Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 30—Uadui kati ya Mwanadamu na Shetani

    “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwanzo 3:15). Hukumu ya Mungu dhidi ya Shetani baada ya anguko la mwanadamu ilikuwa pia unabii, ukijumuisha zama zote hadi wakati wa mwisho na ukiashiria kuwa pambano kuu litahusisha kabila zote za watu watakaoishi duniani.PKSw 386.1

    Mungu anatangaza: “Nami nitaweka uadui” Uadui huu hautokei kwa asili moja kwa moja. Mwanadamu alipovunja sheria ya Mungu, asili yake ilibadilika na kuwa ya uovu, na alikuwa na upatanifu, na siyo tofauti, na Shetani. Hakuna uadui wa asili kati ya mwanadamu mwenye dhambi na mwasisi wa dhambi. Wote ni waovu kwa sababu ya uasi. Mwasi hatulii, mpaka apate huruma na kuungwa mkono kwa kuwashawishi wengine wafuate mfano wake. Kwa sababu hiyo malaika walioanguka na watu waovu huungana katika urafiki wa kutapatapa. Ikiwa Mungu asingeingilia, Shetani na mwanadamu wangeungana na kuunda umoja dhidi ya Mbingu; na badala ya kujenga uadui dhidi ya Shetani, familia nzima ya mwanadamu ingejiunga dhidi ya Mungu.PKSw 386.2

    Shetani alimjaribu mwanadamu kutenda dhambi, kama alivyosababisha malaika kuasi, ili aweze kupata ushirikiano wao katika vita yake dhidi ya Mbingu. Kulikuwa hakuna mgawanyiko kati yake na malaika walioanguka katika suala la chuki dhidi ya Krito; wakati katika mambo mengine yote kulikuwa na uhasama miongoni mwao, waliungana kikamilifu katika kupinga mamlaka ya Mtawala wa Ulimwengu. Lakini Shetani aliposikia tangazo kuwa uadui unapaswa kuwepo kati yake na mwanamke, na kati ya uzao wake na uzao wa mwanamke, alitambua kuwa juhudi zake za kuharibu asili ya mwanadamu zingeingiliwa; kuwa kwa namna fulani mwanadamu angewezeshwa kupinga nguvu zake.PKSw 386.3

    Uadui wa Shetani dhidi ya uzao wa mwanadamu unawashwa moto kwa sababu, kwa njia ya Kristo, wanapata fursa ya kupokea upendo na rehema za Mungu. Shetani anatamani kukwamisha mpango wa Mungu wa ukombozi wa mwanadamu, kumkosesha Mungu heshima, kwa kufuta na kuharibu kazi ya mikono Yake; anatamani kuleta huzuni mbinguni na kuijaza dunia kwa huzuni na ukiwa. Na anaonesha mabaya yote haya kama matokeo ya kazi ya Mungu katika kumuumba mwanadamu.PKSw 386.4

    Ni neema anayoweka Kristo katika roho ambayo huleta uadui ndani ya mtu dhidi ya Shetani. Bila neema hii inayobadilisha na nguvu inayoumba upya, mwanadamu angeendelea kuwa mateka wa Shetani, mtumishi aliye tayari daima kutii maagizo ya Shetani. Lakini kanuni mpya katika roho inaumba mgogoro mahali palipokuwa na amani. Nguvu ambayo Kristo anaitoa inamwezesha mwanadamu kumpinga dhalimu na mnyang'anyi. Ye yote anayeonekana kuichukia dhambi badala ya kuipenda, ye yote anayezipinga na kuzishinda tamaa ambazo zimekuwa zikitawala ndani yake, anaonesha utendaji kazi wa kanuni inayotoka mbinguni.PKSw 386.5

    Upinzani uliopo kati ya roho ya Kristo na roho ya Shetani ulionekana kwa uwazi zaidi katika namna ulimwengu ulivyompokea Yesu. Sababu kubwa ya Wayahudi kumkataa Yesu haikuwa mwonekano Wake wa kutokuwa na mali za dunia, kutokuwa na ufahari, au kutokuwa na utukufu. Waliona kuwa alikuwa na nguvu ambayo ilikuwa muhimu zaidi kuliko hata hayo mambo ya kidunia. Lakini usafi na utakatifu wa Kristo ulisababisha chuki dhidi yake kutoka kwa watu wasiomcha Mungu. Maisha yake ya kujikana nafsi na uaminifu usiokuwa na dhambi ulikuwa kemeo la daima dhidi ya watu wenye kiburi na tamaa. Jambo hili ndilo liliwasha moto wa uadui dhidi ya Mwana wa Mungu. Shetani na malaika waovu waliungana na watu waovu. Nguvu zote za uasi ziliungana dhidi ya Jemadari wa ukweli.PKSw 387.1

    Uadui huo huo unaoneshwa dhidi ya wafuasi wa Kristo kama ulivyooneshwa dhidi ya Bwana wao. Ye yote anayeona ukakasi wa dhambi, kwa nguvu itokayo mbinguni anapinga majaribu, kwa hakika atawasha moto wa ghadhabu wa Shetani na wa wafuasi wake. Chuki dhidi ya kanuni safi za ukweli, na shutuma na mateso dhidi ya watetezi wa ukweli, vitaendelea kuwepo kwa kadiri dhambi na wenye dhambi wanavyodumu kuwepo. Wafuasi wa Kristo na watumwa wa Shetani hawawezi kuafikiana. Kwazo la msalaba halijabatilika. “Wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” (2 Timotheo 3:12).PKSw 387.2

    Mawakala wa Shetani wanafanya kazi daima chini ya maelekezo yake kustawisha mamlaka yake na kujenga ufalme wake katika kupingana na serikali ya Mungu. Kwa ajili hii wanatafuta kuwadanganya wafuasi wa Kristo na kuwafanya waachane na utiifu wao kwa Kristo. Kama kiongozi wao alivyo, wanatafsiri vibaya na kupotosha Maandiko ili kutimiza lengo lao. Kama vile Shetani alivyomtupia lawama Mungu, kadhalika mawakala wa Shetani huwasingizia watu wa Mungu. Roho ile iliyomwua Yesu inawachochea waovu kuwaangamiza wafuasi Wake. Yote haya yalitabiriwa katika unabii ule wa kwanza: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake.” Na uadui huu utaendelea mpaka mwisho wa wakati.PKSw 387.3

    Shetani hukusanya majeshi yake yote na kuingiza nguvu zake zote vitani. Kwa nini hakutani na upinzani mkubwa zaidi? Kwa nini askari wa Kristo wanasinzia na hawajali? Ni kwa sababu wana mshikamano mdogo sana na Kristo; ni kwa sababu hawana Roho Wake. Kwa hiyo dhambi haipingwi na haichukiwi, kama Bwana wao ilivyoipinga na alivyoichukia. Hawaikabili, kama Kristo alivyoikabili, kwa upinzani mkubwa na wa makusudi. Hawatambui uovu na ubaya wa dhambi, na ni vipofu wasioweza kuona tabia na nguvu ya mfalme wa giza. Kuna uadui mdogo sana dhidi ya Shetani na kazi zake, kwa sababu kuna ujinga mkubwa kuhusu nguvu yake na ubaya wake, na ukubwa wa vita yake dhidi ya Kristo na Kanisa Lake. Watu wengi wanadanganyika hapa. Hawajui kuwa adui yao ni generali mwenye nguvu nyingi anayetawala akili za malaika waovu, na kwamba kwa mipango kabambe na mikakati makini anapigana vita dhidi ya Kristo ili kuzuia wokovu wa roho. Miongoni mwa wanaojiita Wakristo, na hata miongoni mwa wahudumu wa injili, mara chache utasikia Shetani akigusiwa, isipokuwa pengine kumtaja kwa dharura mimbarani. Wanashindwa kuona ushahidi wa utendaji wake na mafanikio yake endelevu; wanapuuza maonyo mengi dhidi ya hila zake; wanaonekana kutojali hata uwepo wake mwenyewe.PKSw 387.4

    Wakati ambapo watu hawana ufahamu wa mbinu zake, adui huyu asiyelala usingizi anafuatilia nyendo zao kila wakati. Anapenyeza uwepo wake katika kila idara ya nyumbani, katika kila mtaa wa miji, katika makanisa, katika mabaraza ya kitaifa, katika mahakama, akileta mashaka, akidanganya, akishawishi, kila mahali akiharibu roho na miili ya wanaume, wanawake, na watoto, akivunja familia, akipanda mbegu za chuki, ushindani, ugomvi, uasi, na mauaji. Na ulimwengu wa Kikristo unaelekea kuchukulia mambo haya kana kwamba yamepangwa na Mungu na kuwa ni lazima yawepo.PKSw 388.1

    Shetani anatafuta daima kuwashinda watu wa Mungu kwa kuvunja vizuizi ambavyo vinawatenga na ulimwengu. Waisraeli wa zamani walishawishiwa kutenda dhambi walipojiingiza katika mahusiano haramu na wapagani. Kwa jinsi ile ile wana Israeli wa leo wanapotoshwa. “Mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu” (2 Wakorintho 4:4). Wote ambao siyo wafuasi wa Kristo wenye msimamo thabiti ni watumishi wa Shetani. Ndani ya moyo usioumbwa upya kuna kuipenda dhambi na tabia ya kuipalilia na kuitolea udhuru. Ndani ya moyo ulioumbwa upya kuna kuichukia dhambi na upinzani wa makusudi dhidi ya dhambi. Wakristo wanapochagua kushirikiana na watu wasiomcha na wasiomwamini Mungu, wanakaribisha majaribu wenyewe. Shetani anajificha ili asionekane na anawafunika macho yao wasione mitego ya hila zake. Hawawezi kuona kuwa urafiki kama huo umepangwa kuwaumiza; na huku kwa wakati wote huo wakiwa wanajenga tabia ya ulimwengu, katika maneno na matendo, wanazidi kuwa vipofu.PKSw 388.2

    Kufuata desturi za ulimwengu kunaongoa kanisa na kulifanya liwe la ulimwengu; hakuwezi kuuongoa ulimwengu na kuuleta kwa Kristo. Kuzoeana na dhambi kwa muda mrefu hatimaye kunaifanya dhambi ionekane kana kwamba haina madhara. Yeyote anayechagua kujichanganya na watumwa wa Shetani si muda mrefu ataacha kumwogopa bwana wao. Ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yetu tunakutana na majaribu, kama Danieli alivyokutana nayo katika nyumba ya mfalme, tunaweza kuwa na hakika kuwa Mungu atatulinda; lakini ikiwa tunajiweka wenyewe chini ya majaribu tutaanguka chini punde.PKSw 389.1

    Mjaribu anafanya kazi kwa mafanikio zaidi kupitia kwa wale ambao siyo rahisi kufikiria kuwa wako chini ya utawala wake. Watu wenye talanta na elimu wanavutia na kuheshimiwa, kana kwamba sifa hizi zinaweza kuchukua nafasi ya kicho cha Mungu au kuwastahilisha kupata fadhila ya Mungu. Talanta na ustaraabu, vikichukuliwa vyenyewe kama vilivyo, ni zawadi za Mungu; lakini zawadi hizi zikitumiwa kuziba nafasi ya utakatifu, wakati, badala ya kuzileta roho karibu na Mungu, zinazipeleka roho mbali Naye, ndipo zinakuwa laana na mtego. Kuna wazo ambalo watu wengi wanalo kuwa cho chote kinachoonekana kuwa na sura ya ukarimu au ustaarabu lazima, kwa namna fulani, kiwe upande wa Kristo. Hakuna kosa kubwa kama hilo. Sifa hizi zinapasa kuwa sehemu ya maisha ya kila Mkriso, kwa kuwa zinaleta mvuto mkubwa kwa ajili ya dini ya kweli; lakini inapasa zisalimishwe kikamilifu kwa Mungu, kinyume chake zinakuwa pia nguvu ya uovu. Watu wengi ambao wana akili iliyokuzwa na tabia inayovutia, ambao hawawezi kushiriki katika tendo lo lote lile linalojulikana kuwa ni tendo la kukosa uadilifu, ni vyombo vilivyonolewa katika mikono ya Shetani. Mvuto na mfano wake wa tabia iliyofichika, ya udanganyifu, unamfanya kuwa adui wa hatari zaidi kwa kazi ya Kristo kuliko wale ambao hawana elimu na hawana uzoefu mwingi.PKSw 389.2

    Kwa maombi mengi na kumtegemea Mungu, Sulemani alipata hekima iliyoleta mshangao na mvuto mkubwa ulimwenguni. Lakini alipogeuka na kuacha Chimbuko la nguvu zake, akasonga mbele akijitegemea mwenyewe, aliangushwa na majaribu. Ndipo nguvu za ajabu zilizowekwa juu ya mwenye hekima huyu zilimfanya wakala mwenye ufanisi mkubwa wa adui wa roho.PKSw 389.3

    Shetani anapotafuta daima kuwapofusha akili zao wasiuone ukweli huu, inawapasa Wakristo wasisahau kamwe kuwa “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 6:12). Onyo lililovuviwa linatoa sauti katika karne zote hadi wakati wetu: “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze” (1 Peter 5:8). “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani” (Waefeso 6:11).PKSw 389.4

    Tangu nyakati za Adamu hadi wakati wetu, adui yetu mkubwa amekuwa akitumia nguvu yake kuonea kuangamiza. Kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya kampeni ya mwisho dhidi ya kanisa. Wote wanaotafuta kumfuata Yesu wataingia katika migogoro dhidi ya adui huyu asiyechoka. Kwa kadiri Mkristo anavyokaribia zaidi kufanana na sura wa Mungu, ndivyo atakavyokuwa mlengwa mkubwa zaidi wa mashambulizi ya Shetani. Wote wanaojishughulisha na kazi ya Mungu, wakitafuta kufunua udanganyifu wa Ibilisi na kumwasilisha Kristo mbele ya watu, ataweza kujiunga katika ushuhuda wa Paulo, ambapo anaeleza juu ya kumtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote wa akili, kwa machozi na majaribu mengi.PKSw 390.1

    Shetani alimshambulia Kristo kwa majaribu makali na yaliyojaa hila, lakini alishindwa katika kila pambano. Vita vile vilipiganwa kwa kwa ajili yetu; ushindi ule unatuwezesha tushinde. Kristo atatoa nguvu kwa wote wanaoitafuta. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kushindwa na Shetani bila ridhaa yake. Mjaribu hana mamlaka ya kutawala nia au kumlazimisha mtu atende dhambi. Anaweza kuudhi, lakini hawezi kuchafua. Anaweza kusababisha uchungu, lakini hawezi kusababisha uchafu. Ukweli kuwa Kristo ameshinda unapaswa kuwahamasisha wafuasi Wake kuwa na ujasiri wa kupigana kiume vita dhidi ya dhambi na Shetani. PKSw 390.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents