Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Nane - Ujumbe Wa Malaika Wa Pili

    *****

    MAKANISA ambayo yalikataa kuupokea ujumbe wa malaika wa kwanza yalikataa nuru iliyotoka mbinguni. Ujumbe ule ulipelekwa kwa neema kusudi uwaamshe watu ili waitambue hali yao hasa ya kupenda anasa za dunia na kuasi, wapate kujitayarisha kumlaki Ewana wao.VK 63.1

    Ujumbe wa malaika wa kwanza ulitolewa kwa minajili ya kulitenga kanisa la Kristo na mvuto mpotovu wa dunia. Lakini kwa watu wengine, hata wale waliojidai kuwa ni Wakristo, mambo ya dunia ya kupendeza yalikuwa na mvuto wenye nguvu zaidi ya mambo ya mbinguni. Walichagua kuisikiliza sauti na mashauri ya kidunia wakauacha ujumbe huu mzito na wenye maana.VK 63.2

    Mungu huutoa mwanga kusudi ukuzwe na kutiiwa, si kwamba udharauliwe na kukataliwa. Mwanga unaotolewa na Mungu huwa giza kwa wale wasioujali. Roho ya Mungu anapoacha kuuingiza ukweli katika mioyo ya watu, ndipo kusikia neno la Mungu huwa bure, na mahubiri yote huwa kama kitu kisicho na faida.VK 63.3

    Makanisa yalipolidharau shauri la Mungu kwa kuukataa ujumbe juu ya marejeo ya Kristo, Bwana naye akawakataa. Malaika wa kwanza alifuatwa na wa pili ambaye alipaaza sauti akisema, “Umeanguka, umeanguka, Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake.” Ufunuo 14:8. Watu wale waliokuwa wakiyatazamia marejeo ya Yesu walifahamu ya kwamba ujumbe huu ulitolewa kwa kutangaza kuanguka kwa makanisa kwa njia ya kiroho, kwa sababu yaliukataa ujumbe wa kwanza. Mbiu hii, “Umeanguka Babeli,’’ ilitolewa mnamo 1844» na watu wapata elfu hamsini waliaacha makanisa yale kwa ajili ya maneno haya.VK 63.4

    Wale watu waliouhubiri ujumbe wa kwanza hawakuwa na kusudi la kuleta utengano katika makanisa, wala hawakutazamia kufanya hivyo, tena hawakufikiri kuanzisha shirika mpya. William Miller alisema hivi, “Katika kazi zangu zote, sikuwa na hamu wala fikara yo yote kuanzisha dini nyingine zaidi ya zile zilizopo, wala kuifanikisha dini fulani kwa ajili ya hasara ya dini nyingine. Nalinuia kuwafanikisha wote. Kwa vile nilivyofikiri ya kwamba Wakristo wote wangependezwa kuyatazamia marejeo ya Kristo, ingawa wengine hawawezi kupatana nami katika maoni yangu yote sikudhani ya kwamba wangekuwa na nia mbaya juu yao wanaoshikilia fundisho hili, na kwa hiyo sikuona ya kwamba itakuwa ni lazima kutengana na kuweka mikutano mbali mbali. Kusudi langu kuu lilikuwa kuwageuza watu kwa Mungu, kuwaambia walimwengu juu ya hukumu ijayo, na kuwavuta wenzangu wapate kuitayarisha mioyo yao kwa namna itakavyowawezesha kumlaki Mungu kwa amani. Wingi wa watu walioongoka kwa ajili ya kazi yangu waliungana na makanisa mbali mbali yaliyokuwako. Watu wengine waliponijia wakiniuliza juu ya mambo valiyowapasa kufanya, kila mara naliwajibu nikiwaambia ili waende po pote walipopendezwa kwenda; wala sikuwakatia shauri juu ya dini yo yote kwa kusifu madhehebu fulani zaidi ya nyingine.”VK 64.1

    Kwa muda fulani makanisa mengi yalimsikiliza kwa furaha, lakini kwa jinsi walivyokataa kuisadiki habari ya marejeo ya Kristo, walikuwa na hamu ya kuyakanusha mafundisho yote yaliyohusiana na jambo lile. Wale waliokubali fundisho lile wakawa katika hali ya taabu na mahangaiko ya moyoni. Waliyapenda makanisa yao, na hawakupendezwa kutengana nayo; lakini kwa jinsi. walivyochekelewa na kudhulumiwa, na kukatazwa wasiseme juu ya tumaini lao, wala kuihudhuria mikutano inapohubiriwa habari za kuja kwa Bwana, hatimaye watu wengi waliondoka wakaitupa ile nira iliyokuwa imewekwa juu yao.VK 65.1

    Wale watu waliokuwa wakiyatazamia marejeo ya Kristo, walipoona ya kwamba makanisa yaliukataa ushuhuda wa Neno la Mungu, hawakuyahesabu tena kuwa ni kanisa la Kristo ambaye ni “nguzo na msingi wa kwdi,” na maneno haya, “Umeanguka Babeli,” yalipoanza kutangazwa, waliona kwamba walifanya haki kwa vile walivyojitenga na ushirika wa makanisa yaliyokuwako zamani.VK 65.2

    Tangu ujumbe ule wa kwanza ulipokataliwa, mageuzi ya kusikitisha sana yameonekana katika makanisa. Ukweli unapodharauliwa, ndipo mambo ya uongo yanapopokelewa na kukuzwa. Upendo kwa Mungu na imani kwa Neno lake zimepoa. Makanisa yamemhuzunisha Roho wa Bwana, na kwa kadiri kubwa sana Roho wan Mungu ameondolewa.VK 65.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents