonayo. Hawaruhusiwi kusoma neno la Mungu, na kwa hiyo hawautambui ukweli. [Published in 1888 and 1911. Tazama Kiambatisho.] Hawajawahi kuona tofauti kati ya huduma hai inayotoka moyoni na mzunguko wa taratibu na kaida pekee. Mungu anawatazama watu hawa kwa huruma kama ya mama mzazi, watu walioelimishwa kama walivyo katika imani inayodanganya na isiyoridhisha. Atawezesha miale ya nuru kupenya giza nene linalowazunguka. Atawafunulia ukweli kama unavyopatikana ndani ya Yesu, na wengi watasimama pamoja na watu wa Mungu.PKSw 431.4

    Lakini Urumi kama mfumo haupatani zaidi na injili ya Kristo sasa kuliko wakati mwingine wo wote katika kipindi cha zamani cha historia ya Urumi. Makanisa ya Kiprotestanti yapo katika giza kubwa, isipokuwa kama wangeweza kutambua dalili za nyakati. Kanisa la Kirumi linaona mbali katika mipango yake na mbinu zake za kiutendaji. Linatumia kila njia kupanua mvuto wake na kuongeza nguvu yake katika maandalizi ya mgogoro mkali na wa makusudi wa kurudisha utawala wake juu ya dunia, kuanzisha upya mateso, na kutengua mambo yote ambayo Uprotestanti umeyafanya. Ukatoliki unaendelea kupata nguvu kila upande. Angalia ongezeko la idadi ya makanisa yake na nyumba zake za ibada katika nchi za Kiprotestanti. Angalia umaarufu wa vyuo na seminari zake katika Bara la Amerika, ambavyo hutumiwa sana na Waprotestanti. Angalia ukuaji wa kaida katika nchi ya Uingereza na jinsi watu wanavyorudi nyuma na kujiunga na Wakatoliki. Mambo haya yanapaswa kuamsha wasiwasi wa wote wanaothamini kanuni safi za injili.PKSw 432.1

    Waprotestanti wamechezea na kuulea upapa; wamelegeza misimamo yao na kuacha baadhi ya mafundisho yao kiasi ambacho hata wafuasi wa upapa wenyewe wanashangaa kuona na wanashindwa kuelewa. Watu wanafumba macho yao kiasi kwamba hawaoni tabia halisi ya Urumi na hatari zinazotokana na ukuu wake. Watu wanahitaji kuamshwa ili kupinga madai ya adui huyu adui wa hatari dhidi ya uhuru wa kiraia na kidini.PKSw 432.2

    Waprotestanti wengi wanadhani dini ya Kikatoki haivutii na ibada zake zimepoa, zikiwa na mizunguko isiyo na maana ya kaida. Hapa wanakosea. Wakati ambapo Urumi umejengwa juu ya udanganyifu, Urumi sio uigizaji usio na adabu na usio na weledi. Huduma ya kidini ya Kanisa la Kirumi ni kaida inayovutia sana. Maonesho yake ya kifahari na kaida zake za dhati hugusa sana hisia za watu na kunyamazisha sauti ya mantiki na dhamiri. Macho hufurahishwa. Makanisa makubwa ya kifahari, maandamano yanayovutia, mimbari za dhahabu, madhabahu za vito vya thamani, picha zenye ubora wa hali ya juu, na sanamu maridadi huvutia watu wote wanaopenda uzuri. Sikio nalo hutekwa. Muziki hauna mshindani. Noti tamu za ogani yenye sauti nzito, zikichanganywa na utamu wa sauti nyingi zinazopaa na kujaza kuba za juu na njia kati ya nguzo za makanisa yake makubwa, haziwezi kuacha kuifanya akili iwe na kicho na heshima.PKSw 432.3

    Huu utukufu, ufahari, na usherehekeaji wa nje ambao hudhihaki tu shauku ya roho iliyoumizwa na dhambi, ni ushahidi wa ufisadi wa ndani. Dini ya Kristo haihitaji vivutio vyote hivyo ili ikubalike. Katika nuru inayong'aa kutoka katika msalaba, Ukristo wa kweli huonekana kuwa safi na unaopendeza kiasi kwamba hakuna mapambo ya nje yanayoweza kuongezea thamani yake ya kweli. Ni uzuri wa utakatifu, roho ya upole na ukimya, ambavyo ni vya thamani mbele za Mungu.PKSw 432.4

    Uzuri wa mtindo sio lazima uwe kipimo cha fikra safi na za juu. Uelewa wa juu wa sanaa, uchaguzi bora wa mambo mazuri, mara nyingi huwa katika akili ambazo zimezama katika mambo ya kidunia na ya kimwili. Hutumiwa mara nyingi na Shetani kuwaongoza watu wasahau mambo muhimu ya kiroho, washindwe kuona mambo yajayo, maisha yanayokufa, kumwacha Msadizi asiyekuwa na kikomo, na kuishi kwa ajili ya dunia peke yake.PKSw 433.1

    Dini ya nje inavutia kwa moyo usioumbwa upya. Ufahari na usherehekeaji wa ibada ya Kikatoliki una nguvu ya kurubuni, kuteka, ambayo kwa njia yake watu wengi wanadanganyika; na wanakuja kuliona Kanisa la Rumi kama lango la mbinguni. Ni wale tu ambao wamesimika miguu yao kikamilifu juu ya msingi wa ukweli, na ambao mioyo yao imeumbwa upya kwa Roho wa Mungu, wana kinga dhidi ya mvuto wake. Maelfu ya watu ambao hawana ujuzi halisi wa Kristo wataongozwa kupokea maigizo ya utauwa ambayo hayana nguvu. Dini kama hiyo ndiyo watu walio wengi wanataka.PKSw 433.2

    Dai la Kanisa la kuwa na haki ya kusamehe humwongoza Mrumi kuhisi kuwa ana uhuru wa kutenda dhambi; na huduma ya maungamo, ambayo isipokuwepo msamaha hautolewi, huwa na mwelekeo wa kupalilia uovu. Yeyote anayepiga magoti mbele ya mwanadamu aliyeanguka dhambini, na kufunua katika maungamo mawazo yake ya siri na fikra zake za moyoni, anashusha hadhi ya utu wake na kudhalilisha kila silika bora ya nafsi yake. Kwa kufunua dhambi za maisha yake kwa padri,—mwanadamu mkosaji, mwenye dhambi na anayekufa, na mara nyingi ambaye amenajisiwa kwa pombe na tamaa,—kiwango chake cha tabia hushuka chini, na matokeo yake anachafuka. Mawazo yake kuhusu Mungu hushushwa chini hadi kumfananisha Mungu na mwanadamu aliyeanguka, kwa kuwa padri husimama kama mwakilishi wa Mungu. Ungamo hili linalodhalilisha la mwanadamu kwa mwanadamu ndiyo chemchemi ya siri ambapo mengi ya maovu hububujika ambayo yanachafua ulimwengu na kuundaa kwa ajili ya maangamizi yake ya mwisho. Hata hivyo, kwa mtu anayependa ubinafsi, inafurahisha zaidi, kuungama kwa mwanadamu mwenzake kuliko kufunua roho mbele ya Mungu. Ni jambo tamu kwa silika ya mwanadamu kufanya kitubio kuliko kuacha dhambi; ni rahisi zaidi kutesa mwili kwa magunia na upupu na minyororo inayoudhi kuliko kusulibisha tamaa za kimwili. Mzigo ni mzito ambao moyo usioongoka uko tayari kuubeba kuliko kuinama chini ya nira ya Kristo.PKSw 433.3

    Kuna mfanano wa wazi kati ya Kanisa la Rumi na Kanisa la Kiyahudi wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo. Wakati Wayahudi walipokanyaga kisirisiri kanuni ya sheria ya Mungu, walikuwa na juhudi kubwa katika kutunza miongozo yake, wakiibebesha matakwa na mapokeo yaliyofanya utii kuwa wa maumivu na mzigo. Kama Wayahudi alivyodai kuiheshimu sheria, ndivyo na Warumi nao wanavyodai kuuheshimu msalaba. Wanainua alama ya mateso ya Kristo, wakati katika maisha yao wanamkana Yeye ambaye msalaba unamwakilisha.PKSw 434.1

    Waumini wa upapa huweka misalaba kwenye makanisa yao, kwenye madhabahu zao, na kwenye mavazi yao. Kila mahali panaonekana alama ya msalaba. Kila mahali unaheshimiwa kwa nje na kuinuliwa. Lakini mafundisho ya Kristo yanazikwa chini ya wingi wa mapokeo yasiyokuwa na maana, tafsiri potofu, na matakwa magumu. Maneno ya Mwokozi kwa Wayahudi waliong'ang'ania imani yao kupita kiasi, yanawafaa kwa uzito mkubwa zaidi viongozi wa Kanisa Katoliki la Rumi: “Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao” (Mathayo 23:4). Roho adilifu huwekwa katika hofu ya kudumu zikiogopa ghadhabu ya Mungu aliyekosewa, wakati viongozi wa kanisa wakiishi maisha ya anasa na ya uridhishaji wa tamaa za kimwili.PKSw 434.2

    Ibada ya sanamu na mifupa, maombi kwa watakatifu waliokufa, na uinuaji wa papa ni mbinu za Shetani kuvuta akili za watu kutoka kwa Mungu na kutoka kwa Mwana Wake. Kutekeleza maangamizi yao, anajaribu kuvuta akili zao kutoka kwa Yule ambaye peke Yake wanaweza kupata wokovu. Atawaelekeza kwa kitu kingine cho chote kinachoweza kuwa badala ya Yeye aliyesema: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Ni juhudi ya kudumu ya Shetani kuwakilisha vibaya tabia ya Mungu, asili ya dhambi, na mambo halisi yaliyoko hatarini katika pambano kuu. Uongo wake hupunguza uwajibikaji kwa sheria ya Mungu na huwapatia watu leseni ya kutenda dhambi. Wakati huo huo anawafanya wawe na uelewa potofu wa Mungu ili wamtazame kwa hofu na chuki badala ya kumtazama kwa upendo. Ukatili ambao ni sehemu ya tabia yake mwenyewe anampakazia Mwumbaji; ukatili umewekwa katika mifumo ya dini na huoneshwa katika namna za ibada. Hivyo akili za watu zimepofushwa, na Shetani anawapata na kuwafanya mawakala wake dhidi ya Mungu. Kwa uwelewa potovu wa sifa za Mungu, mataifa ya kipagani waliongozwa kuamini kuwa kafara za wanadamu zilikuwa muhimu ili kupata fadhila ya Mungu; na ukatili wa kutisha ulitendeka chini ya mifumo mbalimbali ya ibada za sanamu.PKSw 434.3

    Kanisa Katoliki la Rumi, likiunganisha mifumo mbalimbali ya upagani na Ukristo, na, kama ulivyo upagani, likiwakilisha vibaya tabia ya Mungu, limekumbatia siyo ukatili na uasi kidogo. Katika siku za utawala wa Rumi kulikuwepo na zana za kutesea watu kuwalazimisha wayakubali mafundisho yake. Kulikuwepo nguzo ya kutesea kwa ajili ya wale ambao walikataa kuyakubali madai yake. Kulikuweko mauaji ya halaiki kwa kiwango ambacho hakitajulikana mpaka yatakapofunuliwa katika hukumu. Viongozi wakuu wa kanisa walijifunza, chini ya Shetani bwana wao, kugundua njia ambazo zingewezesha kuleta mateso makali sana kwa kadiri ambavyo ingewezekana na kumaliza kabisa maisha ya mhanga. Katika matukio mengi ya mchakato huo kuunguza mtu kwa moto kulirudiwa-rudiwa kwa kiwango ambacho mwanadamu asingeweza kustahimili, mpaka mtu alipoacha kupigania uhai wake, na mteswaji alishangilia kukaribisha kifo kama suluhisho tamu.PKSw 434.4

    Hayo ndiyo yalikuwa masahibu ya wapinzani wa Rumi. Kwa wafuasi wake, Kanisa lilikuwa na nidhamu ya viboko, njaa kali, maumivu makali ya mwili ya kila aina, yanayoumiza moyo. Ili kupata ukubali wa Mbingu, waliofanya toba walikiuka sheria ya Mungu kwa kukiuka sheria ya asili. Walifundishwa kutenganisha kile ambacho Mungu alikiumba kubariki ili kufurahisha maisha ya mwanadamu hapa duniani. Viwanja vya makanisa vina mamilioni ya wahanga waliotumia maisha yao bure wakijaribu kutiisha hisia zao za kimwili za asili, kudhibiti, kama jambo linalomchukiza Mungu, kila wazo na hisia ya huruma kwa viumbe wenzao.PKSw 435.1

    Ikiwa tunatamani kuelewa ukatili wa makusudi wa Shetani, uliodhihirishwa kwa mamia ya miaka, siyo miongoni mwa wale ambao hawajawahi kusikia habari za Mungu, bali katikati na katika ulimwengu wote wa Kikristo, tunapaswa kuangalia historia ya Urumi. Kwa njia ya mfumo huu mkubwa wa uongo mfalme wa uovu anafanikisha kusudi lake la kumkosea heshima Mungu na kuharibu maisha ya mwanadamu. Na kama tunavyoona jinsi anavyofanikiwa katika kujigeuza na kutekeleza kazi yake kupitia viongozi wa kanisa, tunaweza kuelewa vizuri zaidi kwa nini anaichukia sana Biblia. Ikiwa Kitabu hiki kitasomwa, rehema na upendo wa Mungu vitafunuliwa; itaonekana kuwa Mungu haweki hii mizigo mizito. Anachohitaji pekee ni moyo uliopondeka, roho ya unyenyekevu, ya utii.PKSw 435.2

    Kristo hatoi mfano wowote katika maisha Yake kwa wanaume na wanawake kujifungia katika nyumba za watawa ili kufaa kuishi mbinguni. Hakuwahi kufundisha kuwa upendo na huruma lazima vidhibitiwe. Moyo wa Mwokozi ulibubujika upendo. Kwa kadiri mwanadamu anapokaribia ukamilifu wa uadilifu, hisia zake zinazidi kuwa makini zaidi, uwezo wake wa kutambua dhambi unakuwa na makali zaidi, na huruma yake kwa wanaotesaka inakuwa ya kina zaidi. Papa anadai kuwa anasimama mahali pa Kristo; lakini kwa jinsi gani tabia yake inafanana na Mwokozi? Je, Mwokozi alijulikana wakati wowote kuwasweka watu gerezani au kwenye kichanja cha kukatia watu shingo kwa sababu walikataa kumpa heshima kama Mfalme wa mbinguni? Je, sauti yake ilisikika ikiwahukumu watu kifo wale ambao hawakumpokea? Alipopuuzwa na watu wa kijiji cha Samaria, mtume alijazwa na hasira, na aliuliza : “Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; kama Eliya naye alivyofanya?” Yesu alimtazama mtume Wake na kumkemea kwa roho yake ya ukali, akisema: “Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa” (Luka 9:54, 56). Ni tofauti kubwa kiasi gani kati ya roho iliyodhihirishwa na Kristo na ile ya yule anayedai kuchukua mahali pa Kristo.PKSw 435.3

    Kanisa la Roma sasa linawakilisha mwonekano wa haki kwa ulimwengu, likifunika kwa kuomba radhi kwa ajili ya kumbumbu zake za ukatili wa kutisha. Kanisa limejivika mwonekano unaofanana na wa Kristo; lakini bado halijabadilika. Kila kanuni ya upapa uliokuwepo katika zama zilizopita ipo pale pale leo. Mafundisho yaliyobuniwa katika zama za giza bado yanashikiliwa. Mtu yeyote asijidanganye. Upapa ambao Waprotestanti sasa wako tayari kuuheshimu ni ule ule uliotawala ulimwengu katika siku za Matengenezo, wakati watu wa Mungu waliposimama imara, wakihatarisha maisha yao, kuanika uovu wake. Kanisa bado lina kiburi kile kile na majivuno yale yale kama nyakati zile Kanisa lilipokuwa juu zaidi ya wafalme na wakuu wa nchi mbalimbali duniani, na lilipodai kuwa na mamlaka sawa na ya Mungu. Roho ya Kanisa haijaacha ukatili na ukandamizaji sasa kuliko wakati lilipovunja vunja uhuru wa binadamu na kuwaua watakatifu Wake Yeye Aliye Juu sana.PKSw 436.1

    Upapa ni ule ule ambao unabii ulitangaza kuwa ungekuwa, uasi wa siku za mwisho (2 Wathesalonike 2:3, 4). Ni sehemu ya sera yake kuwa na tabia inayoweza kulisaidia kutekeleza kusudi lake; lakini chini ya mwonekano unaobadilika wa kinyonga Kanisa linaficha sumu isiyobadilika ya nyoka. “Imani haipaswi kuchanganywa na wazushi, wala watu wanaohisiwa kuwa na uzushi” (Lenfant, volume 1, page 516), Kanisa linasema. Je, mamlaka hii, ambayo kumbukumbu yake ya miaka elfu moja imeandikwa katika damu ya watakatifu, ikubaliwe sasa kama sehemu ya kanisa la Kristo?PKSw 436.2

    Sio kweli kuwa hakuna sababu ya msingi inayowafanya watu wa nchi za Kiprotestanti kutoa madai kuwa Ukatoliki hauna tofauti kubwa sana na Uprotestanti kuliko ilivyokuwa katika nyakati za zamani. Kumekuwepo na badiliko; lakini badiliko haliko katika upapa. Ni kweli kuwa Ukatoliki unafanana na Uprotestanti uliopo sasa, kwa sababu Uprotestanti umeporomoka sana tangu siku za Wanamatengenezo.PKSw 436.3

    Makanisa ya Kiprotestanti yalipoanza kutafuta kukubaliwa na ulimwengu, ukarimu wa uongo ulifumba macho yao. Hawaoni isipokuwa kwamba ni vyema kuangalia wema katika uovu wote, na kama matokeo yasiyoepukika watafikia kuamini hatimaye kuwa uovu wote ni wema. Badala ya kusimama imara kutetea imani waliyoiamani iliyotolewa mara moja kwa watakatifu, kama walivyofanya zamani, sasa wanaomba msamaha kwa Rumi kwa maoni yao yasiyo na ukarimu kwa Kanisa la Kikatoliki, wakiomba msamaha kwa ubaguzi wao wenye chuki dhidi ya Kanisa Katoliki.PKSw 436.4

    Tabaka kubwa, hata la wale wanasiounga mkono Urumi, wanajua kidogo sana kuhusiana na hatari inayotokana na mamlaka yake na mvuto wake. Wengi wanasisitiza kuwa giza la kiakili na kimaadili lililokuwepo katika Zama za Giza liliruhusu usambazaji wa mafundisho yake, ushirikina wake, na ukandamizaji wake, na kwamba akili nyingi zaidi za nyakati hizi za sasa, ueneaji wa jumla wa maarifa, na ongezeko la uhuru katika masuala ya dini huweka mazingira magumu kwa ajili ya uamsho wa kukosa uvumilivu na ukatili. Wazo lenyewe kuwa hali kama hiyo inaweza kutokea katika zama hizi za maendeleo ya elimu, sayansi, na teknolojia linadhihakiwa. Ni kweli kuwa nuru kubwa ya kiakili, kimaadili, na kidini, inaangazia kizazi hiki. Katika kurasa zilizo wazi za Neno Takatifu la Mungu, nuru kutoka mbinguni imeangaza ulimwenguni. Lakini inapaswa ikumbukwe kuwa kwa kadiri nuru kubwa inavyotolewa, ndivyo giza linavyozidi kuwa kubwa zaidi kwa wale wanaoipotosha na kuikataa nuru.PKSw 437.1

    Usomaji wenye maombi wa Biblia ungewaonesha Waprotestanti tabia halisi ya upapa na ungewafanya wauchukie na kuukataa upapa; lakini wengi ni wenye hekima katika kiburi chao wenyewe kiasi kwamba hawahisi hitaji la kumtafuta Mungu kwa unyenyekevu ili waongozwe katika ukweli. Ingawa wanajivunia maarifa yao, hawajui cho chote kuhusu Maandiko wala uwezo wa Mungu. Wao wanacholilia ni kupata njia fulani ya kunyamazisha dhamiri zao, na kukidhi hitaji hilo wanatafuta mambo ambayo ni ya kiroho kidogo sana na ambayo yananyenyekesha kwa kiwango kidogo sana. Wanachotamani ni kupata mbinu ya kumsahau Mungu ambayo itaonekana kama mbinu ya kumkumbuka Mungu. Upapa umejipanga kukidhi mahitaji haya yote. Upapa umejiandaa kwa ajili ya matabaka yote mawili ya wanadamu, ukikumbatia karibu ulimwengu wote—wale ambao wanataka kuokolewa kwa matendo yao mema, na wale ambao wanapenda kuokolewa wakiwa na dhambi zao. Hapa ndipo palipo siri ya nguvu yake.PKSw 437.2

    Siku ya giza kubwa la kiakili imeonesha kuwa na msaada kwa mafanikio ya upapa. Itakuja kudhihirika pia kuwa siku ya nuru kubwa ya kiakili ni msaada mkubwa kwa mafanikio ya upapa. Katika zama zilizopita, watu walipokuwa hawana neno la Mungu na walipokuwa hawana maarifa ya ukweli, macho yao yalikuwa yamefumbwa, na maelfu walinaswa, kwa kutokuona wavu uliotandazwa kutega miguu yao. Katika kizazi hiki kuna wengi ambao macho yao yamepofushwa kwa mng'ao wa makisio ya kibinadamu, “sayansi kama inavyoitwa kwa uongo;” hawatambui wavu, na wanaingia katika wavu kirahisi kama vile hawana macho. Mungu alipanga kuwa uwezo wa kiakili wa mwandamu uchukuliwe kuwa zawadi kutoka Muumbaji wake na utumiwe katika huduma ya ukweli na haki; lakini kiburi na tamaa vinapopaliliwa, na wanadamu wanapoinua nadharia zao juu ya neno la Mungu, akili inaweza kufanya madhara makubwa zaidi kuliko ujinga. Hivyo basi, sayansi ya uongo ya siku hizi, ambayo inadhoofisha imani katika Biblia, italeta mafanikio makubwa katika maandalizi ya nje ya kuupokea upapa, na sherehe zake zinazofurahisha, kama kuzuia maarifa kulivyoleta mafanikio makubwa katika kufungua njia kwa ajili ya kujijengea umaarufu wake katika Zama za Giza.PKSw 437.3

    Katika harakati zinazoendelea sasa katika nchi ya Marekani za kupata kwa ajili ya taasisi na matumizi ya kanisa msaada wa serikali, Waprotestanti wanafuata nyayo za upapa. Hapana, zaidi, wanafungua mlango kwa ajili ya upapa kupata tena katika Amerika ya Kiprotestanti ukuu ambao upapa uliupoteza katika Ulimwengu wa Kale. Na kinachozipa harakati hizi uzito ni ukweli kuwa lengo kuu linalofikiriwa ni ulazimishaji wa utunzaji wa Jumapili—desturi iliyoanzishwa na Rumi, na ambayo Rumi inadai kuwa alama ya mamlaka yake. Ni roho ya upapa—roho ya kufuata desturi za kidunia, kuheshimu mapokeo ya kibinadamu juu zaidi kuliko amri za Mungu—ambayo inapenya na kuenea katika makanisa ya Kiprotestanti na kuwaongoza kufanya kazi ile ile ya kuiinua Jumapili kazi ambayo upapa ulikwisha kuifanya kabla yao.PKSw 438.1

    Ikiwa msomaji anataka kuwaelewa mawakala watakaotumiwa katika pambano ambalo linakuja karibuni, anachopaswa kufanya ni kufuatilia kumbukumbu za njia ambazo Rumi ilizitumia kwa makusudi hayo hayo katika zama zilizopita. Ikiwa anataka kujua jinsi wadau wa upapa na Waprotestanti kwa pamoja watakavyoshughulika na wale waliokataa mafundisho yao, hebu na aangalie roho ambayo Rumi ilionesha kwa Sabato na watetezi wa Sabato.PKSw 438.2

    Maagizo ya kifalme, mabaraza makuu, na sheria za kanisa zilizotekelezwa kwa mamlaka za kiserikali zilikuwa ngazi ambazo ziliwezesha siku kuu za kipagani kupata nafasi ya heshima katika ulimwengu wa Kikristo. Amri ya kwanza iliyolazimisha utunzaji wa Jumapili ilitungwa na Konstantino. (B.K. 321; tazama Kiambatisho maelezo kwa ajili ya ukurasa wa 53.) Amri hii iliwataka wakazi wa mijini kupumzika “siku ya heshima ya jua,” lakini amri iliwaruhusu watu wa vijijini kuendelea na shughuli zao za kilimo. Japokuwa ni sheria ya kipagani kabisa, ililazimishwa na mfalme baada ya kupokea Ukristo kwa jina.PKSw 438.3

    Wakati ambapo mamlaka ya kifalme haikuwa na uwezo wa kusimama badala ya mamlaka ya Mungu, Eusebius, askofu ambaye alitafuta kukubaliwa na wakuu wa kidunia, na ambaye alikuwa rafiki na kibaraka maalumu wa Konstantini, alitoa dai kuwa Kristo alikuwa amehamisha Sabato kutoka Jumamosi kwenda Jumapili. Hakuna aya ya Maandiko hata moja iliyotolewa kuthibitisha fundisho hilo jipya. Eusebius mwenyewe bila kujua anakiri uongo wake na anaelekeza kidole kwa waasisi halisi wa badiliko. “Mambo yote,” anasema, “kila jambo ambalo lilikuwa wajibu kulifanya siku ya Sabato, yote haya tumeyahamishia katika Siku ya Bwana.”—Robert Cox, Sabbath Laws and Sabbath Duties, ukurasa 538. Lakini hoja ya Jumapili, pamoja na kutokuwa na msingi wo wote, ilitumika kuwapa watu ujasiri katika kuikanyaga Sabato ya Bwana. Wote waliotamani kuheshimiwa na ulimwengu waliipokea siku kuu hiyo mpya ambayo ilitokea kuwa maarufu.PKSw 439.1

    Upapa ulipoimarika kikamilifu, kazi ya kuiinua Jumapili iliendelea. Kwa muda fulani watu walijihusisha na kazi ya kilimo ikiwa hawakwenda kanisani, na siku ya saba ilikuwa bado ikichukuliwa kama Sabato. Lakini pole pole badiliko lilitekelezwa. Watu waliokuwa katika ofisi takatifu walikatazwa kupitisha hukumu katika shauri lolote la madai siku ya Jumapili. Muda mfupi baadaye, watu wote, wa daraja lo lote, waliamriwa kuacha kazi za kawaida kwa tishio kuumizwa kwa faini kwa watu walio huru na kwa viboko kwa watumwa. Baadaye, iliamuriwa kuwa watu matajiri walipaswa kuadhibiwa kwa kupoteza nusu ya utajiri wao; na mwisho, kuwa ikiwa wangekuwa wakaidi baada ya hatua hizo kuchukuliwa, wangefanywa watumwa. Watu wa madaraja ya chini wangeadhibiwa kwa kufukuzwa kabisa kutoka nchini na wasionekane tena humo maisha yao yote.PKSw 439.2

    Miujiza pia ilihusishwa. Miongoni mwa maajabu mengine ilielezwa kuwa wakati mkulima ambaye alikuwa anataka kwenda kulima shamba lake siku ya Jumapili aliposafisha jembe lake la kukokotwa na ng'ombe kwa kipande cha chuma, kipande cha chuma kilinata kwenye kiganja cha mkono, na kwa miaka miwili kiling'ang'ania kiganjani mwake na alipaswa kukibeba kila mahali alikokwenda, “akiwa na maumivu makali na aibu.”— Francis West, Historical and Practical Discourse on the Lord’s Day, ukurasa wa 174.PKSw 439.3

    Baadaye papa alitoa maagizo kuwa kila paroko katika kila parokia alipaswa kuwaonya wavunjaji wa Jumapili na kuwataka waende kanisani na kutoa maombi yao, vinginevyo wangejiletea majanga wao wenyewe na majirani zao. Baraza la Kanisa Katoliki lilitoa hoja, tangu wakati huo ambayo imetumiwa mahali pengi, hata na Waprotestanti, kuwa kwa sababu watu walipigwa na radi wakifanya kazi Jumapili, ni lazima Jumapili iwe Sabato. “Inaonesha,” walisema maaskofu, “jinsi chuki ya Mungu ilivyokuwa kubwa kwa sababu ya kupuuza siku hii.” Wito ulitolewa baada ya hapo kuwa mapadri na wachungaji, wafalme na wakuu, na watu wote waaminifu “wajitahidi sana na wawe makini kuhakikisha kuwa siku hii inarudishiwa heshima yake, na, kwa ajili ya heshima ya Ukristo, ituzwe kwa kicho zaidi katika siku zinazokuja.”—Thomas Morer, Discourse in Six Dialogues on the Name, Notion, and Observation of the Lord’s Day, ukurasa 271.PKSw 439.4

    Amri za mabaraza zikionekana na zikithibitika kutotosha, mamlaka za serikali za kidunia ziliombwa zitoe amri ambazo zingechochea hofu katika mioyo ya watu na kuwalazimisha kuacha kufanya kazi siku ya Jumapili. Katika kikao cha sinodi kilichokaa Rumi, maamuzi yote yaliyopita yalithibitishwa kwa nguvu nyingi na uzito mkubwa zaidi. Ziliingizwa katika sheria za kanisa na utekelezaji na mamlaka za kiraia karibu katika ulimwengu wote wa Kikristo. (Tazama Heylyn, History of the Sabbath, pt. 2, ch. 5, sec. 7.)PKSw 440.1

    Bado kutokuwepo kwa mamlaka ya Maandiko kwa ajili ya utunzaji wa Jumapili kulileta sio usumbufu kidogo. Watu walihoji haki ya walimu wao kuweka pembeni tamko chanya la Yehova, “Siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako,” ili kuheshimu siku ya jua. Kufidia upungufu wa ushahidi wa Biblia, mbinu zingine zilikuwa za lazima. Mtetezi mwenye bidii wa Jumapili, ambaye karibu na mwisho wa karne ya kumi na mbili alitembelea makanisa ya Uingereza, alipingwa na mashahidi waaminifu kwa ajili ya ukweli; na kwa hiyo juhudi zake hazikuzaa matunda, hivyo, aliondoka nchini kwa muda na akatafutafuta njia ya kulazimisha mafundisho yake. Aliporudi, mapengo yalizibwa, na katika juhudi zake baada ya hapo alipata mafanikio makubwa. Alileta gombo alilodai kuwa lilitoka kwa Mungu Mwenyewe, ambalo lilikuwa na amri iliyokuwa ikihitajika kwa ajili ya utunzaji wa Jumapili, kwa ajili ya kuwatishia na kuwatia hofu wasiokuwa watiifu. Waraka huu wa thamani—ambao ulikuwa wa kughushi kama amri yenyewe iliyoungwa mkono nao —ulidaiwa kuwa ulianguka kutoka mbinguni na ulikutwa Yerusalemu, kwenye madhabahu ya Mtakatifu Simeoni, kwenye mlima wa Golgotha. Lakini, kwa kweli, waraka ule ulitoka katika ikulu ya papa, Roma. Udanganyifu na kughushi ili kuendeleza mamlaka na mafanikio ya kanisa katika zama zote vimeonekana kuwa halali mbele ya mamlaka za kipapa.PKSw 440.2

    Gombo lilikataza kufanya kazi kuanzia saa ya tisa, yaani saa tisa, Jumamosi mchana, mpaka mapambazuko siku ya Jumatatu; na mamlaka yake yalitangazwa kuwa yalithibitishwa kwa miujiza mingi. Ilitolewa taarifa kuwa watu waliofanya kazi zaidi ya saa zilizopangwa walipata ugonjwa wa kiharusi. Msagishaji wa mashine alipojaribu kusaga mahindi yake, aliona, badala ya unga, damu ikitiririka, na mashine ilitulia, licha ya bubujiko kubwa la maji. Mwanamke mmoja aliyeoka mikate katika oveni aliitoa ikiwa mibichi, ingawa oveni ilikuwa na joto kali. Mwingine aliyekuwa ameandaa madonge ya mikate, ilipofika saa tisa kabla ya kuioka, alidhamiria kuitunza mpaka Jumatatu alfajiri, ambapo aliikuta, siku iliyofuata, kuwa ilikuwa imeiva na ilikuwa imeokwa na nguvu ya Mungu. Mtu aliyeoka mikate baada ya saa tisa Jumamosi alikuta, alipoivunja asubuhi iliyofuata, kuwa damu ilivuja kutoka ndani ya mikate. Kwa maagizo hayo ya kipuuzi na kishirikina watetezi wa Jumapili walijaribu kuonesha utakatifu wa Jumapili. (Tazama Roger de Hoveden, Annals, vol. 2, ukurasa 526-530.)PKSw 440.3

    Katika nchi ya Scotland, kama ilivyokuwa katika nchi ya Uingereza, heshima kubwa zaidi kwa ajili ya Jumapili ilipatikana kwa kuiunganisha na sehemu ndogo ya Sabato ya zamani. Lakini wakati uliotakiwa kuheshimiwa kama wakati mtakatifu ulikuwa tofauti. Amri kutoka kwa mfalme wa Scotland ilitangaza kuwa “Jumamosi kuanzia saa sita mchana inatakiwa kuhesabiwa kuwa takatifu,” na kuwa hakuna mtu tangu wakati huo mpaka Jumatatu asubuhi, anapaswa kujihusisha na shughuli za kidunia.—Morer, ukurasa 290, 291.PKSw 441.1

    Lakini licha ya juhudi zote za kujenga utakatifu wa Jumapili, wadau wa upapa wenyewe walikiri hadharani mamlaka ya Kiungu ya Sabato na chimbuko la kibinadamu la Jumapili ambayo ilikuwa iwekwa badala ya Sabato ya Jumamosi. Katika karne ya kumi na sita baraza la papa lilitangaza wazi wazi: “Inawapasa Wakristo wote wakumbuke kuwa siku ya saba ilitakaswa na Mungu, na ilipokelewa na kutunzwa, sio tu na Wayahudi peke yao, bali pia na wengine wote wanaojifanya kumwabudu Mungu; japokuwa sisi Wakristo tulibadilisha Sabato yao na kuwa Siku ya Bwana.”— Ibid., ukurasa 281, 282. Waliochezea sheria ya Mungu hawakuwa wajinga kuhusiana na kazi waliyofanya. Kwa makusudi walijiweka juu ya Mungu.PKSw 441.2

    Kielelezo kizuri cha sera ya Rumi dhidi ya wale wanaopingana na Kanisa lao ni mateso ya muda mrefu na ya umwagaji damu ya Wawaldensia, ambao baadhi yao walikuwa watunza Sabato. Wengine waliteswa kwa jinsi hiyo hiyo kwa ajili ya uaminifu wao kwa amri ya nne. Historia ya makanisa ya Ethiopia na Abyssinia ni ya muhimu sana. Katikati ya utusitusi wa Zama za Giza, Wakristo wa Afrika ya Kati hawakuonwa na walisahauliwa na ulimwengu, na kwa karne nyingi walikuwa huru kutekeleza imani yao. Lakini hatimaye Rumi iligundua uwepo wao, na mfalme wa Abyssinia alihadaiwa kwa muda mfupi na kukiri kuwa papa alikuwa mwakilishi wa Kristo. Matukio mengine yalifuata. Amri ilitolewa iliyokataza utunzaji wa Sabato kwa tishio la adhabu kali. (Tazama Michael Geddes, Church History of Ethiopia, ukurasa 311, 312.) Lakini ukatili wa papa muda si mrefu ulikuja kuwa mzigo unaoudhi sana kiasi kwamba watu wa Abyssiania waliazimia kuuondoa mabegani mwao. Baada ya pambano la kutisha Warumi walifukuzwa kutoka katika maeneo yao, na imani yao ya zamani ilirudishwa upya. Makanisa yalifurahia uhuru wao, na hawakusahau somo walilojifunza kuhusu udanganyifu, ushikiliaji sana mambo bila kutumia akili, na mamlaka ya kiimla ya Rumi. Ndani ya ufalme wao uliojitenga waliridhika kubaki bila kujulikana kwa ulimwengu uliobaki wa Kikristo.PKSw 441.3

    Makanisa ya Afrika yalishika Sabato kama ilivyoshikwa na kanisa la papa kabla ya uasi kamili. Wakati ambapo walishika siku ya saba kutii amri ya nne ya Mungu, waliacha kazi siku ya Jumapili ili kwenda sawa na desturi ya kanisa. Baada ya kupata mamlaka ya juu kabisa, Rumi ilikanyaga Sabato ya Mungu na kuinua Jumapili yake; lakini makanisa ya Afrika, yakiwa yamefichwa kwa karibu miaka elfu moja, hayakushiriki katika uasi huu. Yalipoletwa chini ya utawala wa Rumi, yalilazimishwa kuacha Sabato ya kweli na kuinua sabato ya uongo; lakini haukupita muda mrefu baada ya kupata uhuru wao walirudia kuitii amri ya nne. (Tazama Kiambatisho.)PKSw 442.1

    Kumbukumbu hizi za nyuma hufunua waziwazi uadui wa Rumi na Sabato ya kweli na watetezi wa Sabato ya kweli, na mbinu ambazo Roma inazitumia kuheshimu siku waliyoiweka wenyewe. Neno la Mungu linafundisha kuwa mandhari hizi zitarudiwa wakati Wakatoliki wa Rumi na Waprotestanti watakapoungana katika kuiinua Jumapili.PKSw 442.2

    Unabii wa Ufunuo 13 hueleza kuwa mamlaka inayowakilishwa na mnyama mwenye pembe mbili mfano wa mwanakondoo ataifanya “dunia na wote wakaao ndani yake” wausujudie upapa—ambao katika unabii unawakilishwa na mnyama “mfano wa chui.” Mnyama mwenye pembe mbili pia atawaambia “wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama;” na, zaidi ya hapo, atawaamrisha wote, “wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,” wapokee alama ya mnyama (Ufunuo 13:11-16). Imeoneshwa kuwa nchi ya Marekani ndiyo mamlaka inayowakilishwa na mnyama mwenye pembe mbili mfano wa mwanakondoo, na kwamba unabii huu utatimizwa wakati nchi ya Marekani itakapolazimisha utunzaji wa Jumapili, jambo ambalo Rumi inadai kuwa utambuzi wa ukuu wake. Lakini katika heshima hii kwa upapa nchi ya Marekani haitakuwa peke yake. Nguvu ya Roma katika nchi ambazo wakati fulani zilikiri utawala wake bado haijaisha. Na unabii unatabiri urejeshwaji wa nguvu yake. “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule” (Aya 3). Pigo la jeraha la mauti huwakilisha kuanguka kwa upapa mwaka 1798. Baada ya hili, nabii anasema, “pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Paulo anataja wazi wazi kuwa“mtu wa kuasi“ataendelea hadi wakati wa ujio wa pili (2 Wathesalonike 2:3-8). Hadi mwisho wa wakati ataendelea na kazi yake ya kudanganya. Na nabii wa Ufunuo anaeleza, pia akizungumzia upapa: “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima” (Ufunuo 13:8). Katika Ulimwengu wa Kale na Ulimwengu Mpya, upapa utasujudiwa kwa heshima itakayotolewa kwa agizo la Jumapili, ambayo imejengwa juu ya mamlaka ya Kanisa la Rumi.PKSw 442.3

    Tangu katikati ya karne ya kumi na tisa, wanafunzi wa unabii katika nchi ya Marekani wamekuwa wakitoa ushuhuda huu kwa ulimwengu. Katika matukio yanayotokea sasa kunaonekana maendeleo ya haraka kuelekea kutimizwa kwa utabiri. Kwa upande wa walimu wa Kiprotestanti kuna dai lile lile la mamlaka ya Kiungu ya utunzaji wa Jumapili, na kutokuwepo kule kule kwa ushahidi wa Kimaandiko, kama ilivyo kwa viongozi wa kipapa walioghushi miujiza ili kujaza pengo la kutokuwepo kwa amri ya Mungu. Dai kuwa hukumu za Mungu zinamwagwa juu ya watu kwa kuvunja kwao sabato ya Jumapili, litarudiwa; tayari linaanza kusisitizwa. Na harakati za kulazimisha utunzaji wa Jumapili zinazidi kushika kasi.PKSw 443.1

    Kanisa la Rumi ni la ajabu katika werevu na ujanja. Linaweza kusoma kile kitakachokuwa. Linasubiri wakati mzuri, likizingatia kuwa makanisa ya Kiprotestanti yanalisujudia Kanisa la Rumi kwa kukubali sabato yake ya uongo na kuwa wanajiandaa kuilazimisha kwa njia zile zile lilizotumia katika siku zilizopita. Wanaokataa nuru ya ukweli watatafuta msaada wa mamlaka hii iliyojiweka yenyewe ili kuinua Jumapili ambayo ilianzishwa na mamlaka yenyewe. Ni kwa haraka kiasi gani Kanisa la Rumi litakuja kutoa msaada kwa Waprotestanti katika kazi hii ambayo siyo ngumu kujua cha kufanya. Ni nani anayejua vizuri zaidi ya viongozi wa upapa jinsi ya kushughulika na wale ambao siyo watiifu kwa kanisa?PKSw 443.2

    Kanisa Katoliki la Rumi, pamoja na taasisi zake zote ulimwenguni kote, huunda shirika moja kubwa chini ya udhibiti, na limebuniwa kukidhi maslahi ya, uongozi wa papa. Mamilioni ya waumini wake, katika kila nchi duniani kote, wanafundishwa kushikamana kwa pamoja katika utii kwa papa. Hata kama wana utaifa gani au wako chini serikali ipi, inawapasa kuchukulia kuwa mamlaka ya kanisa iko juu ya mamlaka zingine zote. Ingawa wanaweza kula kiapo cha utii kwa serikali zao, lakini nyuma yake kipo kiapo cha utii kwa Rumi, kikiwaondoa katika kila kiapo kilicho kinyume na maslahi ya Rumi.PKSw 443.3

    Historia inathibitisha juhudi za Rumi zenye ustadi wa hali ya juu na uvumilivu mkubwa za kujipenyeza katika mambo ya serikali; na ikipata nafasi, kuendeleza makusudi yake, hata kwa kuwaua wakuu na watu. Mwaka 1204, Papa Innocent III alipata kutoka kwa Petro II, mfalme wa Aragoni, kiapo kifuatacho, ambacho si cha kawaida: “Mimi, Petro, mfalme wa Waaragoni, nakiri na kuahidi kuwa mwaminifu na mtiifu daima kwa bwana wangu, Papa Innocent, kwa warithi wake wa Kikatoli, na Kanisa la Rumi, na kwa uaminifu kuhifadhi ufalme wangu katika utii wake, kuilinda imani ya Kikatoliki, na kuwatesa wazushi.”—John Dowling, The History of Romanism, b. 5, ch. 6, sec. 55. Jambo hili linaafikiana na madai yanayohusu mamlaka ya kiongozi wa Kanisa la Rumi “kuwa ni halali kwake kuwapindua wafalme” na “kwamba anaweza kuondoa utii wa raia kutoka kwa watawala dhalimu.”— Mosheim, b. 3, cent. 11, pt. 2, ch. 2, sec. 9, note 17. (Tazama pia maelezo ya Kiambatisho kwa ajili ya ukurasa wa 447.)PKSw 443.4

    Na ikumbukwe, ni majivuno ya Kanisa la Rumi kuwa halibadiliki. Kanuni za Gregori VII na Innocent III bado ndizo kanuni za Kanisa Katoliki la Rumi. Na kama lingekuwa na uwezo, lingeweza kutekeleza yote hayo kwa nguvu kama ilivyokuwa karne zilizopita. Waprotestanti wanajua kidogo kile wanachokifanya wanapopendekeza kukubali misaada ya Rumi katika kazi ya kuiinua Jumapili. Wakati wanajielekeza kutimiza kusudi lao, Rumi analenga kurudisha mamlaka yake, kufufua ukuu wake uliopotea. Acha kanuni ianzishwe katika nchi ya Marekani kuwa kanisa liweze kutumia au litawale nguvu ya dola; kuwa siku kuu za kidini zilazimishwe kuwa sheria za kiserikali; kwa kifupi, kuwa mamlaka ya kanisa na dola itawale dhamiri, na ushindi wa Rumi katika nchi ya Marekani utakuwa umethibitishwa.PKSw 444.1

    Neno la Mungu limetoa onyo la hatari inayokuja; acha onyo hili lisisikilizwe, na ulimwengu wa Waprotestanti utajifunza kile ambacho ni makusudi halisi ya Rumi, wakati ambao watakuwa wamechelewa kuepuka mtego. Kanisa la Rumi linaendelea kukua katika mamlaka yake kimya kimya. Mafundisho yanaendelea kueneza mvuto wake katika majengo ya kutunga sheria, katika makanisa, na katika mioyo ya watu. Linaendelea kurundika makanisa marefu na makali katika maeneo yaliyojificha ambayo ndani yake mateso yake ya zamani yatarudiwa. Kimya kimya na bila kushukiwa linaimarisha majeshi yake kuendeleza malengo yake ili wakati ukiwadia liweze kupiga. Linachohitaji ni kupata mazingira mazuri, na mazingira haya tayari linaendelea kutengenezewa. Siyo muda mrefu tutaona na tutahisi kusudi la Uroma ni nini. Ye yote atakayeliamini na kulitii neno la Mungu atapata aibu na mateso.PKSw 444.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents