Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Luther Ajitenga na Rumi

    Kanisa la Kirumi lilifikiri kumwua Luther, lakini Mungu alimlinda. Mafundisho yake yalienea pote—katika nyumba za watauwa, katika nyumba za watu, katika ngome za watu mashuhuri, katika vyuo vikuu, katika majumba ya kifalme; na watu mashuhuri waliondoka kila upande ili wamsaidie.VK 39.2

    Katika barua yake aliyomwandikia mtawala na wakuu wa Ugermani juu ya Matengenezo ya Ukristo, Luther aliandika hivi juu ya Papa: “Ni jambo la kuchukiza sana kumwona mtu anayejiita mjumbe atawalaye mahali pake Kristo, akifanya fahari ambayo hakuna mtawala anayeweza kufanya kufanana nayo. Je. hii maana yake ni kuwa kama maskini Yesu, au mnyenyekevu Petro? Wanadai wakisema ya kwamba yeye ni bwana-wa dunia! Lakini Kristo, ambaye Papa anajidai kwamba yeye ni mjumbe wake, alisema hivi, ‘Ufalme wangu si wa dunia hii.’ Je, mamlaka ya mjumbe inaweza kunena zaidi ya mkubwa wake?”VK 39.3

    Aliandika hivi juu ya vyuo vikuu: “Ninaogopa sana ya kwamba vyuo vikuu vitakuwa milango mikubwa ya jehanum, visipofanva juhudi sana katika kueleza Maandiko Matakatifu, na kuyaimarisha mioyoni mwa vijana. Natoa shauri ya kwamba mtu ye vote asimpeleke mtoto wake katika skuli ambapo Biblia haifundishwi kama somo kuu. Kila skuli ambapo watu hawashughuliki kila mara na Neno la Mungu haina budi kupotoka kabisa.”VK 40.1

    Maneno haya yalienezwa pote katika Ugermani. na yakawa na nguvu sana kwa kuvuta mioyo ya watu. Taifa lile lote liliamshwa na kushindania lile jambo la matengenezo. Adui za Luther, walikuwa na hamu kuu ya kulipa kisasi, tena walimshurutisha Papa amfanyie mashauri makali. Amri ilitolewa ili mafundisho yake yakatazwe kabisa. Luther na wafuasi wake walipewa siku sitini wapate kugeuka, na wakikataa, basi wao wote wataharimishwa kanisani.VK 40.2

    Tangazo la Papa lilipomfikia Luther, alisema hivi: “Ninaidharau sana amri hiyo, tena nitaishambulia. kwani haimstahi Mungu, ni ya uongo . . . Kristo mwenyewe amehukumiwa katika amri hiyo. . . . Nafurahi kuyachukua mabaya ya namna hii kwa ajili ya kazi iliyo bora, yaani ya Mungu. Naona uhuru mkuu sana moyoni mwangu; kuwa sasa nimetambua ya kwamba Papa ni yule mwongo aliyempinga Kristo; na ya kwamba kiti chake cha enzi ni kiti cha Shetani mwenyewe.”VK 40.3

    Lakini neno la askofu mkubwa wa Rumi bado lilikuwa na nguvu. Alitumia gereza, ukatili, na upanga kama silaha zilizotumiwa kwa kuwatiisha watu. Kila jambo lililotendeka lilikuwa kana kwamba kazi ya Luther ilikaribia kukomeshwa. Wadhaifu na wenyc hofu walitetemeka mbele ya amri ya Papa, na inirawa katika mahali pengi watu walishiriki katika maono ya Luther, watu wengi waliona ya kwamba haifai kujihatarisha maisha kwa ajili ya kutengeneza kwa upya mambo ya kanisa.VK 41.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents