Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Patakatifu pa Duniani na pa Mbinguni

    Katika uchunguzi wao waliona ya kwamba patakatifu pa duniani, palipojengwa na Musa kwa amri ya Mungu, kwa kuufuata mfano aliopewa mlimani, palikuwa kania “mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa.” yaani patakatifu pake pawili palikuwa “nakala za mambo yaliyo mbinguni;” na ya kwamba Kristo Ktihani wetu Mkuu, ndiye “mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu na ya kwamba “Kristo hakuingia patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni paMungu kwa ajili yetu.” Ebr. 9:9, 23; 8:2; 9:24.VK 78.1

    Patakatifu pa mbinguni, ambapo Yesu anahudumu kwa ajili yetu, ndipo patakatifu pa kwanza, na palipo pakuu, ambapo palipojengwa na Musa palikuwa mfano wake. Kwa jinsi ambavyo patakatifu pa duniani palikuwa na sehemu mbili, yaani patakatifu na patakatifu pa patakatifu (au patakatifu mno), vivyo na patakatifu pa mbinguni pana patakatifu pawili. Sanduku la agano ambamo kuna sheria ya Mungu, na madhabahu ya uvumba, na vifaa vingine vilivyopatikana katika patakatifu pa duniani, vilikuwa mifano ya vile vilivyomc katika patakatifu pa mbinguni. Mtume Yohana alipokuwa katika njozi yake takatifu, aliruhusiwa aingie mbinguni, na pale alipata kuziona taa saba za moto na madhahabu ya uvumba, na “Hekalu ya Mungu ilipofunguliwa,” ndipo akaona “sanduku la Agano.” Ufunuo 4:5; 8:3; 11:19.VK 78.2

    Wale waliokuwa wakiitafuta kweli waliyapata mambo yaliyowathibitishia kabisa ya kwamba pana patakatifu mbinguni. Musa alipajenga patakatifu pa duniani kwa mfano alioonyeshwa. Paulo aliarifu ya kwamba mfano ule ndio uliokuwa patakatifu pa asili palipo mbinguni. Ebr.8:2,5.) Yohana pia alishuhudia ya kwamba alipaona mbinguni.VK 78.3

    Mnamo mwisho wa siku 2,300 katika 184-4, hakuna patakatifu palipokwisha kuwako duniani kwa kame nyingi; kwa hiyo yamkini patakatifu pa mbinguni ndipo palipoonyeshwa kwa maneno haya, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Lakini patakatifu pa mbinguni pangewezaje kuwa na haja ya kutakaswa? Wale watu waliokuwa wakivachunguza maneno ya unabii walianza kurudia Maandiko tena, wakaona ya kwamba kutakaswa kwa patakatifu hakukuwa kuondoa uchafu wo wote unaoonekana, kwa kuwa utakaso ulipasa kufanywa na damu, na kwa hiyo lazima kuwe kutakaswa dhambi. Hivi ndivyo asemavyo mtume: “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo (yaani damu ya wanyama), lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo (yaani damu yenye thamani ya Kristo).” Ebr. 9:23.VK 79.1

    Kwa kusudi la kupata ujuzi kamili wa utakaso uliotajwa katika maneno ya unabii, iliwapasa kufahamu namna ya huduma inayofanyika katika patakatifu pa mbinguni. Huduma hii ya mbinguni iliweza kufahamiwa tu kwa kujifunza juu ya huduma ya patakatifu pa duniani; kwa sababu Paulo asema ya kwamba makuhani waliohudumu katika patakatifu pa duniani walihudumu “kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni.” Ebr. 8:5.VK 79.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents