Habari ya Maisha ya Wayahudi Yarudiwa
Nalielekezwa kwa mambo yaliyotokea zamani katika siku ambazo kuja kwa Kristo mara ya kwanza kulitangazwa. Yohana alitumwa katika roho na nguvu za Eliya ili aitengeneze njia ya Yesu. Wale waliokataa ushuhuda wa Yohana hawakufaidiwa hata kidogo na mafundisho ya Yesu. Kukataa kwao kwa ujumbe uliotabiri kuja kwake kulifanya wasiweze kukubali hata ushuhuda ulio thabiti ya kwamba Yeye ndiye Masiya. Shetani alizidi kuwaongoza wale walioukataa ujumbe wa Yohana wapate kuasi zaidi, hata wamkatae na kumsulibisha Kristo. Kwa kufanya hivyo, walijiweka katika hali ambayo kwayo hawakuweza kupata mbaraka ule siku ya Pentekote. ambao ungaliwafundisha njia iendayo hata patakatifu pa mbinguni.VK 89.2
Kupasuliwa kwa pazia la hekalu kulionyesha ya kwamba dhabihu na sadaka zao zisingekubaliwa tena. Dhabihu kuu ilikwisha kutolewa na kukubaliwa. na Roho Mtakatifu aliyeshuka siku ya Pentekote alielekeza nia za wanafunzi kwa patakatifu pa mbinguni badala ya patakatifu pa duniani. Yesu alikuwa ameingia katika patakatifu pa mbinguni kwa ajili ya damu yake. kuwamiminia wanafunzi wake mibaraka ya upatanishi wake. Lakini Wayahudi waliachwa katika giza nene. Walipotewa na nuru yote ambayo wangaliweza kupokea juu ya azimio la wokovu, wakadumu kuziamini dhabihu na sadaka zao zisizo na faida yo yote. Patakatifu pa mbinguni palikuwa pamechukua nafasi ya patakatifu pa duniani, walakini hawakulifahamu geuzo hilo. Kwa sababu hiyo hawakuweza kufaidiwa na kazi ya Yesu ya kuwaombea watu katika patakatifu.VK 89.3
Kuna watu wengi wanaochukizwa mno kwa jinsi Wayahudi walivyomkataa Kristo na kumsulibisha; na wanaposoma jinsi alivyotendewa vibaya na kuaibishwa, wanafikiri ya kwamba wanampenda Yesu, na ya kwamba wenyewe wasingalimkana kama Petro alivyofanya, wala kumsulibisha kama walivyofanya Wayahudi. Lakini Mungu, asomaye fikira za mioyo ya watu wote, amekuwa akijaribu upendo wao wanaojidai ya kwamba wanampenda Yesu.VK 90.1
Wote wa mbinguni walishughulika sana katika kutazama jinsi watu walivyoupokea ujumbe wa malaika wa kwanza. Lakini wengi waliojidai ya kwamba walimpenda Yesu, na ambao walitoka machozi waliposoma habari za msalaba, waliidharau habari njema ya kuja kwake. Badala ya kuupokea ujumbe huu kwa furaha; walitangaza ya kwamba ni udanganyifu mtupu. Waliwachukia wale waliopenda kufunuliwa kwake, wakawazuia wasiingie katika makanisa. Wale waliokanusha ujumbe wa kwanza hawa-kuweza kufaidiwa na ujumbe wapili; wala hawakufaidiwa na kilio cha usiku wa manane, ambacho kilikuwa kimekusudiwa kuwatayarisha kwa kuingia na Yesu kwa imani katika patakatifu mno palipo mbinguni. Na kwa kuukataa ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili. wamezitia giza akili zao, hata wasiweze kuiona nuru katika ujumbe wa malaika wa tatu, ambao unaongoza hata patakatifu pa patakatifu.VK 90.2