Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 36—Pambano Linalotarajiwa Karibuni

    Tangu mwanzo kabisa wa pambano kuu mbinguni, kusudi la Shetani ni kupindua sheria ya Mungu. Ilikuwa kwa kusudi la kufanikisha jambo hili aliingia katika uasi dhidi ya Muumbaji wake, na ingawa alitupwa nje ya mbingu, anaendelea na vita ile ile duniani. Kudanganya wanadamu, na hatimaye kuwaongoza kuvunja sheria ya Mungu, ni lengo lake ambalo analitafuta kwa bidii sana. Iwe anafanikisha lengo hili kwa kutupilia mbali sheria yote kabisa, au kukataa sheria moja, matokeo ni yale yale hatimaye. Anayejikwaa “katika neno moja,” anaonesha dharau kwa sheria yote; mvuto na mfano wake vipo upande wa uvunjaji wa sheria; na huwa “amekosa juu ya yote” (Yakobo 2:10).PKSw 445.1

    Katika kutafuta kuonesha dharau kwa sheria ya Mungu, Shetani amepotosha mafundisho ya Biblia, na makosa hayo yameingizwa katika imani ya maelfu wanaodai kuamini Maandiko. Pambano kuu la mwisho kati ya ukweli na uongo ni shindano la mwisho la pambano la muda mrefu juu ya sheria ya Mungu. Tunaingia sasa katika vita hii—vita kati ya kanuni za Yehova na sheria za wanadamu, kati ya dini ya Biblia na dini ya hadithi za kubuni na mapokeo ya wanadamu.PKSw 445.2

    Mawakala ambao wataungana dhidi ya ukweli na haki katika shindano hili sasa wako kazini. Neno takatifu la Mungu, ambalo limerithishwa kwetu kwa gharama kubwa ya mateso na damu, linathaminiwa kidogo sana. Biblia inaweza kupatikana kwa watu wote, lakini kuna watu wachache sana wanaoikubali kama mwongozo wa maisha. Ukafiri unatawala kwa kiwango kikubwa na cha kutisha, siyo katika ulimwengu pekee, bali pia kanisani. Wengi wameyakana mafundisho ambayo ni nguzo hasa za imani ya Kikristo. Ukweli mkuu wa uumbaji kama ulivyowasilishwa na waandishi waliovuviwa, anguko la mwanadamu, upatanisho, na uendelevu wa sheria ya Mungu, vinakataliwa wazi wazi, ama sheria yote au sehemu yake, na ulimwengu unaodai kuwa wa Kikristo. Maelfu ya watu wanaojivuna kuwa wenye hekima na walio huru huchukulia kuwa ni udhaifu kuiamini kabisa Biblia; wanafikiri kuwa ni ushahidi wa talanta ya juu na usomi wa hali ya juu kuyakataa Maandiko na kuupinga ukweli wake muhimu. Wachungaji wanawafundisha watu wao, na maprofesa na walimu wanawafundisha wanafunzi wao, kuwa sheria ya Mungu imebadilishwa au imefutwa; na wale wanaochukulia matakwa yake kuwa bado ni ya halali, yanayopaswa kutiiwa kama yalivyo, wanafikiriwa kuwa watu wa kudharauliwa au kudhihakiwa.PKSw 445.3

    Kwa kuukataa ukweli, wanadamu wanamkataa Mwasisi wa ukweli. Kwa kuikataa sheria ya Mungu, watu wanaikana mamlaka ya Mtoa sheria. Ni rahisi kuchonga sanamu ya mafundisho ya uongo na nadharia za uongo sawa na kuchonga sanamu ya mti au jiwe. Kwa kuwasilisha vibaya sifa za Mungu, Shetani anawaongoza watu kumwelewa Mungu kwa tabia isiyokuwa sahihi. Kwa watu wengi, sanamu ya kifalsafa imewekwa juu ya kiti cha enzi badala ya Yehova; wakati Mungu aliye hai, kama alivyofunuliwa katika neno Lake, ndani ya Kristo, na katika kazi za uumbaji, anaabudiwa na watu wachache. Maelfu ya watu wanafanya vitu vya asili kuwa miungu yao huku wakimkataa Mungu wa vitu vya asili. Japokuwa ni katika miundo mbalimbali, ibada ya sanamu ipo katika ulimwengu wa Kikristo leo katika uhalisia wake kama ilivyokuwa miongoni mwa Waisraeli katika siku za Eliya. Mungu wa wengi wanaodai kuwa wenye hekima, wanafalsafa, watunzi wa mashairi, wanasiasa, waandishi wa habari—mungu wa wanamitindo, mungu wa vyuo na vyuo vikuu, hata mungu wa baadhi ya taasisi za kitheolojia—ni miungu isiyomzidi sana Baali, mungu jua wa Wafoinike.PKSw 445.4

    Hakuna kosa ambalo likikubaliwa na ulimwengu wa Kikristo linapiga kwa ujasiri zaidi dhidi ya mamlaka ya Mbingu, hakuna kosa ambalo linapingana zaidi na busara tu ya kawaida, hakuna kosa lililo na matokeo mabaya zaidi, kuliko fundisho la kisasa, ambalo linaendelea kukubaliwa na watu wengi kwa kasi, kuwa sheria ya Mungu haiwafungi watu tena. Kila taifa lina sheria zake, ambazo zinaheshimiwa na kutiiwa; hakuna serikali inayoweza kudumu kuwepo ikiwa haina sheria; na inawezaje kuingia akilini kuwa Muumbaji wa mbingu na nchi hana sheria za kutawala viumbe aliowaumba? Hebu chukulia kuwa wachungaji mashuhuri waanze kufundisha hadharani kuwa sheria zinazotawala nchi na zinazotawala haki za wananchi si za lazima— kuwa zinabana uhuru wa watu, na hivyo hazipaswi kutiiwa; watu hao wangeweza kuvumiliwa kwa muda gani wakifundisha hivyo mimbarani? Lakini, je, ni kosa kubwa zaidi kupuuza sheria za nchi na za mataifa kuliko kukanyaga kanuni za Mungu ambazo ndiyo msingi wa serikali zote?PKSw 446.1

    Ingekuwa afadhali kwa mataifa kuondoa sheria zao, na kuwaruhusu watu wafanye wanavyopenda, kuliko Mtawala wa sayari zote kubatilisha sheria Yake, na kuuacha ulimwengu bila kiwango cha kuhukumu mwenye hatia au kumpa haki mtiifu. Je, tungependa kujua matokeo ya kubatilisha sheria ya Mungu? Jaribio limeshawahi kufanywa. Matokeo yake yalikuwa ya kutisha kama nini katika nchi ya Ufaransa wakati ukanamungu ulipofanywa kuwa mamlaka ya utawala. Wakati huo ilidhihirika kwa ulimwengu kuwa kutupilia mbali vizuizi ambavyo Mungu ameviweka ni kuruhusu utawala wa ukatili wa watu katili. Kiwango cha haki kinapoondolewa, njia inafunguliwa kwa ajili ya mfalme wa uovu kuimarisha mamlaka yake duniani.PKSw 446.2

    Mahali popote sheria za Mungu zinapokataliwa, dhambi inaacha kuwa na ubaya na haki inakosa umuhimu na haitamaniwi. Wanaokataa kujisalimisha chini ya serikali ya Mungu hawafai kabisa kujiongoza wenyewe. Kwa njia ya mafundisho yao mabaya roho ya uasi inapandikizwa katika mioyo ya watoto na vijana, ambao kwa asili hawana uvumilivu wa kutawaliwa; na matokeo yake ni hali ya uasi na uvunjaji wa sheria katika jamii. Wakati wakidhihaki wepesi wa kuamini wale wanaotii matakwa ya Mungu, watu walio wengi wanapokea kwa furaha udanganyifu wa Shetani. Wanasalimisha hatamu zao kwa tamaa na wanatenda dhambi ambazo zinaleta hukumu juu ya wapagani.PKSw 446.3

    Wale ambao wanafundisha watu kuchukulia kwa wepesi amri za Mungu wanapanda mbengu ya uasi wavune matunda ya uasi. Acha kizuizi kilichowekwa na sheria ya Mungu kiondolewe kabisa, na sheria za wanadamu zitapuuzwa muda si mrefu. Kwa kuwa Mungu anakataza matendo yasiyokuwa ya uaminifu, kutamani, kusema uongo, na kudanganya, wanadamu wako tayari kukanyaga amri za Mungu kama kikwazo cha kupata mafanikio ya kidunia; lakini matokeo ya kuondoa kabisa kanuni hizi yangekuwa tofauti kabisa na jinsi walivyotegemea. Ikiwa sheria haimbani mtu, kwa nini mtu ye yote aogope kuivunja? Mali isingeweza salama tena. Watu wangejipatia mali za jirani zao kwa mabavu, na walio na nguvu zaidi kuliko wengine ndiyo wangekuwa matajiri kuliko watu wote. Uhai wenyewe usingeheshimiwa. Kiapo cha ndoa kisingekuwa tena ngome takatifu ya kuilinda familia. Yule ambaye angekuwa na nguvu nyingi, angeweza, akipenda, kumchukua mke wa jirani yake kwa nguvu. Amri ya tano ingeondolewa na amri ya nne. Watoto wasingesita kuwaua wazazi wao ikiwa kwa kufanya hivyo wangeweza kupata mahitaji ya mioyo yao iliyoharibika. Ulimwengu uliostaarabika ungekuwa genge la majambazi na wauaji; na amani, utulivu, na furaha vingetoweka duniani.PKSw 447.1

    Tayari fundisho kuwa watu wameachiliwa kutoka katika utii wa matakwa ya Mungu limedhoofisha nguvu ya uwajibikaji wa kiuadilifu na limefungulia mafuriko ya uovu ulimwenguni. Uasi, ubadhirifu, na ufisadi vinatufunika kama wimbi la maji. Katika familia, Shetani yuko kazini. Bendera yake inapepea hata katika nyumba zinazodai kuwa za Kikristo. Kuna kijicho, kuwazia mabaya wengine, unafiki, utengano, uadui, ugomvi, usaliti wa mambo matakatifu, uendekezaji wa tamaa mbaya. Mfumo mzima wa kanuni na mafundisho ya kidini, ambao ungeunda msingi na mwelekeo wa maisha ya kijamii, unaonekana kama bonge linaloyeyuka, linaloekea kutoweka. Wahalifu wakuu, wanapotupwa gerezani kwa makosa yao, mara nyingi wanapewa zawadi na kushabikiwa sana kana kwamba wamepata ushindi fulani mkubwa wa kuonewa wivu. Tabia yao na uhalifu wao unatanganzwa sasa. Vyombo vya habari vinatangaza uovu wao kwa kina, na kwa njia hiyo vinawafundisha wengine kufanya matendo ya wizi, unyang'anyi, na mauaji; na Shetani anashangilia mafanikio ya mipango yake ya kijehanamu. Kufurahia uovu, mauaji ya kikatili, ongezeko la kutisha la kutokuwa na kiasi na uovu wa kila aina na wa kila kiwango, vyapaswa kuwaamsha wote wanaomcha Mungu, kujiuliza nini kifanyike kuzuia wimbi la uovu.PKSw 447.2

    Mahakama zinapokea rushwa. Watawala wanasukumwa na tamaa ya mapato na kupenda anasa za mwili. Kukosa kiasi kumetia mawingu akili za wengi kiasi kwamba Shetani anawatawala karibu katika kila hali. Ulevi na sherehe, tamaa, kijicho, kukosa uaminifu kwa njia mbalimbali, vinawakilishwa miongoni mwa wale wanaosimamia sheria.” Haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia” (Isaya 59:14).PKSw 448.1

    Uovu na giza la kiroho vilivyotawala chini ya himaya ya Rumi vilikuwa matokeo ya moja kwa moja ya kukandamiza Maandiko; lakini ni wapi tunapata chimbuko la ukafiri ulioenea kote, kuikataa sheria ya Mungu, na ufisadi unaofuata baada ya kuikataa sheria ya Mungu, chini ya nuru kamilifu ya injili katika zama za uhuru wa kidini? Sasa kwa kuwa Shetani hawezi kuendelea zaidi kuutawala ulimwengu kwa kuzuia Maandiko, anatumia njia zingine kutimiza lengo lile lile. Kuharibu imani kwa Biblia kunamsaidia Shetani kutimiza kusudi lake na kuharibu Biblia yenyewe. Kwa kuingiza imani kuwa sheria ya Mungu haimbani mtu, Shetani anawaongoza watu kirahisi kuivunja kana kwamba hawajui kanuni zake. Na sasa, kama ilivyokuwa katika zama za kale, amefanya kazi kupitia kanisa kuendeleza mipango yake. Mashirika ya kidini ya leo yamekataa kusikiliza ukweli usiopendwa ulioelezwa wazi wazi katika Maandiko, na ili kuushinda huo ukweli wameupatia tafsiri na wameweka misimamo ambayo imepanda kila mahali mbegu za mashaka. Wakishikilia makosa ya kipapa ya asili ya kutokufa na ufahamu katika umauti, wamekataa ulinzi pekee dhidi ya madanganyifu ya imani ya kuongea na wafu. Fundisho la maumivu ya milele motoni limewafanya wengi kutoiamini Biblia. Na madai ya amri ya nne yanapoelezwa kwa watu, inaonekana kuwa utunzaji wa Sabato ya siku ya saba umeamriwa; na kama njia pekee ya kujinasua kutoka katika wajibu ambao hawako tayari kuufanya, walimu mashuhuri walio wengi hutangaza kuwa sheria ya Mungu haimbani mtu tena. Hivyo wanatupilia mbali sheria pamoja na Sabato. Kwa kadiri kazi ya matengenezo ya Sabato inavyopanuka, ukataaji huu wa sheria ya Mungu ili kuepuka madai ya amri ya nne utakuwa karibu na watu wote duniani. Mafundisho ya viongozi wa dini wamefungulia mlango ukafiri, imani ya kuongea na wafu, na dharau kwa sheria takatifu ya Mungu; na juu ya viongozi hawa kuna uwajibikaji wa kutisha kwa ajili ya uovu uliomo katika ulimwengu wa Kikristo.PKSw 448.2

    Hata hivyo, tabaka hili hili wanadai kuwa ufisadi unaoenea kwa kasi unatokana na kunajisi kile kinachoitwa “sabato ya Kikristo,” na kuwa ulazimishaji wa utunzaji wa Jumapili utaweza kuboresha zaidi maadili ya jamii. Dai hili linasisitizwa hasa hasa Amerika, mahali ambapo fundisho la Sabato ya kweli limehubiriwa sana. Hapa, kazi ya kiasi, moja ya matengenezo ya kimaadili na muhimu sana, mara nyingi inaunganishwa na vuguvugu la Jumapili, na watetezi wa Jumapili wenyewe wanajinasibu kuwa wanafanya kazi ya kutetea maslahi ya jamii; na watu wanaokataa kuungana nao wanalaumiwa kama maadui wa kiasi na matengenezo. Lakini ukweli kuwa vuguvugu la kuendeleza uongo limeunganishwa na kazi ambayo kama ilivyo yenyewe ni nzuri, siyo hoja ya kuunga mkono uongo. Tunaweza kuificha sumu kwa kuichanganya na chakula kizuri, lakini hatubadilishi asili yake. Kinyume chake, imefanywa kuwa ya hatari zaidi, kwa kuwa ina uwezekano wa kumezwa na mtu bila habari. Ni moja ya mbinu za Shetani kuchanganya uongo na ukweli ili kuupa uongo uwezo wa kukubalika. Viongozi wa vuguvugu la Jumapili wanaweza kutetea matengenezo ambayo watu wanayahitaji, kanuni ambazo zinapatana na Biblia; lakini, kwa kuwa matengenezo haya yamechanganywa na takwa ambalo ni kinyume na sheria ya Mungu, watumishi Wake hawawezi kuungana nao. Hakuna jambo lolote linaloweza kuwahalalisha kwa kuacha amri za Mungu na badala yake kutii kanuni za wanadamu.PKSw 448.3

    Kwa njia ya mafundisho mawili ya uongo, kutokufa kwa roho na utakatifu wa Jumapili, Shetani atawaweka watu chini ya madanganyifu yake. Wakati fundisho la kwanza linajenga msingi wa imani ya kuongea na wafu, fundisho la pili linajenga mshikamano wa kuikubali Rumi. Waprotestanti wa Marekani watakuwa mstari wa mbele katika kunyosha mikono yao kutoka upande mmoja hadi mwingine wa korongo refu kushikana mikono na imani ya kuongea na wafu; watavuka shimo kubwa kushikana mikono na mamlaka ya Kirumi; na chini ya mvuto wa muungano wa mamlaka tatu, nchi hii itafuata katika nyayo za Rumi katika kukanyaga haki za dhamiri.PKSw 449.1

    Kwa kuwa imani ya kuongea na wafu inaigiza kwa karibu sana Ukristo wa jina wa wakati wetu, ina nguvu zaidi ya kudanganya na kunasa. Shetani mwenyewe ameongoka, kulingana na hali ya sasa ya mambo. Atatokea katika tabia na mwonekano wa malaika wa nuru. Njia ya wakala wa imani ya kuongea na wafu, miujiza itatendwa, wagonjwa wataponywa, na maajabu mengi yasiyokanushika yatafanywa. Na kwa kuwa pepo watadai kuwa wanaiamini Biblia, na kuonesha heshima kwa taasisi za kanisa, kazi zao zitakubaliwa kama udhihirisho wa nguvu ya Mungu.PKSw 449.2

    Mstari unaogawa watu kati ya wanaojiita Wakristo na watu wasiomwamini Mungu kwa sasa hauonekani vizuri. Washiriki wa Kanisa wanapenda vitu ambavyo watu wa kidunia wanavipenda na wako tayari kujiunga nao, na Shetani ameazimia kuwaunganisha wote katika jumuiya moja na kwa njia hiyo aweze kuimarisha kazi yake kwa kuwaingiza watu wote katika imani ya kuongea na wafu. Waumini wa mfumo wa upapa, wanaojivunia miujiza kama ishara ya kanisa la kweli, watadanganywa kirahisi na nguvu hii inayotenda miujiza; na Waprotestanti, wakiwa wametupilia mbali ngao ya ukweli, nao pia watadanganywa. Waumini wa upapa, Waprotestanti, na watu wa kidunia wote kwa pamoja wataupokea mfano huo wa utauwa usiokuwa na nguvu ya Mungu, na wataona katika muungano huo vuguvugu kubwa la kuuongoa ulimwengu na uingizaji wa kipindi cha miaka elfu moja kilichosubiriwa kwa muda mrefu.PKSw 449.3

    Kwa njia ya imani ya kuongea na wafu, Shetani ataonekana kama mfadhili wa jamii ya wanadamu, akiponya magonjwa ya watu, na akidai kuwasilisha mfumo mpya na wa juu zaidi wa imani ya kidini; lakini wakati huo huo anafanya kazi kama muuaji. Majaribu yake yanawaongoza wengi kwenda kuuawa. Kutokuwa na kiasi kunaondoa uwezo wa kufikiri vizuri; kupenda anasa, migogoro, na umwagaji damu hufuata. Shetani anapenda sana vita, kwa sababu vita vinaamsha mihemko mibaya zaidi kuliko yote kutoka rohoni na vinawafagilia wahanga wote katika umilele wakiwa na mwelekeo wa uovu na umwagaji damu. Ni kusudi lake kuchochea mataifa yapigane vita taifa moja dhidi ya taifa jingine, kwa sababu kwa njia hiyo anaweza kuhamisha akili ya watu isijishughulishe na kazi ya maandalizi ya kusimama katika siku ya Mungu.PKSw 450.1

    Shetani hufanya kazi kupitia nguvu za asili kukusanya mavuno yake ya roho zisizojiandaa. Amejifunza siri za maabara ya ulimwengu, na anatumia nguvu zake zote kutawala nguvu za asili kwa kiwango kile ambacho Mungu anaruhusu. Aliporuhusiwa kumtesa Ayubu, ni kwa kasi kubwa kiasi gani kondoo, ngamia, ng'ombe, watumishi, nyumba, watoto, walifagiliwa mbali, janga moja likifuata jingine kama kwa dakika moja. Ni Mungu anayewakinga viumbe Wake na kuwazungushia wigo dhidi ya nguvu ya mwuaji. Lakini ulimwengu wa Kikristo umeonesha dharau kwa sheria ya Yehova; na Bwana atafanya vile ambavyo ameahidi kuwa atafanya—ataondoa mibaraka Yake duniani na ataondoa ulinzi Wake kwa wale wanaoasi dhidi ya sheria Yake na kuwafundisha na kuwalazimisha wengine kuasi kama wao. Shetani anawatawala wale wote ambao hawako chini ya ulinzi wa Mungu. Shetani anawapendelea na kuwafanikisha baadhi ili kuendeleza mipango yake, na atawaletea matatizo wengine na kuwaongoza watu kuamini kuwa ni Mungu anayewatesa.PKSw 450.2

    Wakati akionekana kwa wanadamu kama mganga mkuu anayeweza kuponya magonjwa yao, ataleta magonjwa na majanga, hadi miji yenye wakazi wengi itabaki magofu na ukiwa. Hata sasa yuko kazini. Katika ajali na majanga katika bahari na katika nchi kavu, ajali za mioto mikubwa, katika vimbunga vikali na tufani ya mvua ya mawe ya kutisha, katika dhoruba, mafuriko, tufani, mawimbi ya kujaa na kupya kwa bahari, na matetemeko ya ardhi, kila mahali na katika miundo maelfu, Shetani anatumia nguvu yako. Anafagia mazao yanayoelekea kukomaa, na njaa na hofu hufuata. Anaweka hewani harufu mbaya inayofisha, na maelfu huangamia kwa magonjwa. Matukio haya yatazidi kuwa ya mara kwa mara na ya kutisha zaidi. Mauti itakuwa juu ya mwanadamu na mnyama. “Dunia inaomboleza, inazimia,” “watu wakuu ... wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele” (Isaya 24:4, 5).PKSw 450.3

    Na ndipo mdanganyaji mkuu atawashawishi watu kuwa wanaomtumikia Mungu ndiyo chimbuko la majanga hayo. Tabaka ambalo limechokoza hasira ya Mbingu litatupia lawama kwa wale ambao utii wao kwa amri za Mungu ni kemeo la kudumu kwa wakosaji. Itatangazwa kuwa watu wanamkosea Mungu kwa kuvunja sabato ya Jumapili; kuwa dhambi imeleta majanga ambayo hayatakoma mpaka utunzaji wa Jumapili utakapotekelezwa kikamilifu; na kuwa wale wanaowasilisha madai ya amri ya nne, na kwa njia hiyo kuharibu heshima kwa ajili ya Jumapili, ni wataabishaji wa watu, wakizuia urejeshwaji wao kwa upendeleo wa Mungu na mafanikio ya duniani. Kwa hiyo shitaka lililotolewa zamani na mtumishi wa Mungu litarudiwa na kwa sababu ambazo ni za msingi: “Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli? Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali” (1 Wafalme 18:17, 18). Wakati hasira ya watu itakapochochewa kwa mashitaka ya uongo, watafuata njia ya kutafuta kuwaua mabalozi wa Mungu sawa sawa na jinsi Waisraeli walioasi walivyotafuta kumuua Eliya.PKSw 451.1

    Nguvu itendayo miujiza inayodhihirishwa kwa njia ya imani ya kuongea na wafu itaeneza mvuto wake dhidi ya wale wanaochagua kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mawasiliano kutoka kwa roho za pepo yatatangaza kuwa Mungu amewatuma kuwashawishi wapinzani wa Jumapili kuhusu kosa lao, yakithibitisha kuwa sheria za nchi zinapaswa kutiiwa kama sheria ya Mungu. Watasikitika kwa sababu ya uovu mkubwa ulioko ulimwenguni na wataunga mkono ushuhuda wa viongozi wa dini kuwa hali ya maadili yaliyoporomoka imesababishwa na kunajisi Jumapili. Hasira kubwa itachochewa dhidi ya wote watakaokataa kukubali ushuhuda wao.PKSw 451.2

    Sera ya Shetani katika mgogoro huu wa mwisho na watu wa Mungu ni ile ile aliyoitumia wakati wa uanzishaji wa pambano kuu mbinguni. Alieleza kwamba alikuwa akitafuta kuongeza uimara wa serikali ya Mungu, wakati kisirisiri alikuwa akielekeza juhudi zake zote kutafuta njia za kuipindua. Na kazi ile ile aliyokuwa akitafuta kuifanya aliwasingizia malaika watiifu kuwa ndio walikuwa wakiifanya. Sera ile ile ya udanganyifu imekuwa sifa ya historia ya Kanisa la Rumi. Linaeleza kuwa linafanya kazi kama mwakilishi wa Mbingu, wakati likitafuta kujiinua juu ya Mungu na kubadilisha sheria Yake. Chini ya utawala wa Rumi, wale waliouawa kwa ajili ya uaminifu wao kwa injili walilaumiwa kama watenda maovu; walitangazwa kuwa na mshikamano na Shetani; na kila njia inayowezekana ilitumika kuwafanya wadharauliwe, kuwafanya waonekane katika macho ya watu na hata kwao wenyewe kuwa ni wabaya kuliko wahalifu wote. Ndivyo itakavyokuwa hata sasa. Wakati akitafuta kuwaangamiza wale wanaoheshimu sheria ya Mungu, atasababisha washitakiwe kama wavunja sheria, kama watu wanaomkosea heshima Mungu na kuleta hukumu juu ya dunia.PKSw 451.3

    Mungu halazimishi nia au dhamiri; lakini juhudi ya Shetani daima— kutawala wale ambao hawezi kuwashawishi— ni kulazimisha kwa ukatili. Kwa njia ya hofu au nguvu hutafuta kutawala dhamiri na kupata fursa ya yeye mwenyewe kuabudiwa. Kufanikisha hili kusudi, hufanya kazi kupitia mamlaka za kidini na kiserikali, akiwaongoza kulazimisha sheria za wanadamu zinazopingana na sheria ya Mungu.PKSw 452.1

    Wanaoheshimu Sabato ya Biblia watashutumiwa kama maadui wa sheria na utaratibu, kama watu wanaovunja vizuizi vya maadili vya jamii, wakisababisha uasi na ufisadi, na kuita hukumu za Mungu juu ya ardhi. Uaminifu wao usioyumba utatangazwa kuwa ukaidi, ukorofi, na dharau kwa mamlaka. Watashitakiwa kwa kukosa uzalendo kwa serikali. Wachungaji wanaokataa uwajibishaji wa sheria ya Mungu watahubiri kutoka madhabahuni wajibu wa utii kwa mamlaka za kidunia umeamuriwa na Mungu. Katika majengo ya kutunga sheria na mahakama za kutoa haki, watunza amri watawakilishwa vibaya na kuhukumiwa. Tafsiri ya uongo itatolewa kwa maneno yao; na nia zao zitatafsiriwa vibaya.PKSw 452.2

    Makanisa ya Kiprotestanti yanapokataa hoja za wazi, za Kimaandiko zinazotetea sheria ya Mungu, watatamani kuwanyamazisha wale ambao imani yao hawawezi kuishinda kwa Biblia. Ingawa wanafumba macho yao wasiuone ukweli, sasa wanapita katika njia ambayo itawaongoza kuwatesa wale ambao, kwa kutii dhamiri zao, watakataa kufanya kile ambacho ulimwengu wote wa Kikristo unakifanya, na kukiri madai ya sabato ya kipapa.PKSw 452.3

    Viongozi wa kanisa na wa dola wataungana kuhonga, kushawishi, au kulazimisha matabaka yote kuiheshimu Jumapili. Kukosekana kwa mamlaka ya Kiungu kutajazwa kwa sheria kandamizi. Ufisadi wa kisiasa unaua kupenda haki na kuheshimu ukweli; na hata katika nchi huru ya Marekani, watawala na watunga sheria, ili wapate ukubali wa umma, watajisalimisha kwa madai ya walio wengi kwa ajili ya sheria ya kulazimisha utunzaji wa Jumapili. Uhuru wa dhamiri, ambao umegharimu kafara kubwa, hautaheshimiwa tena. Katika pambano linalokuja tutaona mfano wa maneno ya nabii: “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu” (Ufunuo 12:17).PKSw 452.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents