Sura Ya Kumi Na Nne - Imani Juu Ya Kuongea Na Mizimu
*****
IMANI ya kwamba mwanadamu ana roho isiyoweza kufa imefanya njia tayari kwa dini ya siku hizi ya kuongea na mizimu. Ikiwa ni kweli ya kuwa wafu hukubaliwa kwenda mbele za Mungu na malaika watakatifu, na kupewa maarifa yanayozidi yale waliyokuwa nayo zamani, je, wasingeweza kurudi duniani kuwafundisha walio hai? Wale wanaoamini ya kama wanadamu wanaendelea kuishi peponi baada ya kufa, wanawezaje kukataa mafundisho ya uongo yanayokuja kwao kama ni nuru ya Mungu inayoletwa na pepo zilizotukuzwa? Hapa kuna njia ambayo watu hudhani ya kwamba ni takatifu lakini hutumiwa na Shetani ili ayatimize makusudi yake. Malaika waovu wanaofanya mapenzi ya Shetani huonekana kuwa ni wajumbe watokao kuzimuni. Hapo Shetani anapojidai ya kwamba anawawezesha walio hai kuzungumza na wafu, ndipo anapotumia uwezo wake wa giza kwa kuwadanganya katika fikara zao.VK 98.1
Shetani ana uwezo hata kufanya watu watokewe na mifano ya rafiki zao waliokwisha fariki. Mfano huu ni kamili; maneno na sauti huigizwa sawasawa. Wengi hufarijiwa kwa kuamini ya kwamba wapenzi wao wamo katika hali ya heri mbinguni, na bila kutambua ya kwamba wamo hatarini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.VK 98.2
Watu wanapokwisha kuongozwa kuamini ya kwamba wafu hurudi kweli na kuongea nao, Shetani huwafanya watokelewe na wale walioshuka kaburini pasipo kuwa tayari kumlaki Mungu. Hao nao huanza kujidai ya kwamba wako katika hali ya heri mbinguni, na ya kwamba wana madaraka ya heshima huko, na hivi fundisho la uongo huenczwa ya kwamba hakuna tofauti baina ya wenye haki na waovu. Wadanganyifu hawa wanaojidai kwamba hutoka kuzimuni pengine hulcta maonyo na mashauri yaonekanayo kuwa ni ya kweli. Ndipo wakisha kuwavuta watu wawasadiki, huanza kulcta mafundisho yanayoharibu imani ya watu katika Maandiko Matakatifu. Kwa kuonekana ya kwamba hujisliughulisha sana kwa mambo mema ya wenzao hapa duniani, hueneza mafundisho mabaya sana. Kwa jinsi ambavyo mara nyingine husema yaliyo kweli, na mara nyingine wanaweza kuyabashiri mambo yajayo maneno yao huonekana kuwa ya maana na mafundisho yao ya uongo hukubaliwa na watu wengi mara moja na kuaminiwa kabisa kana kwamba ni kweli ya Mungu sawa na mambo makubwa matakatifu ya Biblia. Sheria ya Mungu haifuatwi, roho ya neema hudharauliwa, na damu ya agano huhesabiwa kuwa kitu kisicho kitakatifu. Pepo hukana kabisa ya kwamba Kristo si Mungu, hata humhesabu Muumbaji kuwa sawa nao. Hivi kwa hila nyingine, mwasi mkuu huendelea kufanya vita vile na Mungu alivyoanzisha mbinguni na kufanya duniani tangu miaka elfu sita.VK 99.1
Watu wengi hujaribu kueleza sababu ya maonyesho ya uwezo wa pepo wakisema ya kwamba hufanyika kwa hila au kwa matendo ya kiinimacho yanayofanywa na yule kijumbe wa pepo. Ingawa ni kweli ya kama mara nyingine watu wapata kudanganvwa va knwa matendo va kiini- macho ndiyo maonyesho hakika ya pepo, lakini kumekuwa na matendo mengine ambayo yameonekana dhahiri kwamba yametendeka kwa uwezo usio wa kibinadamu. Mabisho ya ajabu iliyokuwa mwanzo wa dini ya siku hizi ya kuamini juu ya kuongea na mizimu haikufanywa na werevu na hila ya kibinadamu, lakini ni matendo halisi ya malaika waovu, na kwa tendo lile walianzisha fundisho ambalo limewadanganya watu wengi na kuwaharibu. Wengi watashikwa kwa ajili ya kuamini ya kama nguvu za pepo ni ujanja wa wanadamu tu; na kama wakiona maonyesho na matendo ya pepo, mambo ambayo hawana budi kukubali ya kwamba yametendeka na nguvu isiyo ya kibinadamu, watadanganywa na kuamini ya kwamba mambo hayo yalifanywa na uwezo mkuu wa Mungu.VK 99.2
Watu hawa hawafikiri jinsi Maandiko Matakatifu yasemavyo juu ya maajabu yafanywayo na Shetani na wafanyi kazi wake. Waganga wa Farao waliyaigiza matendo ya Mungu kwa usaidizi wa Shetani. Mtume Yohana, akieleza uwezo wa kuifanya miujiza katika siku za mwisho, asema hivi: “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya.” Ufunuo 13:13,14. Hapa hatuambiwi juu ya ujanja tu. Wanadamu wanadanganywa kwa miujiza ambayo wafanyi kazi wa Shetani wanawezeshwa kuifanya, si mambo tu ambayo wanajisingizia ya kuwa wanaweza kuyafanya.VK 100.1