Muda wa Kukawia
Mwaka wa 1843 ulipopita kabisa bila Yesu kuonekana, wale waliokuwa wakimngoja kwa imani wakawa na shaka na fadhaa kuu. Walakini ingawa waliuona uchungu mkuu wa namna ile, wengi waliendelea kusoma Biblra kwa makini, wakiichunguza bayana ya imani yao, na pia waliyachunguza sana maneno ya unabii kusudi wapate nuru zaidi. Ushuhuda wa Biblia juu ya maoni yao ulionekana kuwa dhahiri na uliothibitika. Dalili ambazo zilionekana wazi zilionyesha ya kuwa kuja kwa Yesu mara ya pili kulikaribia sana. Wale waarninio hawakuweza kuueleza sababu ya jambo lile lililowatilia uchungu; lakini walifahamu dhahiri ya kuwa Mungu alikuwa amewaongoza katika siku zilizopita.VK 65.4
Imani yao iliimarishwa sana kwa kuyasoma mafungu yale ya Maandiko yaliyoonyesha ya kwamba kutakuwa muda wa kukawia. Mnamo mwaka wa 1842, Roho wa Mungu alimwongoza Charles Fitch apate kuitengeneza ramani ya wakati ule uliotabiriwa na nabii, na ramani ile lihesabiwa na wengi wa Waadventista (wale waliotazamia kuja kwa Kristo) kuwa kama utimizo wa agizo lililotolewa na nabii Habakuki kwa maneno haya, “Iandike njozi, ukaifanye iwe wazi sana katika vibao.” Hakuna hata mmoja aliyeona neno la wakati ule wa kukawia jinsi ulivyotabiriwa katika unabii ule ule. Lakini baada ya uchungu ule kwa kutomwona yule waliyemtazamia, ndipo maana halisi ya maandiko yale ikatambulikana. Hivi ndivyo asemavyo nabii, “Iandike njozi, ukaifanye iwe wazi sana, katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja haitakawia.” Hab. 2:2,3.VK 66.1
Wale waliokuwa wakingoja walifarahi kwa kuwa Yeye aujuaye mwisho tangu mwanzo alikuwa ametazama vizazi, akaona jinsi watakavyoona uchungu, ndipo akawapa maneno ya kuwatia nguvu na tumaini. Kama mafungu ya namna hii yasingalikuwako katika Biblia, yanayoonyesha ya kwamba njia waliyokuwa wameifuata ilikuwa sawa, imani yao ingalipunguka katika siku zile za taabu.VK 66.2
Katika mfano wa wanawali kumi, tunaousoma katika Mathayo 25, mambo yaliyotokea kwa wale waliotazamia kurudi kwa Yesu yameelezwa kwa kufuata mambo yatendekayo katika arusi katika nchi za Mashariki “Ndipo ufalme wa mbingurii utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.” “Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.”VK 67.1
Mabadili yaliyoenea sana duniani baada ya kutangazwa kwa ujumbe wa kwanza, yalilinganishwa na kuondoka kwa wale wanawali; tena kupita kwa wakati wa kumngoja Kristo, na wakati wa uchungu kwa ajili ya kutomwona, haya yote yalionyeshwa kwa kukawia kwa bwana arusi. Baada ya wakati uliotazamiwa kupita, waaminio wa kweli waliendelea kuamini ya kwamba mwisho wa mambo yote ulikuwa umekaribia lakini baadaye kidogo ilionekana ya kwamba walikuwa wakianza kupotewa na juhudi yao na kujitoa kwao kwa kadiri fulani na walikuwa wameanza tayari kuwa katika hali iliyoelezwa katika mfano wa wanawali waliokuwa wakilala usingizi wakati bwana arusi alipo-kawia.VK 67.2
Ushupavu wa dini ulianzishwa mnamo wakati ule. Wengine kati yao waliojidai kuwa waaminio wenye juhudi katika ujumbe huu walianza kulikataa Neno la Mungu kuwa ni kiongozi cha pekee kisichoweza kukosa, na kwa ajili ya kujidai ya kwamba waliongozwa na Roho wa Mungu, walianza kufuata. fikara na maono yao wenyewe. Kuli- kuwa na wengine ambao walionyesha juhudi na ushupavu pasipo kutumia akili, wakiwashutumu wote wasiokubaliana nao kwa matendo yao. Mambo yao na matendo yao ya ushupavu wa dini hayakupendelewa na wingi wa watu waliokuwa wakitazamia kurudi kwa Kristo; na pia matendo ya watu wale yalileta lawama juu ya kazi ya Mungu.VK 67.3
Kuhubiriwa kwa ujumbe wa kwanza katika 1843, na kuhubiriwa kwa kilio cha usiku wa manane katika mwaka wa 1844, kulisaidia kutuliza ushupavu wa dini na mafarakano. Wale waliokuwa wakishirikiana katika mashauri haya walisikilizana; mioyo yao ilijaa upendo wao kwa wao, na kwa Yesu pia, ambaye walikuwa wakimngoja. Imani. ile ile, tumaini lile lile lenye baraka, liliwaweka katika hali ya kutoongozwa na mvuto wo wote wa kibinadamu, ikiwa kama ngao juu ya mashambulio ya Shetani.VK 68.1