Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Kumi Na Tano - Sauti Kuu

    *****

    NILIWAONA malaika wakiruka huko na huko mbinguni, wakishuka duniani, na tena wakipanda mbinguni, wakifanya mambo tayari kwa utimizo wa tokeo fulani lililo kuu. Tena nikamwona malaika mwmgine mwenye mamlaka kuu aliyetumwa ashuke duniani, kusudi aiunganishe sauti yake na ya malaika wa tatu. akatie nguvu na uwezo kwa ujumbe wake. Malaika yule alipewa uwezo mkuu na utukufu, aliposhuka, dunia iliangazwa na utukufu wake. Mwanga uliomfunika malaika huyu ulipenyeza pote alipolia kwa nguvu kwa sauti kuu, “Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.” Ufunuo 18:2VK 106.1

    Ujumbe huu juu ya kuanguka kwa Babeli, jinsi ulivyotolewa na malaika wa pili, umerudiwa hapa, na pia yametajwa mabaya ambayo yamekuwa yakiingia makanisani tangu 1844. Kazi ya malaika huyu imeanzishwa kwa wakati uliofaa na kuungana na kazi Suu ya ujumbe wa malaika wa tatu unapotolewa kwa sauti kuu. Na hivi watu wa Mungu wanatayarishwa wapate kusimama wakati wa majaribu, ambayo yatawapata baada ya siku si nyingi. Naliiona nuru kuu ikiwakalia, wakaungana pamoja kwa kuutangaza ujumbe wa malaika wa tatu kwa ushujaa.VK 106.2

    Malaika wengine walitumwa wapate kumsaidia malaika yule mwenye mamlaka kuu, aliyetoka mbinguni, tena nalisikia sauti iliyokuwa ikienea pote ikisema hivi: “Tokeni kwake. enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufunuo 18:4,5. Ujumbe huu ulionekana ya kwamba uliongezwa juu ya ujumbe wa tatu, ukiungana nao kama vile kilio cha usiku wa manane kilivyoungana na ujumbe wa malaika wa pili katika mwaka wa 1844. Utukufu wa Mungu uliwakalia watakatifu waliovumilia wakingoja, nao wakalitoa onyo la mwisho kwa ushujaa, wakilitangaza anguko la Babeli, na kuwaita watu wa Mungu watoke kwake, kusudi waepukane na hukumu yake ya kutisha.VK 107.1

    Mwanga ule uliowakalia wale waliokuwa wakimngoja Bwana ulipenyeza na kumulika pote, na - wale waliokuwa katika makanisa yaliyopata nuru yo yote,, na ambao hawakusikia na kuzikataa habari zilizoletwa na malaika walatu, watu kama hao waliuitikia wito, wakatoka katika makanisa yale yaliyoanguka. Wengi walikuwa wamepata umri wa watu wazima na kupata kufahamu mambo zaidi tangu malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu walipoanza kutoa habari zao, nao sasa walipewa nuru, na walikuwa na nafasi ya kuchagua uzima au kifo. Wengine walichagua uzima, wakasimama pamoja na wale waliokuwa wakimtazamia Bwana wao na kuzishika amri zake zote. Ujumbe wa tatu ulipaswa kuitimiza kazi yake; na wote walijaribiwa na maneno ya ujumbe ule, na waliokuwa wenye haki walitoka katika dini mbali mbali.VK 107.2

    Uwezo uliotoka juu uliwabidisha waaminifu, na huku maonyesho ya uwezo wa Mungu uliwatia hofu jamaa na raiiki zao wasioamini, na kuwashika wasithubutu kuwazuia wale ambao waiiona ya kwamba walishurutishwa na Roho wa Mungu waifanye kazi yake. Wito wa mwisho ulipelekwa hata kwa watumwa maskini; na wale waliokuwa wakimcha Mungu kati yao waliimba kwa furaha na shangwe kuu wakitazamia kuokolewa kwao. *Twajua ya kwamba itakuwako hali ya utumwa wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili, kwa vile Yohana alivyosema katika kitabu cha Ufunuo 6:15, 16, akisimulia ya kwamba “kila mtumwa, na mwungwana” wataiambia milima na miamba iwaangukie na kuwasitiri “mbele za uso wake veye aketiye juu ya kiti cha enzi.” Matajiri hawakuweza kuwazuia; walishikwa na woga na mshangao. Miujiza ya ajabu ilifanywa, wagonjwa waliponywa, na waaminio walifanya ishara na maajabu mengi. Mkono wa Mungu ulikuwa kazini, na bila kuwa na hofu ya matokeo yake watakatifu wote waliyafuata maoni ya dhamiri zao, wakaungana na wale waliokuwa wakizishika amri zote za Mungu; na kwa uwezo mkuu waliueneza ujumbe wa malaika wa tatu. Naliona ya kwamba ujumbe huu utakoma kwa nguvu na uwezo unaozidi ule wa kilio cha usiku wa manane.VK 107.3

    Watumishi wa Mungu, wakijaa uwezo uliotoka juu na nyuso zao ziking’aa, wakajitoa kabisa kwa Mungu, waliondoka wautangaze ule ujumbe uliotoka mbinguni. Watu waliokuwa wametawanyika katika dini mbali mbali, waliuitikia wito ule, na wateule wa Mungu walitoka mara katika makanisa yale yaliyohukumiwa, kama Luti alivyoondoshwa hima kutoka katika Sodoma kabla ya kuharibiwa kwake. Watu wa Mungu waliongezewa nguvu, na utukufu mkuu uliowafunika kwa wingi ukawatayarisha wapate kuvumilia katika wakati wa majaribu. Kila mahali nalisikia sauti za watu wengi wakisema hivi: “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu; hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ufunuo 14:12.VK 108.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents