Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Alikuwa Mtangulizi Katika Matengenezo

    Kwa maongozi ya Mungu, Luther alikusudia kuzuru Rumi. Kuachiwa kosa (indulgence) kulikuwa kumeahidiwa na Papa kwa wote ambao wangepanda kwa magoti ngazi ile iliyoitwa “ Pilate’s Stair case.’’ Siku moja, Luther alipokuwa akitimiza tendo hilo la kutembea kwa magoti, mara akasikia sauti kama sauti ya ngurumo ikimwambia hivi, “Mwenye haki ataishi kwa imani!” Kwa aibu na woga, akasimama mara, akatoka hima pale alipofanya tendo lile la upuzi. Hakuyasahau kamwe maneno ya fungu lile. Tangu wakati ule alifahamu zaidi udanganyifu wa kuamini kazi za kibinadamu kwa kuleta wokovu, na haja ya kuamini daima juu ya wema wa Kristo. Macho yake yalikuwa yamefumbuliwa, na hayakuweza kufumbwa tena asiyafahamu madanganyifu mabaya ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi. Alipogeuza uso wake kutoka kwa mji wa Rumi arudi Ugermani, moyo wake pia ulikuwa umeanza kugeuka kutoka kwa kanisa la Rumi. Tangu wakati ule utengano ule ulizidi kuongezeka, mpaka akatengana kabisa na kanisa la Kirumi.VK 36.3

    Baada ya kurudi kwake kutoka Rumi, Luther alipata daraja ya kuwa Mtaalam wa Biblia (Doctor of Divinity) katika kile Chuo Kikuu cha Wittenberg. Sasa alikuwa na nafasi ya kujitoa kabisa, zaidi ya zamani, kwa Maandiko Mtakatifu aliyoyapenda. Alikuwa ameweka nadhiri kusoma kwa uangalifu, na kulihubiri Neno la Mungu hasa, lisilochanganywa na maneno ya mapapa, kwa juhudi katika siku zote za maisha yake. Hakuwa tena kama “monk” wa kawaida, au mwalimu mkuu wa kawaida, bali akawa mwalimu mkuu wa Biblia. Alikuwa ameitwa kuwa mchunga kwa kuwalislia watu wa kundi la Mungu ambao walikuwa na njaa ya kusikia Neno la kweli. Alitangaza kwa uthabiti ya kwamba haiwapasi Wakristo kuyapokea mafundisho mengine zaidi ya yale yaliyoandikwa katika Maandiko Matakatifu. Maneno haya yalisbambulia kabisa mafundisho ya utawala wa mapapa. Yalikuwa maneno yaliyoonekana kuwa asili kabisa ya Matengenezo ya dini.VK 37.1

    Luther alianza kwa ujasiri kujionyesha ya kwamba yeye ni mtetezi wa ukweli. Aliposimama kwenye mimbara, sauti yake ilisikika ikitoa maonyo makuu na ya ajabu. Aliwaambia watu jinsi dhambi inavyomchukiza Mungu, na akawafundisha ya kwamba haiwezekani kwa mwanadamu, kwa matendo yake mwenyewe, kupunguza makosa wala kuepukana na adhabu ya dhambi. Hakuna kitu cho chote kinachoweza kumwokoa mwenye dhambi isipokuwa kutubu na kumwamini Kristo. Neema ya Kristo haiwezi kununuliwa; hutolewa bure pasipo gharama. Luther aliwashauri watu wasinunue vyeti vya kuachiliwa dhambi (indulgence), lakini kwa imani wamtazamie Mwokozi aliyesulibiwa. Alisimulia jinsi alivyopata uchungu na maumivu maishani mwake, alipojidhilisha na kufanya mambo yaliyokuwa kama adhabu ya makosa yake, mambo ambayo yalikuwa bure kwa kujipasisha wokovu; tena aliwahakikishia wasikilizaji wake ya kwamba alipata amani na furaha kwa vile alivyoacha kujitegemea mwenyewe na kumwamini Kristo peke yake.VK 38.1

    Mafundisho ya Luther valiwavuta wengi walioelimika katika nchi yote ya Ugermani. Mafundisho na mahubiri yake yalileta mwanga uliowaamsha na kumulika roho za watu maelfu. Imani kuu ilianza kuingia badala ya urafiki uliokuwa umeenea kanisani kwa miaka mingi. Kila mara watu walikuwa wakipoteza tumaini lao juu ya mambo ya ushirikina ya Kirumi. Nia ya kuchukia mambo yo yote yasiyotoka kwa papa, ilianza kupungua. Neno la Mungu, ambalo kwalo Luther alitegemeza mafundisho yake yote na madai yake yote, lilikuwa upanga ukatao kuwili, likiikata mioyo ya watu. Kila mahali kulikuwa na hamu ya maendeleo katika mambo ya kiroho. Po pote palikuwa na njaa na kiu ya haki kwa namna isivyokuwa katika vizazi vingi tangu zamani. Watu, ambao kwa miaka mingi walikuwa wakiongozwa kutumaini ibada na kawaida za kibinadamu na wapatanishi wa kibinadamu, wakaanza kugeuka na kutubu na kumwamini Kristo aliyesulibiwa.VK 38.2

    Maandiko na mafundisho ya yule Mtengenezaji yalikuwa yakienea katika mataifa yote walio Wakristo. Kazi yake ikaenea mpaka nchi za Switzerland na Holland. Katika Uingereza mafundisho yake yalipokewa na kukubaliwa kuwa ni maneno ya uhai. Ukweli ukaenea pia hata nchi za Belgium na Italia. Watu maelfu walikuwa kama watu walioamka kutoka hali ya kuzimia na kupata furaha na tumaini kwa kuishi maisha ya imani kwa Mungu.VK 39.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents